Adhabu ya TFF/bodi ya ligi kwa Mbwana Makata, sio kila gari ni Ambulance.

Sasa si unaona wenye mamlaka ndo walichanganya mambo?
Sasa kesi ya Simba na yanga inahusiana vipi na namungo na mbeya kwanza? Hauoni Kama ni kesi tofauti
 
Sikuona sababu ya Namungo kupewa points 3 kama alie sababisha mchezo usichezwe kapewa adhabu mechi ingepangwa siku nyingine
 
Ni jukumu la kanuni sio mtu fulani kufanya kama anavyoona au kutaka. Weledi uko wapi kama mtu anafananisha Prado na Ambulance? Ambulance inaweza kuwa Prado lakini Prado haliwezi kuwa ambulance.

Narudia tena kwa sauti kubwa
Anaye amua hatma ya mchezo ni KAMISAA

Kama kakosea Kamisaa haikua jukumu la Makata


Hebu aasume Pirates wangekataa kuingiza timu uwanjani kwasababu kanuni zimekiukwa?
Walichofanya Pirates ndicho walipaswa kufanya Mbeya Kwanza

Kukiukwa kwa kanuni kwa namna yoyote ile hakumpi UHALALI Makata kuto kuingiza timu uwanjani iwapo officials wameridhia

Kila mtu asimame kwenye nafasi ya na atahukumiwa kwa nafasi yake
 
Sikuona sababu ya Namungo kupewa points 3 kama alie sababisha mchezo usichezwe kapewa adhabu mechi ingepangwa siku nyingine

Mkuu kosa lingine la TFF ni hilo

Hakutakiwa kupewa adhabu Makata kama Makata
Ilitakiwa kupewa adhabu Mbeya kwanza kama timu
Tunapo taja Makata tunamaanisha mbeya kwanza timu

Linapokuja swala la maamuzi ndani ya uwanja ni kocha ndio anabeba maamuzi ya klabu

Mbeya kwanza ilitakiwa kupokwa alama na kupigwa faini ndefu sana kama timu na sio kudeal na kocha kama kocha
 
mkuuu unazunguka Sana juz hapa yanga waligomea mechi wazi wazi kabisa Hakuna adhabu aliyopewa kiongoz wowote tena badala yake viongoz wa yanga kuwa Kama mnataka mechi irudiwe mfungulieni mwakalebela mwakalebela akafunguliwa, Kama utafata kanuni za club licence kila klabu inatakiwa iwe na kiwanja na timu za vijana Kama hilo la ambulance wameshindwa je wataweza kusimamia kila club iwe na uwanja na timu za vijana tuna viongozi au Takataka
 
Nini kitafanyika iwapo;

Ambulance ikiletwa uwanjani kwa wakati ili kutimiza matakwa ya kikanuni halafu ikatoweka huku mechi inaendelea.

BTW:Adhabu za TFF hutolewa kwa mihemko tu.

Je,kuna yeyote aliwajibishwa kuahirishwa kwa derby ya Simba na Yanga?
 
Hao washashushwa daraja rasmi...
 
namungo ni timu ya waziri mkuu.
nilishabashiri kitakachompata Makata. pole kwake, familia yake hasa watoto na wife. miaka mitano ya Baba kukosa kazi rasmi sio jambo dogo. ni mateso.

waliomuadhibu makata wamefanya hivyo ili kutengeneza mazingira ya kujipendekeza na kuimarisha uchawa wao kwa waziri mkuu.
 
Dakika 30 za Kanuni ya pili hazikufika. Ambulance ilishafika, Wangeingiza timu kisha wapeleke Rufaa yao na sio kuongoza mgomo.

Kufungiwa ni sawa tu tena wakirudia sikunyingine wafungiwe maisha.

Timu ipo mkiani waliona hawana uwezo wa kupata ushindi uwanjani na kutafuta mbinu mbadala.
 
Sasa si unaona wenye mamlaka ndo walichanganya mambo?
Sasa kesi ya Simba na yanga inahusiana vipi na namungo na mbeya kwanza? Hauoni Kama ni kesi tofauti
Hapa napo mamlaka ndiyo iliyochanganya mambo kwakuwa siku ile hakukuwa na ambulance kwaajili ya mchezo ule, kulikuwa na Prado na ambulance ambayo ilikuwa off and on pale uwanjani, yaani wakati wowote ingehitajika kwa kazi nyingine nje ya uwanja kuokoa maisha ya watu nje ya uwanja. Ajali nayo haina kinga inaweza kutokea wakati wowote bila kujali ambaulance ipo au haipo.
 
