Advance Physics ilivyokuwa inatugeuka ndani ya chumba cha mtihani

Hili somo lilifanya nimtajirishe mgote maana kila pamphlet lake nilikua nalo ila bado kwa necta nikaunguza, nina uhakika prac ndio ilinibeba
Naona buroka alikuingiza chaka
Hahahahahahaaaaa.

Notes za Mgote zimenitoa kimaso maso na maswali yake mengi yaliyosolviwa kutoka vitabu mbalimbali.
 
Mkuu umenikumbusha mbali sana, Enzi za Azaboy Taifa Kubwa. Aisee pale Mchikichini sidhani kama kuna banda sikuwahi kusomea lakini matokeo yake Physics ilichonitenda siyo Njema. Nilikuwa najua mpaka washikaji walinichangia buku buku ikafika Twenty ili nikapige forging ya Practical kwa Mtiga, kumbuka wandewa wakikupa hela yao lazima uwe makini sana kwa sababu hiyo buku kiadvance ni kubwa sana. Ila kilichonitokea ni historia ambayo haiwezi kufutika akilini mwangu
 
Ulilambwa KARAI nini mkuu?
 
All in all wakuu, kuna Kitu kinaitwa Medicine, Duuuhhh ni hatari au akili chuo huwa zinapungua... Shikamoo Anatomy, Pharmacology na Pathology haya masomo sikuwahi kupata B, zilikuwa ni C tu zingine za After supplementary
Hayo masomo yana watabe wake.

Halaiki ni kutafuta C na kusonga mbele
 
Mstaarabu sana yule na ndio Head of Department.Ana sauti fulani hivi nzuriiiiiiiiiiiiii......

Yaah mpole sana baba yao alikua katekista tabora..alifaulu ifunda ila mambo ya utoto akazalishwa hvyo akakatisha masomo kulea mtoto so akaanza private school ...mdogo wake tulisoma nae primary some body Deogratius ...kile kichwa achana nacho
 
kama kuna vitopic nulikuwa najipigia basi ni projectile hata swali likunjwe vipi..., Tena ya kwenye vitabu ndio nilimeza hadi majibu, yaani nikiona tu swali nakumbuka na jibu bila hata kusolve, ....shughuli ilikuwa kwenye Electromagnetism aaaaah hapo nilivyoosha mikono
 
Projectile likikukuta swali la kuderive utaeleza, bora ya kutafuta height na range.
 
Pure Math aisee.

Math sio kitu kwa mnyama physics,sema math inachukuliwa janga kwa kuwa inasomwa na watu wengi na failures wanakuwa wengi ukilingasha na wachache walio opt PHYSICS.
 
Pure Math aisee.

Math sio kitu kwa mnyama physics,sema math inachukuliwa janga kwa kuwa inasomwa na watu wengi na failures wanakuwa wengi ukilingasha na wachache walio opt PHYSICS.
 
Deadbody umenichekesha sana na uandishi wako hasa ukizingatia nilikuwa nakumbuka matukio ya advance. Kwa kweli ile level ya elimu kwa masomo ya sayansi ni ngumu kupita hata masomo ya digrii ya kwanza (sijui kuhusu ya pili).
Old moshi hiyo,tulikuwa tunafundishwa na mwalimu (aka Pdiddy) ana sauti ndogo halafu ana aibu sana hivyo anaishia kusema na ubao tu. Mifano yake ubaoni mnaelewa vizuri tu sema sasa akiacha maswali unaona kama haukuwamo darasani vile.
Prep ya physics nikifanikiwa swali moja tu kutoka kwenye UP,siku imeisha maana nakuwa nimetumia si chini ya masaa 3-4 kupata ufumbuzi ukijumlisha na baridi la moshi ndio hamu ya kulalal inakuja haraka.
Nakumbuka tulikuwa na mshikaji wangu tukakubaliana kuuza godoro moja (tuwe tunatumia moja kwa zamu) ili kupunguza muda wa kulala ili fiziksi isitushinde lakini mwisho wa hakuna cha maana tulichopata.
Nadhani sitamshauri mwana familia wangu yeyote kusoma advance, ni kupoteza muda tu.
 

Advanced physics ni zaidi ya Bsc. kwa mwaka wa kwanza kozi zote za Engineering .Yale Ma-Newton's rings unaweza kwenda bank kuombea mkopo kama dhamana
 
Ungeweka na mwaka ulosoma a level ingekua poa sana,
 
Mimi nilisoma PCM. Rafiki wa dingi alikuwa mwalimu wa physics akaniambia ukitaka utoboe advance physics kuwa serious na practical ..niliufuata ushauri wake na nikatoboa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…