mjingamimi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 42,209
- 51,004
Sasa si unaona wenye mamlaka ndo walichanganya mambo?
Sasa kesi ya Simba na yanga inahusiana vipi na namungo na mbeya kwanza? Hauoni Kama ni kesi tofauti
Sasa kesi ya Simba na yanga inahusiana vipi na namungo na mbeya kwanza? Hauoni Kama ni kesi tofauti
shida ilikuwa TFF kuahirisha mechi bila kufuata kanuni za kuahirisha mechi, na kusababisha simba na yanga zote kwa nyakati tofauti kugomea mechi. Hii inafanana kabisa naTFF na wadau wake Namungo kushindwa kupeleka ambulance mapema uwanjani kama kanuni inavyotaka na kusababisha Mbeya kwanza kugomea mechi. Mkuu huoni kuwa kuna kufanana hapo? na kwanini baada ya dk 15 za kupeleka ambulance kupita mechi haikuahilishwa kama inavyotakiwa huku wakijua kwamba hakuna uhakika wa ambulance kurudi? je, kamba ambulance ingepata kazi nyingine huko ilikokwenda ingekuwaje? na je, kama katikati ya mechi ambulance ingepata dharura nyingine na kuondoka je, mechi ingesimama kuisubiri irudi? Au walikuwa na nia gani kwa wachezaji na watazamaji ambayo walikusanyika pale pale kama angetokea mmojawao kuihitaji ambulance kuokoa uhai wake?