Adhabu ya TFF/bodi ya ligi kwa Mbwana Makata, sio kila gari ni Ambulance.

Adhabu ya TFF/bodi ya ligi kwa Mbwana Makata, sio kila gari ni Ambulance.

Ambulance kuwepo uwanjani ni muhimu sana, hao waliogomea mchezo kwa kutokuwepo Ambulance wapo sahihi kabisa
 
Wangecheza, halafu baada ya mechi wakate rufaa, kosa haliwezi kuhalalishwa kwa kosa.
Haiko hivyo, Kuna wachezaji na watatamaji wanaofia uwanjani kwa sababu mbalimbali kabla, wakati na hata baada ya mechi. Kanuni ya kuwepo kwa ambulance (sio Prado) full time imezingatia ukweli huo. Kucheza bila ambulance ni kuhatarisha kwa kuweka rehani maisha ya wachezaji na watazamaji wa mechi. Kumbuka kuwa wakati wa mechi kunaweza kutokea ajali kwa wachezaji kugongana au kupigana ikitokea vurugu. Hata mashabiki pia wanaweza kupigana uwanjani au hata kupingwa na polisi kama ikitokea vurumai, hivyo uwepo wa ambulance masaa yote ni lazima (risks register and management)
 
Makata kudai ambulance kuwepo uwanjani ni suala la kikanuni na Ambulance haikuwepo uwanjani bila kujali kuwa ilikwenda wapi kufanya nini. Ambulance ni gari maalumu lenye miundombinu inayoweza kuokoa maisha ya mgonjwa mwenye afya mbaya wakati anakimbizwa kuwahi matibabu kamili ya hospitali.

Sio kila Prado inaweza ku-replace uwepo na umuhimu wa ambulance.

Kama kanuni inataja Ambulance na Ambulance haikuwepo basi kumfungia kocha kwa miaka 5 na kumpa pointi 3 mpinzani ambae hakuleta Ambulance uwanjani sio sawa.

Kama kanuni inasema Ambulance isipokuwepo uwanjani baada ya 15 minutes kupita ofisa anaahirisha mechi lakini yeye hakufanya hivyo, mechi hii sio sawa. Tayari kosa la kukosekana kwa ambulance limetendeka lakini, badala yake ofisa akapiga ramli kuwa Ambulance itarudi ilikokwenda, hivyo mechi iendelee kuchezwa nayo sio sawa, maana mchezaji angeweza kuumia uwanjani hata dakika ya 2 TU baada ya mchezo kuanza wakati Ambulance haijarudi ilikokwenda.

Kumuadhibu Makata kwa kutumia kanuni ya dk 30 badala ya ile ya dk 15 ni sawa na polisi kusubiri mhalifu atende kosa la pili ili amkamate.

Haki ingekuwa kuwaambia Namungo walete Ambulance on time bila kisingizio chochote maana tarehe na muda wa mechi ulifahamika mapema na uhaba na matumizi ya ambulance Yao wanaufahamu wao sio Mbwana na mbeya Kwanza.

Mwaka mmoja ungetosha badala ya miaka 5.
wamemuonea,lakini nadhani wana shida nae nyingine
 
wamemuonea,lakini nadhani wana shida nae nyingine
Nimemsikia Leo kaomba msamaha TFF asamehewe. Ni vizuri lakiñi angekuwa mm nisogea siti za mbele ijulikane kama nimekosea au naonewa. Huko siti za mbele bodi ya ligi ingekwenda kunithibitishia kama ni kweli ambulance Ile ingekuwepo ingekuwepo full time wakati wa mchezo ule, bila shaka wangeonyesha barua (mou) kutoka hospital inayowapa ruhusa ya kukaa na ambulance Ile kwa dakika zote 90 za mchezo ule bila kuhitajika kwa kazi nyingine kwa muda wote w mchezo.
 
Back
Top Bottom