Adhabu ya TFF/bodi ya ligi kwa Mbwana Makata, sio kila gari ni Ambulance.

Adhabu ya TFF/bodi ya ligi kwa Mbwana Makata, sio kila gari ni Ambulance.

Mpira wetu una safari ndefu kweli kweli kabla ya kufikia mafanikio, Mbeya kwanza wakate rufaa na ikibidi waende mahakamani
 
Makata kudai ambulance kuwepo uwanjani ni swala la kikanuni na ambulance haikuwepo uwanjani bila kujali kuwa ilikwenda wapi kufanya nini. Ambulance ni gari maalumu lenye miundombinu inayoweza kuokoa maisha ya mgonjwa mwenye afya mbaya wakati anakimbizwa kuwahi matibabu kamili ya hospital.

Sio kila prado inaweza ku replace uwepo na umuhimu wa ambulance.

Kama kanuni inataja ambulance na ambulance haikuwepo basi kumfungia Kocha kwa miaka 5 na kumpa point 3 mhalifu ambae hakuleta ambulance uwanjani sio sawa.

Kama kanuni inasema ambulance isipokuwepo uwanjani baada ya 15 minutes kupita ofisa anaahilisha mechi lakini yeye hakuahilisha mechi hii sio sawa. Tayari kosa la kukosekana kwa ambulance kwa dk 15 limetendeka lakini mechi haikuahilishwa, badala yake ofisa akapiga ramli kuwa ambulance itarudi ilikokwenda hivyo mechi iendelee kuchezwa nayo sio sawa, maana mchezaji angeweza kuuamia uwanjani hata dk 2 TU baada ya mchezo kuanza wakati ambulance haijarudi ilikokwenda.

Kumuadhibu Makata kwa kutumia kanuni ya dk 30 badala ya Ile ya dk 15 ni sawa na polisi kusubiri mhalifu atende kosa la pili ili amkamate.

Haki ingekuwa kuwaambia namungo walete ambulance on time bila kisingizio chochote maana tarehe na muda wa mechi ulifahamika mapema na uhaba na matumizi ya ambulance Yao wanaufahamu wao sio Mbwana na mbeya Kwanza.

Mwaka mmoja ungetosha badala ya miaka 5
Adhabu kweli ni kali nasema ni ADHABU KALI lakini kitendo cha kocha wa timu ya ligi kuu na viongozi wa timu husika kutokujua kanuni zinazoongoza ligi husika ni UJUHA KULIKO UJUHA WA MFALME JUHA mwenyewe. Wao waligoma kuingiza timu wakidhani kanuni ni dkk15 kumbe uhalisia ni dkk30 ujuha wa mfalme juha ukaanzia hapo gari(ambulance) limefika ndani ya muda wa kikanuni saa 16:23 wao wakakaza mafuvu kuwa ni nje ya muda hawaingizi timu. Masikini mbeya kwanza timu ya nyumbani ujuha+ kupenda kitonga kumeiponza timu hakuna namna ya kukwepa adhabu tujiandae kupishana na Ihefu another home boys
 
Tatizo linaanzia pale raisi anapokuwa anatoka Somalia hana uzalendo sasa unamfungia mtu miaka yote ataishije.
 
Kanuni haisemi Prado, inataka ambulance ambayo ndani yake Kuna vifaa tiba, tiba na watoa tiba, je ndani ya Prado hilo kulikuwa na vitu hivyo? Mbona Simba na Yanga ziiligomea mechi na Simba na Yanga lakini hakuna aliyefungiwa hata mmoja?
Bila shaka hukukusudia kuni qoute mimi.
 
kucheza under protest ni kanuni ya ligi namba ngapi? kanuni zinatungwa na kusambazwa ili ziheshimiwe badala ya kusubiri huruma au maoni ya mtu fulani.
Hiyo kanuni iko wapi inayosema timu ikatae kucheza kama ambulance imechelewa kuwepo uwanjani dakika 15? Kutoa adhabu kwa timu mwenyeji ni jukumu la TFF, sio la timu kugomea mchezo
 
Hiyo kanuni iko wapi inayosema timu ikatae kucheza kama ambulance imechelewa kuwepo uwanjani dakika 15? Kutoa adhabu kwa timu mwenyeji ni jukumu la TFF, sio la timu kugomea mchezo
Hata chuoni Kuna kanuni ya muda wa mwanafunzi kumsuburi mwalimu kwenye kipindi chake, ukipita wanafunzi wanatimka. Au wewe hukusoma? Unapotunga kanuni inayo taja muda maada yake baada ya muda huo kupita Kuna consequences zake. La sivyo usitunge kanuni ambayo unataka isitumike na kusumlbiri busara ya ya mtu kuamua consequences.
 
