Wewe mpaka leo shetani asili yake hujui ingawa tulishakuelewesha
Hii ni mara ya mwisho kukufundisha, wacha biblia iseme shetani alikuwa nani katika Ezekiel 28:13-15.
Soma uelewa shetani alikuwa nani
[emoji116]
13. Ulikuwa katika Edeni, bustani ya Mungu. Kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, zabarijadi, topazi na yaspi; krisolito, shohamu na yashefi; yakuti, feruzi na zumaridi; nao ufundi wa viwekeo na wa vitundu vyako ulikuwa wa dhahabu ndani yako. Vilitayarishwa katika siku ya kuumbwa kwako. 14 Wewe ndiye kerubi aliyetiwa mafuta anayefunika, nami nimekuweka wewe. Ulikuwa katika mlima mtakatifu wa Mungu. Ulitembea katikati ya mawe yenye moto. 15 Hukuwa na kosa katika njia zako tangu siku ya kuumbwa kwako mpaka ukosefu wa uadilifu ulipoonekana ndani yako."