Afande Meki wa Oyster Bay Polisi, kwa kumrusha kichura babu yangu (73) lazima upatwe na la kukupata

Nazjaz

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
7,730
Reaction score
9,088
Afande Mecky, mwembamba mrefu na mweupe, ulikuwa bodyguard wa RPC, juzi umemusha babu yangu kichura na umri wake wa miaka 73.

Mzee sasa anaumwa na hawezi hata kwenda kujisaidia haja ndogo.

Sababu ya mateso yote hayo eti kapita kwenye nyumba za polisi.

Sisi mambo ya shirki hatuna na hatuyajui, ila tunaamini kwenye kitu kimoja tu, mwana kulitafuta mwana kulipata.

Kitakachokupata itakuwa gumzo kwa polisi wenzako wasio na adabu hata kwa watu wenye umri wa babu zao.
 
Miaka 73 sawa na King Charles, King Chalz anakimbia kabisa yule, mambo ya jogging, squat, kuruka kamba c unajua tena ila sisi wabongo ndio vile tena....![emoji23]

Joking, Pole sana Mkuu...kama nayeye ana wazazi au Watoto Mungu atamlipiza
 
Wakipita kambi za JW wakirushwa kichura,hampigi kelele,wakipita kambi za polisi na kurushwa kichura,kelele zinaanza.
Je wafanyaje?
Kuishi nao uraiani,kusiwafanye mkawazoea sana.Ni askari hao.
 
Huyo mzee muiga hakupaswa kukubali bora angemruhusubampige kama angetaka.
Nchi hii tumezidi uoga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…