Ukishindwa kuleta ambulance, basi mchezo usichezwe.
Siyo lazima muwe na timu ya Moira, kama hamuwezi acheni.
 
Hiyo sio kweli kabisa, kwani kwenye mechi ya simba na yanga iliyoahirishwa hakukuwa na kamisaa? mbona timu ziliingia mitini zenyewe? Kama kamisaa ndio kila kitu kusingekuwa na kanuni za ligi ambazo timu zinasaini kuzikubali na kuzitii. Kanuni ndio muongozo wa ligi wacha uongo wako, kamisaa ni nani hadi atunge kanuni zake. kwanini kamisaa alikubali Prado badala ya ambulance, kwanini baada ya dk 15 kumalizika bila ambulance hakufanya kama kanuni inavyoelekeza afanye. Nani alimwambia kuwa ambulance itarudi ndani ya dk 30, nani kamwambia kuwa ambulance haitaondoka tena wakati mchezo unaendelea.
 
Ukishindwa kuleta ambulance, basi mchezo usichezwe.
Siyo lazima muwe na timu ya Moira, kama hamuwezi acheni.

Anaye amua hatma ya mchezo ni KAMISAA na sio Makata mkuu

Kosa la Makata ni kuchukua maamuzi yasio muhusu kisheria

Hivi Mtibwa wakikiuka kanuni na kuingilia mlango sio timu pinzani itagoma kwasababu kanuni zimekiukwa

Wajibu wa timu ni kufuata maelekezo ya officials na kama wanahisi sivyo ndivyo wajibu wao ni kupeleke malalamiko yao baada ya mchezo na sio KUGOMA

Siwatetei TFF kama gari haikuwepo kweli ni makosa
Lakini Makata kugoma ni KOSA pia
 
Mifumo yote ndani ya taifa moja lazima isomane, kabla ya kutunga kanuni ya ligi lazima ufanye situational analysis na physibility study kujua kama kanuni fulani inatekelezeka au la. Kama unafahamu kuwa ambulance hazipo na timu hazina viwanja kwani utunge kanuni ambayo haitekelezeki? Kamisaa na akili zake anaona Prado = ambulance, kweli jamani?
 
kifupi pale hapakuwa na ambulance, iliyokuwepo ilikuwa ya wenyewe na wenyewe walikuwa na kazi nayo. Hakuna mganga mkuu wa hospitali mwenye akili zake timamu atakubali hospitali yake ikose ambulance hata kwa dk tano. Hata hiyo Prado sijui ilikuwa ya nani.
 
dawa ya tatizo hilo ni kuifuta kanuni kama haitekelezeki, lakini sio kuachia mtu atafasiri yeye kwa kutumia hekima, akili na moyo wake nje ya kanuni.
 

Unachanganya mambo mawili mkuu

Mosi, Kuna kanuni kukiukwa na pili kuna kugomea mechi

Hizo habari za prado sijui benzi ni habari za kamisaa na sio Makata........ kuna kanuni zaidi ya 100 na anaye sema kanuni zipo ok ni Kamisaa sio Kocha.
Kama officials walijiridhisha(hata kama ni kimakosa) haikua wajibu wa Makata kususa, wajibu wake ilikua kuingiza timu na kuja kufungua malalamiko....... Sijui kwako ni kipi kigumu kuelewa hapa

Officials sio malaika wanakosea pia, utahangaika sana kutafuta uhalali wa prado lakini hio sio KIGEZO cha Makata KUGOMA

Mifano yako ya Simba na yanga nimesema Two wrong can’t make it right
 
dawa ya tatizo hilo ni kuifuta kanuni kama haitekelezeki, lakini sio kuachia mtu atafasiri yeye kwa kutumia hekima, akili na moyo wake nje ya kanuni.

Hapa tupo pamoja
Tulalamikie ubutu wa kanuni na sio kumtetea Makata eti alikua na HAKI ya kugoma
 

Hakuna timu yenye ambulance
Hakuna tff mkoa au wilaya wenye ambulance
Hata Mbeya Kwanza hawana Ambulance
Ni busara tu za officials ndio zinafanya game zichezwe mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…