Adhabu ya TFF/bodi ya ligi kwa Mbwana Makata, sio kila gari ni Ambulance.

Ndiyo ikosekane ambulance??
Basi bora tusiwe na ligi. Usipende kutetea mambo ya kijinga.

Mkuu unaelewa umuhimu wa ambyulensi lakini??
Yaani ni Bora hata kamisaa wa mchezo asiwepo ila ambyulensi iwepo.

Acheni kutetea ujinga. MbK wameonewa

Wewe unatazama jinsi inavyo takiwa kuwa mimi naongelea UHALISIA

Zaidi ya asilimia 60 ya mechi ligi kuu zinacheza bila ambulance...... kama hutaki sikulazimishi mkuu
Na sio kama hawataki bali HAWANA wanategemea za KUOMBA kwenye hospitali

Michezo yote haijalishi ligi gani au aina gani ya mchezo ambulance ni LAZIMA kisera na kikanuni za michezo........ hata ligi za wilaya au ndondo cup lazima ziwepo na SIO LIGI KUU TU
Jiulize sasa hizo ambulance unaziona huko? Na sio kama hawataki ziwepo ni HAWANA

Huko championship ndio kabisaa wakiamua kama Mbwana makata game zote zitasusiwa

Sitetei ujinga naelezea uhalisia
Kutunga kanuni bila kuweka mazingira rafiki hii ndio shida yake
Huyo Makata hata yeye sio uwanja wao wala timu wala chama cha mpira mkoa chenye ambulance, anajua wanaomba na kuna wakati wanakosa wanaweka defender ya polisi kama emergency ambulance
 

Nguvu nyingi sana inatumika kumtetea Mbwana makata bila kuangalia UHALISIA mkuu

Pamoja na makosa yote ya kikanuni HAIKUWA jukumu la kocha kugomea mechi

Katika moja ya makosa makubwa sana ni pamoja na kugoma kucheza

Kama unaona kuna kanuni zimekiukwa utalalamika baada ya mchezo na zikiwa sahihi utanufaika nazo lakini sio kugoma kucheza

Yaani refa atoe labda red card kimakosa au penalty halafu unatoa timu nje ya uwanja?
Kugomea mchezo kwa mazingira hayo haikubaliki
 
Mimi naona TFF wapo SAHIHI.
ambulance ilikwenda uwanjani ikapata dharura ikatoka ikarudi kabla ya muda wa kisheria wa kughairishwa mechi kufika.
Lakini huyo kocha akakomaa nadhani alikuwa anatafuta Sababu.
Na anayaruhusiwa kughairisha mchezo ni msimamizi wa mchezo SIO KOCHA
Alichokipata ni HAKI YAKE
 
Muda wa kanuni wa kughairisha mchezo ni dakika 30 je zilifika hizo dakika 30?
Kanuni haisemi Prado, inataka ambulance ambayo ndani yake Kuna vifaa tiba, tiba na watoa tiba, je ndani ya Prado hilo kulikuwa na vitu hivyo? Mbona Simba na Yanga ziiligomea mechi na Simba na Yanga lakini hakuna aliyefungiwa hata mmoja?
 
Kama ni hivyo basi, kwakuwa ambulance unasema hazipo kanuni ya ligi isitaje ambulance, badala yake iseme kuwepo na gari standby ya kusafirisha watu. Lakini ukishasema kuwe na ambulance basi lazima kuwe na ambulance na sio Prado. Shida hapa ni TFF sio Makata.
 
Muda wa kanuni wa kughairisha mchezo ni dakika 30 je zilifika hizo dakika 30?
Hiyo ya dakika 30 ni kanuni nyingine, kanuni ya ambulance uwanjani ni dk 15. Je, ambulance ilikuwepo ndani ya dk 15 baada ya muda wa mchezo kufika? Kama haikuwepo kwanini kanuni haikutekelezwa on time? Je, ofisa alikuwa na uhakika gani kama ambulance ingerudi kabla ya dk 30? kama alikuwa na uhakika huo je, hiyo Prado ililetwa kwasababu zipi? Je, Prado ni Ambulance?
 
Hizi adhabu za kukomoana hazi mjingi mtu bali ni kumdhoofisha
 

Sio jukumu la Makata kuamua game ichezwe au la...... ni jukumu la kamisaa

Makata angeingiza timu icheze kisha akaja kulakamika baadae....... hii ndio fair play kwa watazamaji waliolipa viingilio, tv right nk nk

