Adhabu ya kunyongwa hadi kufa ndio Siri ya uchumi mkubwa duniani

Lile jiwe lilikuwa fisad8 kubwa!
Tumeliwa Sana Ndugu Zangu
Tumechezewa Sana Ndugu Zangu
Tumelaliwa Mno Ndugu Zangu


Nileteeni Gwajima x 3
Nileteeni Daniel x3
Nileteeni Tulia, Nitatulia




Msipomchagua Huyu Hii Mtalimia Meno
Maji Hamtapata Siwatishi Nasema Wazi Wazi
 
Kuna hekima kwenye utungaji sheria mkuu.Unapowaza sheria itungwe,fikiri na the negative side,hasa matumizi mabaya ya sheria hiyo.
Hii ni Africa,sio China.
Hapo umenena, yawezekana ikawa kama mtego wa panya !! Nadhani Uzalendo wa kweli ni muhimu sana katika kudhibiti Mali na Rasilmali za Nchi,
 
Hapo umebugi huyo mama ni fukara wa kutupwa alikotokea alikuw ni house gerl standard 7 failure ,mara ya mwisho alikuwa house girl wa kikwete wakati kikwete alikuwa ajulikani katika nchi hii
 
Watawekaje Sheria Kali wakati watunga Sheria ndy wezi wenyewe?
 
Kabisa tena wamepewa Kinga hata wasiostahili Kinga. Maajabu hayataisha nchi hii
 
Sasa kama watawala wanavitia korokoroni vyama vingi, ni nani huyo unayemtarajia atunge sheria kali na kutekeleza hukumu ya kifo kwa mafisadi, wahujumu uchumi na wauza madawa ya kulevya (ambao kama ujuavyo wana connection na watawala)?
 
Maelezo uliyotoa hapa ndio katiba mpya yenyewe inayopigiwa debe na wapinzani. Usitarajie kabisa uzalendo mbele ya pesa. Hadi sasa ni Nyerere peke yake, katika hali ya kushangaza sana, ndiye kiongozi “aliyedharau sana” pesa na wanaozitafuta kifisadi.

Hata huko US na Ulaya wapo waroho wengi tu. Lakini waliamua mapema kuandika katiba makini na kutunga sheria za uhakika kudhibiti umungu, udikteta na ufisadi miongoni mwa viongozi na raia. Walipigana vita kufanikisha makubaliano sahihi ya kitaifa. Leo hii hawafanyi mchezo na mambo hayo ya msingi.
 
Uzalendo ni kuwajibika, pasi na kuwajibika katiba mpya inaweza ikawepo na watu wakaipuuza kwa baadhi ya vipengele kama ilivyo kwa Covid-19 na hamna kitu mtafanya.
 
Sawa kabisa, tatizo ni viongozi. Linatatuliwaje?

Btw hili ni tatizo la enzi na enzi. Watu weusi walisombwa kwa malaki kwenda utumwani Ulaya, Amerika na Uarabuni SI kwa nguvu ya wageni pekee, BALI kwa kuwindwa na kuuzwa na viongozi wao ambao pia waliotoa nguvu kazi ya kusaidia kuwaswaga hadi pwani kwenye merikebu.
 
Uzalendo ni kuwajibika, pasi na kuwajibika katiba mpya inaweza ikawepo na watu wakaipuuza kwa baadhi ya vipengele kama ilivyo kwa Covid-19 na hamna kitu mtafanya.
Ni kama Nyerere alivyowaambia Wachina kuwa Ujamaa ni imani wakamshangaa sana. Mwishowe “roho ya ubinafsi” ilimshinda.

Ukitegemea Watanzania wawe “wazalendo” bila mfumo makini wa udhibiti, sahau kuwa na nchi yenye maendeleo.
 
Nitajibu hilo la "viongozi"
Linaanzia kwa wananchi, kuwachagua viongozi wanaoamini wanaweza kushughulikia swala hilo kwa umakini mkubwa. Utaona hapa, tena tunarudi kwa "tatizo ni wananchi" wanaochagua viongozi wabovu

Laiti kama pangejitokeza na kiongozi mwenye msimamo thabiti, na mwenye uwezo wa kuwashawishi wananchi waelewe wajibu wao wa kuchagua viongozi imara, hapa tungekuwa tumeanza hatua muhimu.

Ngoja nikwambie jambo.
Pamoja na ubovu wote aliokuwa nao Magufuli, lakini katika swala la rushwa na mambo ya aina hiyo, watu waliweza kumwelewa (hata kama alikuwa akiwahadaa).
Basi atokee Magufuli mwingine, asiyekuwa na matabia mengine ya hovyo hovyo kama aliyokuwa nayo Magufuli, lakini akajitoa mhanga kabisa kusimamia sheria zinazobana jambo hili. Watu watamwelewa sana, na utaona hali inabadilika sana kuliko ilivyo sasa.

Hatuwezi kuacha kujishughulisha na tatizo eti kwa vile ni "tatizo la enzi na enzi". Si unaona utumwa ulikomeshwa? Kwa nini tusifanye tunayoweza kufanya kwa sasa kwa kufikiri tu kwamba ni tatizo la enzi na enzi?
 
Ni kama Nyerere alivyowaambia Wachina kuwa Ujamaa ni imani wakamshangaa sana. Mwishowe “roho ya ubinafsi” ilimshinda.

Ukitegemea Watanzania wawe “wazalendo” bila mfumo makini wa udhibiti, sahau kuwa na nchi yenye maendeleo.
Ndio lazma kuweka mfumo wa kudhibiti ambao utaondoa michongo ya kulindana
 
Sasa kama watawala wanavitia korokoroni vyama vingi, ni nani huyo unayemtarajia atunge sheria kali na kutekeleza hukumu ya kifo kwa mafisadi, wahujumu uchumi na wauza madawa ya kulevya (ambao kama ujuavyo wana connection na watawala)?
Mamlaka yote yanatoka kwa umma, umma usikubali jina LA wanyonge Na unyonge. Hakuna aliye mkubwa kuuzidi umma. Huwezi kuipata pepo bila kufa kwanza. Ni bahati mbaya tu kuwa viongozi wetu wa upinzani wengi wao ni wapenda mali, wanayo mali inayohitaji kulindwa. Yaani wanacho cha kupoteza. MTU mwenye mali nyingi ni nadra sana kufaa kuongoza upinzani.
 
Naona umeweka post za June 2015 na heading ya Magufuli, nlitaka kuuliza by June 2015 raisi alikua Magufuli au JK?
Tarehe kukosewa hapo kwenye hilo gazeti la Mtanzania haifuti ufisadi wa TZS 1.5 trilioni aliofanya Magufuli na kumfanya kuwa fisadi Papa wa muda wote.

Ufisadi huo uliofichuliwa na CAG Profesa Musa Assad uliandikwa kila mahali ikiwa ni pamoja na hapa JF.

Kukosewa kwa tarehe kwenye hicho chanzo kimoja cha habari hakuwezi kumpa hifadhi wala kumsitiri Magufuli pamoja na genge lake na ufisadi huo wa historia.
 
Hii ni kweli kabisa,leo hii wewe ukifanya hivyo wanajitokeza eti watu wa haki za binadamu kuwatetea wakati hawakuwahi kujitokeza kuwatetea wagonjwa hospital kipindi hela za dawa zinaibiwa.
 
Nchi imegeuka ya kisultani, ukiwanusa wabunge, wakuu wa mikoa Na wilaya, wakurugenzi, Na watumishi wa umma utakutana Na harufu Kali za watoto, wake, wajukuu, ndugu Na marafiki wa viongozi wa kisiasa Na serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…