Advance Physics ilivyokuwa inatugeuka ndani ya chumba cha mtihani

Hahaaa advance kazi yangu ilikua ni kukariri page za vitabu na maswali+majibu yake kwenye page husika...
Kwahio mtu akiniletea swali namtajia page alipolitoa halafu namtajia jibu kwa mbwembwe mwisho na swali linanishinda..
 
T.O alikuwa mduwanzi sana, ukisoma kwa moudy physics utacheka kipindi anampiga madongo t.o
 
Nampata huyo, bila shaka ni T.O from Tosa boys
 
Watu tunatofautiana kweli kweli.. Mie chemistry ndio ilinipa tabu..
Physics hasa form 5 ilikuwa kitonga kwangu kwa kiasi kikubwa namkumbuka madam aliyekuwa ananipigia pindi, nilianza nae na mkosi ila tukaishia kuwa marafiki wakubwa..

Kipindi cha likizo ya kumaliza form 4 watu walijichimbia mchikichini na tuition center kupiga mapindi.. Mie nilikuwa najilia zangu bata.. Sasa siku ya kwanza nareport school nakuta madam wa phyics anapiga pindi la measurements, nikaenda zangu kukaa kiti cha nyuma kabisa, kutupa jicho ubaoni naona mapicha picha tu, kidogo sijakaa vizur madam ananiita na kuniuliza swali, halaf njemba sijui kitu nikaona leo maseke, nikamwambia tu sijui kitu, wacha anichane we hujui kitu bado umechelewa kuripoti shule, na bado unakaa nyuma, kuanzia leo ukae mbele, darasa lote halina mbavu.
Kutokana mie katuni nikamwambia ticha usipate tabu nipe siku 3 tu ntakuwa safi ila mbele sikai sababu macho yangu hayaoni karibu maana hata yeye mwenyewe simuoni vizur kwa jinsi tulivyokaribu kicheko kikaongezeka.. Baadae alikuja kuwa swahiba wangu mzuri tu, kama ningekaza ningeruka pale..

Physics yoote ya 4m 5 naikumbuka mpaka leo hii
Nakumbuka nilikuwa mie na mwanangu jonii kutumia measurement tukajidai kitengeneza formula ya kwichi kwichi(kokojoa), tukasaka vitu muhimu katika kwichi kwichi kama vile friction force, heat, velocity n.k halafu hisia tukaweka costant(K)[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji85] [emoji85] [emoji85]
 
Mgote alikuwa mass nondo, nilikuwa namuita mkompliketi maisha na mipamplets yake.. Ukiona dubwasha la projectile zigo hilo, kwa moudy ni kimtindo tu ila idea yake iko kwa kichwa mpaka kesho.
 
Mkuu umenikumbusha mbali sana, sisi kihombo alikuja kutupigia tuition shule,akakuta watu wanakomaa na vitini vya kina muddy,mgote nk acha aanze kutupondea, mara ooh madogo nyie mnaandaa buyu...akaanza kutuimiza kusolve atleast vitabu 8 vya physics sijui Roger muncaster,UP,nelkon edition zote,chand nk ***** watu tukaanza kuona maisha magumu ukishika tu roger maswali hayatembei...kudadadeki si akatunga test nilitembea na 5/100,jamaa kiukweli alitukimbiza ile mbaya...
Nb mwaka wetu aliyeongoza physics alikua na C ndo ujue hili dude si la mchezo
 
Hiyo Projectile motion ilinipa marks zote kwenye pure maths... alaf watu wa egm walikuwa wanaiogopa vibaya mi nikasema nakomaa nayo... kama mtoa mada nikawa nacalculate height, range, angle na kuderive formula tu na swali likaja humo humo!!

Ila wanafunzi wa Advanced Physics kuwen wakweli, ambacho huwa kinawafelisha hasa ni kipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…