Ndio maana adhabu za kukiuka kanuni zipo na sio KUGOMA kucheza
 
Hapana NI UONGO.
Weka kanuni hyo inayosema baada ya dakika 15 Kama ambulance haijafika mchezo ughairishwe.
Alafu nitajie timu inayomiliki ambulance hapa Tanzania
 
mchezo wa Simba na yanga shida ilikuwa Nini?
shida ilikuwa TFF kuahirisha mechi bila kufuata kanuni za kuahirisha mechi, na kusababisha simba na yanga zote kwa nyakati tofauti kugomea mechi. Hii inafanana kabisa naTFF na wadau wake Namungo kushindwa kupeleka ambulance mapema uwanjani kama kanuni inavyotaka na kusababisha Mbeya kwanza kugomea mechi. Mkuu huoni kuwa kuna kufanana hapo? na kwanini baada ya dk 15 za kupeleka ambulance kupita mechi haikuahilishwa kama inavyotakiwa huku wakijua kwamba hakuna uhakika wa ambulance kurudi? je, kamba ambulance ingepata kazi nyingine huko ilikokwenda ingekuwaje? na je, kama katikati ya mechi ambulance ingepata dharura nyingine na kuondoka je, mechi ingesimama kuisubiri irudi? Au walikuwa na nia gani kwa wachezaji na watazamaji ambayo walikusanyika pale pale kama angetokea mmojawao kuihitaji ambulance kuokoa uhai wake?
 

Two wrong can’t make it right.

Yaani timu zianze kugoma tu sasa kwasababu Yanga/Simba hazikuadhibiwa?
 
Halafu mkiambiwa ligi yetu n dhaifu mnakaza mishipa ya shingo kilichotokea kwa Makata ndo udhaifu wenyewe kuna mda Hawa TFF na bodi ya ligi wanajionaga Kama wao n serekali bila kujali chochote Namungo na chama cha mpira Lindi kaz yao ilikuwa n kuhakikisha kuna ambulance uwanjani mwanzo had mwisho wa mchezo
 
sasa Kama Hakuna anayeweka ambulance wanaweka kanuni na sheria za nn kwahiyo hiz kanun zinatumika kwa baadhi ya timu na kwahao viongoz kukosekana kwa ambulance wao wamejiwajibisha ????au kanun haziwahusu
 
kucheza under protest ni kanuni ya ligi namba ngapi? kanuni zinatungwa na kusambazwa ili ziheshimiwe badala ya kusubiri huruma au maoni ya mtu fulani.
 
Gari ilikuja kabla ya dakika 30 wakakataa kuingiza timu uwanjani ili wapate mbeleko ya point za bure. Na hiyo adhabu waliopewa ni ndogo ilibidi wafungiwe maisha kabisa.
Ilikuwa wapi ikifanya nini? Nani alikuwa na uhakika kwamba ambulance haitahitajika tena huko ilikochelewa na kuondoka wakati mechi ikiendelea na kuacha wachezaji bila ambulance? Ambulance ilikuwa na kazi nyingi
 
Ni jukumu la kanuni sio mtu fulani kufanya kama anavyoona au kutaka. Weledi uko wapi kama mtu anafananisha Prado na Ambulance? Ambulance inaweza kuwa Prado lakini Prado haliwezi kuwa ambulance.
 
shida ni yule msomali wa karume pale kila kitu yy anatumia nguvu,mbona simba na yanga makocha hawakufungiwa?
Hilo nalo neno. Timu ndgo zinaumia sana kwa maamuzi ya kipuuzi ya viongozi wasiojali
 
sasa Kama Hakuna anayeweka ambulance wanaweka kanuni na sheria za nn kwahiyo hiz kanun zinatumika kwa baadhi ya timu na kwahao viongoz kukosekana kwa ambulance wao wamejiwajibisha ????au kanun haziwahusu

Mkuu hizo kanuni ni “international standards “ na zinatakiwa kuwepo kwenye michezo YOTE rasmi......... namaanisha michezo na ligi zote Afya imepewa kipaumbele

Lakini sasa je miundombinu na raslimali uchumi zetu zina ruhusu mkuu?
Hapo Lindi utakuta Ambulance ni moja tu ya hospitali ya mkoa
Ambulance hiyo mama waja wazito wagonjwa mbali mbali nk halafu huku mpira dk 90
Ndio maana inatumika tu busara, Ambulance ilikuja japo kwa kuchelewa lakini Mbwana akatumia hapo kugoma

Tatizo kubwa lina kuwa sio kazi ya Mbwana kuamua hatma ya mchezo ni KAMISAA

Hata Fifa wanakosea na wanawajibishana baada ya timu kupeleka malalamiko lakini sio kugomea

Mkuu huko daraja la tatu sijui hawajui hata kama kuna hiyo kanuni
Mpira wetu bado sana kukidhi na kufuata vigezo vyote 100% kwasababu za kimipangilio na uchumi
 
Hilo nalo neno. Timu ndgo zinaumia sana kwa maamuzi ya kipuuzi ya viongozi wasiojali
Timu iliyoshinda kwa kupewa points za mezani itamfunga nani kwenye mashindano ya caf? Kuna timu inaogopwa na timu zote kwenye ligi kwa chupli. Timu zinaona heri zipewe adhabu kuliko kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo siku ya mechi na timu hiyo kwa Mkapa. TFF inachekelea tu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…