Afande Muliro: Atakayethubutu kuandamana Dar es Salaam kesho atakiona

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
WAKATI mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe akitangaza uwepo wa Maandamano ya Chama hicho Siku ya jumatatu September 23 ,Jeshi la Polisi Nchini limeweka mkazo wake kuwa piga marufuku maandamano hayo .

Kuwa maandamano hayo yana viashiria vyote vya uvunjifu wa amani Nchini.

Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro ametoa Kauli hiyo leo Jumapili Septemba 22.2024) kuwa Jeshi hilo lilipokea taarifa ya chama hicho kuhusu dhamira ya kufanya maandamano hayo, taarifa ambayo ilijibiwa kwa kuelezwa kuwa maandamano husika yamepigwa marufuku hivyo yeyote atakayefanya kinyume na hapo atashughulikiwa kikamilifu kwa mujibu wa sheria

Hata hivyo alisema kumekuwa na kauli zinazoashiria wazi kuwa maandamano hayo yana lengo la kuvuruga amani nchini kutokana na kauli tofauti zinazotolewa na viongozi wa CHADEMA na kwamba Jeshi la Polisi kama wasimamizi wa sheria na wenye jukumu la kuhakikisha ulinzi wa raia na mali zao (amani) hawako tayari kuruhusu kufanyika kwa matukio ya namna hiyo

"Maandamano yale yamepigwa marufuku, wao wametoa taarifa na sisi tumewapa taarifa, kwa hiyo wakifanya kinyume sasa tutachukua hatua kali za kisheria za kuyazuia na kushughulika na watu watakaojihusisha na maandamano hayo vikali na kwa mujibu wa sheria" -SACP Muliro

Hata hivyo Muliro aliwataka wananchi kutohudhuria maandamano hayo kwa kuwa yamepigwa marufuku, na kwamba marufuku hiyo imetokana na kauli na matamko ynayotolewa na viongozi wa chama hicho hivyo kudai kuwa maandamano hayo hayatakuwa ya amani kama inavyoelezwa badala yake dhamira ya maandamano hayo ni kuvuruga amani

"Jeshi la Polisi kama taasisi tumeshatoa tamko kwamba watu wasishiriki, wasijitokeze kwenye maandamano hayo, lakini watu wema waendelee na shughuli zao za kawaida mbalimbali za ujenzi wa Taifa, ujenzi wa kiuchumi na masuala mengine ambayo yanasaidia watu kujenga ustawi wa maeneo yao" -SACP Muliro

Mapema leo Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo ( CHADEMA)Taifa Freeman Mbowe kupitia mitandao ya kijamii akisisitiza uwepo wa maandamano kesho jumatatu .

Mbowe ametoa Msimamo huo wakati akizungumzia Msimamo wa CHADEMA kupitia 'X space' leo, Jumapili Septemba 22.2024 Mbowe amesema kuwa maandamano hayo yatahusisha njia mbili ambazo ni Magomeni kupitia Barabara ya Morogoro mpaka viwanja vya Mnazi mmoja na njia ya pili ni ile inayotoka Ilala Boma Sokoni kupitia Barabara ya Uhuru mpaka viwanja vya Mnazi mmoja, ambapo kwa lugha rahisi viwanja vya Mnazi mmoja ndipo sehemu ya makutano ya maandamano hayo

Mbowe amesema maandamano hayo yanatarajiwa kuanza majira ya saa 03 asubuhi, hivyo kutoka wito kwa wafuasi wa chama hicho na Watanzania kwa ujumla wake kujitokeza kwa wingi kushiriki bila woga wowote kwa kuwa maandamano hayo ni ya amani.

Soma Pia:

Source: Matukio Daima
 
Ndugu zangu Watanzania,

Sitaki kuwa na Maneno Mengi.ila nawasogezeeni habari hii kuwa kamanda wa Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam SCAP Jumanne Mulilo,amesema ya kuwa hakuna maandamano yatakayofanyika Dar es salaam.na kwamba Atakayethubutu Kuandamana atakiona .

Mimi Mwashambwa Lucas ,siandiki mengi sana ila nitaandika kesho pale ambapo atajitokeza mtu kuandamana katika maandamano haramu na yaliyopigwa marufuku. Nawaonea huruma sana ambao watajitoa akili na kuingiza pua zao barabarani.kwa hakika watatamani siku hiyo isingekuwepo na watailaani siku hiyo.

Nawaambieni tena chezeni na vyote lakini msichezee na amani ya Taifa letu na wala msichezee wala kuigusa siku ya kesho kwa kuingia barabarani.mtajuta majuto ya Karne.
Screenshot_20240922-221912_1.jpg

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Sitaki kuwa na Maneno Mengi.ila nawasogezeeni habari hii kuwa kamanda wa Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam SCAP Jumanne Mulilo,amesema ya kuwa hakuna maandamano yatakayofanyika Dar es salaam.na kwamba Atakayethubutu Kuandamana atakiona .

Mimi Mwashambwa Lucas ,siandiki mengi sana ila nitaandika kesho pale ambapo atajitokeza mtu kuandamana katika maandamano haramu na yaliyopigwa marufuku. Nawaonea huruma sana ambao watajitoa akili na kuingiza pua zao barabarani.kwa hakika watatamani siku hiyo isingekuwepo na watailaani siku hiyo.

Nawaambieni tena chezeni na vyote lakini msichezee na amani ya Taifa letu na wala msichezee wala kuigusa siku ya kesho kwa kuingia barabarani.mtajuta majuto ya Karne.View attachment 3103675

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Vunja Miguu kenge hao
 
Back
Top Bottom