Phyz ilikuwa ngumu sana lakini nilikomaa naye na ikanitoa kimasomaso NECTA.
Miongoni mwa somo lililokuwa linanipanikisha kwenye pepa ilikuwa ni Phyz.
Sikuwahi kumaliza pepa hata moja la physics, siku moja nilienda kupiga mtihani(series) kwa mtiga ilikuwa pepa one.
Mechanics ilikuwa imesimama aisee, kila swali nikigusa haliendi na lina concepts mpya. Muda wa masaa 3 nauona kama lisaa limoja.
Baada ya Mechanics kugoma nikahamia swali la Environmental Physics nikajipoza kidogo kabla navuta pumz nasikia muda umeisha, nikapanic sana. Nilirudi shule nimenuna sana.
Sikukata tamaa nikakaza buti zaidi, wiki inayofuata nikarna tena kupiga series nyingine ambayo ilikuwa pepa two.
Kufika kituoni nikakuta matokeo ya wiki iliyopita yamebandikwa, nikajikuta nipo top ten japo niliambulia 40%, kuona hivyo nikajisemea kumbe mambo yanawezekana hapa. Nikaingia kupiga pepa na kwenye pepa hiyo nikawa na above 50% nikaingia top ten pia.
Kuanzia muda huo nikawa sikosi series kila wiki huku nikikomaa kusahihisha makosa yaliyojitokeza kwenye series zilizopita, ikafika muda nikaimprove na pepa moja nikawa wa kwanza. Hadi hapo nikacha kwenda kupiga series tena.
Physics ni somo nililotumia muda mwingi na pesa nyingi kulisoma kuliko masomo mengine.