Usije ukathubutu kuondoka mwenyewe kwenye chumba cha mtihani eti kisa msimamizi amechelewa kwa zaidi ya dakika 30, utapigwa discontinuation ya kujitakia. Anayethibitisha kwamba mtihani haujaletwa katika chumba cha mtihani ni Examination Officer na baadhi ya reputable universities ni Quality Assurance Officer, na sio mwanafunzi
 
Kanuni haisemi Prado, inataka ambulance ambayo ndani yake Kuna vifaa tiba, tiba na watoa tiba, je ndani ya Prado hilo kulikuwa na vitu hivyo? Mbona Simba na Yanga ziiligomea mechi na Simba na Yanga lakini hakuna aliyefungiwa hata mmoja?
Mbwana ameadhibiwa kwa kushawishi wachezaji kugomea mechi na waliondoka kabla ya dakika 30
 
Hata chuoni Kuna kanuni ya muda wa mwanafunzi kumsuburi mwalimu kwenye kipindi chake, ukipita wanafunzi wanatimka. Au wewe hukusoma? Unapotunga kanuni inayo taja muda maada yake baada ya muda huo kupita Kuna consequences zake. La sivyo usitunge kanuni ambayo unataka isitumike na kusumlbiri busara ya ya mtu kuamua consequences.
Vipi mwalimu akija baada ya muda kupita akafundisha
 
Mkuu kosa lingine la TFF ni hilo

Hakutakiwa kupewa adhabu Makata kama Makata
Ilitakiwa kupewa adhabu Mbeya kwanza kama timu
Tunapo taja Makata tunamaanisha mbeya kwanza timu

Linapokuja swala la maamuzi ndani ya uwanja ni kocha ndio anabeba maamuzi ya klabu

Mbeya kwanza ilitakiwa kupokwa alama na kupigwa faini ndefu sana kama timu na sio kudeal na kocha kama kocha
Kocha alishawishi wachezaji kugomea mechi,wao walikuwa tayari kucheza
Anadhani ligi ya mchangani hii
 
Kama yote ni sawa kwanini Prado isingepeleka mgonjwa na ambulance ikabaki, tuache ndoto za mchana.
 
Usije ukathubutu kuondoka mwenyewe kwenye chumba cha mtihani eti kisa msimamizi amechelewa kwa zaidi ya dakika 30, utapigwa discontinuation ya kujitakia. Anayethibitisha kwamba mtihani haujaletwa katika chumba cha mtihani ni Examination Officer na baadhi ya reputable universities ni Quality Assurance Officer, na sio mwanafunzi
Kama kanuni ni kuondoka baada ya dk 30 uki appeal mahakamani mwanafunzi atashida kesi. Pale UDSM mwanafunzi alifeli na kupingwa disco lakini akakata rufaa kuwa amefeli kwakuwa umeme ulikuwa ukikatika chuo kila mara hivyo alishindwa kusoma vizuri kule library. Swali la hakini kwa chuo lilikuwa moja TU kuwa ni kweli umeme huwa unakatika chuoni? Wakajibu ndiyo Kuna siku unakatika, mwanafunzi akashida kesi.

Swali kwa TFF ni moja TU, ni kweli ambulance haikuwepo uwanjani dk 15 baada ya muda wa kuanza mchezo kupita? Wakijibu ndivyo haikuwepo, Makata kashinda kesi.
 
Swali kwa TFF ni moja TU, ni kweli ambulance haikuwepo uwanjani dk 15 baada ya muda wa kuanza mchezo kupita? Wakijibu ndivyo haikuwepo, Makata kashinda kesi.
Kwani amefungua kesi? Ataishia kuomba msamaha kama Mwakalebela
 
Kwani amefungua kesi? Ataishia kuomba msamaha kama Mwakalebela
Kama hajafungua kesi atakuwa mujinga. Hata akina Mdee wako bado mjengoni pamoja na kufukuzwa na chadema kwakuwa wameenda mahakamani kipinga.
 
Kama hajafungua kesi atakuwa mujinga. Hata akina Mdee wako bado mjengoni pamoja na kufukuzwa na chadema kwakuwa wameenda mahakamani kipinga.
akina Mdee siasa huku Makata mpira. Haiwezekani uhamasishe timu isiingie kucheza halafu uchekewe, eti kisa hakuna ambulance. Si angewasubiri walioweka kanuni waje kuiadhibu timu mwenyeji?
 
akina Mdee siasa huku Makata mpira. Haiwezekani uhamasishe timu isiingie kucheza halafu uchekewe, eti kisa hakuna ambulance. Si angewasubiri walioweka kanuni waje kuiadhibu timu mwenyeji?
Basi kusingekuwa na kanuni ambazo kila timu ilisaini kuzitii na kuzifiata, tungesubiri busara ya kamisaa.
 
Back
Top Bottom