Watu tunatofautiana kweli kweli.. Mie chemistry ndio ilinipa tabu..
Physics hasa form 5 ilikuwa kitonga kwangu kwa kiasi kikubwa namkumbuka madam aliyekuwa ananipigia pindi, nilianza nae na mkosi ila tukaishia kuwa marafiki wakubwa..
Kipindi cha likizo ya kumaliza form 4 watu walijichimbia mchikichini na tuition center kupiga mapindi.. Mie nilikuwa najilia zangu bata.. Sasa siku ya kwanza nareport school nakuta madam wa phyics anapiga pindi la measurements, nikaenda zangu kukaa kiti cha nyuma kabisa, kutupa jicho ubaoni naona mapicha picha tu, kidogo sijakaa vizur madam ananiita na kuniuliza swali, halaf njemba sijui kitu nikaona leo maseke, nikamwambia tu sijui kitu, wacha anichane we hujui kitu bado umechelewa kuripoti shule, na bado unakaa nyuma, kuanzia leo ukae mbele, darasa lote halina mbavu.
Kutokana mie katuni nikamwambia ticha usipate tabu nipe siku 3 tu ntakuwa safi ila mbele sikai sababu macho yangu hayaoni karibu maana hata yeye mwenyewe simuoni vizur kwa jinsi tulivyokaribu kicheko kikaongezeka.. Baadae alikuja kuwa swahiba wangu mzuri tu, kama ningekaza ningeruka pale..
Physics yoote ya 4m 5 naikumbuka mpaka leo hii
Nakumbuka nilikuwa mie na mwanangu jonii kutumia measurement tukajidai kitengeneza formula ya kwichi kwichi(kokojoa), tukasaka vitu muhimu katika kwichi kwichi kama vile friction force, heat, velocity n.k halafu hisia tukaweka costant(K)[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji85] [emoji85] [emoji85]