Adhabu ya kunyongwa hadi kufa ndio Siri ya uchumi mkubwa duniani

Sasa hivi tunaandika humu kama mchezo lakini hakika maandishi yetu haya yatakuja kutafutwa kwenye archives ili yasomwe Na wajukuu wetu kama hatua mojawapo ya ukombozi wa taifa kiuchumi.

Ni heri ya anaetafuta wawekezaji kuliko anayetafuta misaada, hakuna cha bure ndugu zangu tuambine ukweli. Vya bure vina madhara, vina ndoana nyingi sana ambazo zitalinasa taifa kooni huko mbele ya safari, ni heri watoto Na wajukuu wetu wakute msululu wa orodha ndefu za majina ya watanzania wenzetu tuliowanyonga sisi wenyewe kwa makosa ya ufisadi, rushwa Na uzembe wa kuingia mikataba mibovu kuliko kukuta msululu wa watu Na mataifa wanaotudai. Watatudharau sana kama tunavyowabeza Leo akina Chief Mangungo wa Msovero dhidi ya akina Karl Peters.
 
Unapokuwa na adhabu kubwa kama ya kunyonga ni lazima uwe na penal codes makini za support , ili usinyonge watu kwa petty crimes
Uhujumu uchumi kwetu ni neno pana sana ikiwemo kuharibu mali ya umma , yani unaweza ukaigonga nguzo ya waya ya Tanesco na hapo hapo ikaunekana unataka kuhujumu uchumi
 
Ni heri ukosee kuchukua hatua kuliko kuacha kuchukua hatua. Wazungu wamefika huko kwa kuchukua hatua makosa madogo ya kudhaniwa Na kusingiziwa tu. Ndio maana hata vitabu vya dini viliandika kuwa dhambi ni dhambi hakuna dhambi ndogo. Wazungu wanapopigana vita wanaweza kupiga Bomu hata hospitali, nia yao ni kuacha uzembe wa kufikiria kuwa adui hawezi kujificha kwenye hospitali, kanisani, msikitini, shuleni au kwenye msafara wa maharusi.

Watoto wangu wote wamesoma kwakuwa nilikuwa sipuuzii taarifa hata kama walisingiziwa tu kuhusu tabia zao mbaya zisizoendana Na shule. Mimi nilitoa adhabu stahili bila kusema nikweli au sio kweli kafanya. Ukianza kutenga makosa utashindwa tu.
 
Mafisadi wanyongwe Hadharani...

Tena kama wale hasa walio liingiza taifa kwenye mikataba Mibovu kama ile ya Gass ya Mtwara asee...



Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Tunawasifu wachina wanachapa Kazi Na uchumi wao unapaa, aisei, hali hiyo haikutokea tu, IPO machinery inayosukuma hayo yatokee. Sisi hapa tunashindwa kumsogeza machinga atoke kwenye njia zinazotumiwa na watanzania wenzao kupea ajali za magari. Eti kumwambia machinga sogea kuepusha ajali kwa wenzako nako kunahitaji mjadala mrefu, kumnyonga MTU aliyeiba twiga mzima mchana kweupe na kumpakia kwenye ndege kupeleka uarabuni tutaweza?
 
Wapeane wao tuu najua akija mwamba mmoja atatutengeneza tuu vyema
 
Hata hiyo fafanuzi uliyo toa MAZUZU BADO AWAJAKUELEWA
 
Huyu Mama anataka kuwaonyesha wanaume walichokuwa wakikosea kwa miaka 60 mfululizo. Shida yetu wananchi ilikuwa kuwachagua watu maskini sana kwenye ukoo kuwa viongozi. Mtu maskini anafikiria na kutenda kimaskini hata ofisini. Anafikiria matumbo ya watu Badala ya tumbo kubwa la nchi.
 
Na maandiko matakatifu yanasema hivi,
"Shetani hawezi kumfukuza shetani mwenzake"
 
Na maandiko matakatifu yanasema hivi,
"Shetani hawezi kumfukuza shetani mwenzake"
Lakini, dawa ya moto ni moto, na mwizi anakamatwa na mwizi mwenzie, mchawi mpe mwanao a Lee.
 
Lakini, dawa ya moto ni moto, na mwizi anakamatwa na mwizi mwenzie, mchawi mpe mwanao a Lee.
Kwa misemo hii ni rahisi kuingia choo cha jinsia tofauti.

Sijawahi kuona gari ya zimamito ikibeba moto kwenda kuzima moto ila maji.
 
Kwa misemo hii ni rahisi kuingia choo cha jinsia tofauti.

Sijawahi kuona gari ya zimamito ikibeba moto kwenda kuzima moto ila maji.
Shida iko hivi, maji ni mbabe wa moto na moto ni mbabe kwa maji , yaani hakuna mbabe kati ya maji na moto. Yaani moto unayakausha maji na kutobakiza hata tone na maji yanauzima moto na kutobakiza hata cheche moja.
 
Mkuu na siku zote ukiona mtu anazungumzia Kinga ujue ni muovu
Unahubiri kufungua makama nyingi za mafisi ili wahukumiwe haraka sana lakini wakati huohuo unajiongezea mwenyewe na rafiki zako kinga ya kutokushitakiwa kwenye mahakama hizo, na wanyonge wanageuka mazuzu wanashangilia mkombozi wa wanyonge kaletwa na Mungu. Kweli wajinga hawaishi hata siku ya kiyama watakuwepo tu!!
 
Umenena vyema Tza fisadi afungwi ulipa faini mbuzi kibaka ufungwa sababu hana pesa ya kumuhonga hakimu.
 
Hii nchi inatafunwa hatari tunaopiga kelele ni sisi tusiopata nafasi
 
Pia Nyerere alikuwa akiwahamisha wizara wezi eti ndo adhabu mtu kaiba anahamishwa.
 
Sasa tunaanza kuongea vitu vya maana , kongole kwa wote watakaounga mkono hoja hii !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…