Afande Sele hafahamu kuwa miradi iliyotekelezwa na Rais Samia kipindi hiki ni mingi kuliko wakati mwingine wowote?

Sisi tunakushangaa wewe unaemshangaa Afande sele.
 

Tozo muwatoze wananchi halafu sifa mnampa mama Samiah. Ulitakiwa kwanza uwasifu wananchi ndio umsifie mama Samiah.
 
Tutajitegemea kwa kadri ya uwezo wetu na pale juhudi zetu zitakapoishia Basi ndio tutatafuta namna ya kuunganisha nguvu zetu kwa kuomba mikopo ya mashariti nafuu na yasiyo ya kuhatarisha Uhuru na usalama wetu na Rasilimali zetu, tutakopa kwa Yale tunayaona nguvu zetu pekee hazitamaliza kwa haraka, Hatutakopa kwa kila kitu hata kwa Yale tunayoweza kuyafanya wenyewe kwa nguvu na jasho letu,

lazima tujibane kidogo kuijenga nchi yetu, Hii ndio njia waliyopita wenzetu pia, njia ya maendeleo siyo ya mkato, inahitaji kujitoa na kujitolea, inahitaji uvumilivu ,inahitaji juhudi, inahitaji uzalendo, inahitaji umoja na mshikamano, watanzania Hatuna budi kumuunga mkono mh Rais wetu mpendwa katika mapambano ya kuijenga nchi yetu
 

Tozo+Kodi+ mikopo+ misaada
 
Ni tozo hizo zilizopelekea kusogezwa kwa huduma karibu ya mwananchi, watanzania wameridhishwa na namna miradi ilivyotekelezwa kutokana na tozo, kila mtu anajivunia mafanikio tuliyoyapata kwa kuwa tunajuwa Ni nguvu zetu
Punguza ujinga basi au na wewe ni miongo mwa walamba asali
 
Tozo muwatoze wananchi halafu sifa mnampa mama Samiah. Ulitakiwa kwanza uwasifu wananchi ndio umsifie mama Samiah.
Wananchi wamepongezwa na nimekuwa nikiwapongeza Sana kwa moyo wao wa uzalendo wa kuamua kumuunga mkono mh Rais wetu mpendwa katika juhudi hizi za kuijenga nchi yetu kwa mikono yetu wenyewe,

Nimekuwa nikimpongeza mh Rais wetu mpendwa kwa kuwa amefanya kazi ya kutukuka katika kuhakikisha kuwa fedha hizi na kila Senti inayopatikana inatumika vizuri na kuwa hakuna wa kuichezea hovyo na akibainika mtu kagusa anawajibishwa kwa haraka

Lakini pia mh Rais wetu mpendwa nampongeza kwa kuchagua na kuongoza njia hii aliyoichagua kwani ndio njia waliyopita wenzetu waliyopiga hatua kimaendeleo, njia inayotutaka kuwa wazalendo kujitolea kwa ajiri ya nchi yetu na kujivunia kwa pamoja mafanikio yatakayopatikana
 
Tunataka tujitegemee, hatutaki tukope kwa kila kitu hata vilivyo ndani ya uwezo wetu, lazima Sasa tuanze kujibana ili kuijenga nchi yetu kupitia vipato vyetu, Hatutaki mzigo wa madeni uwe mkubwa kuliko mabega yetu

Kuna wakati mnatulazimisha tupigwe ban bila sababu.

Unaweza kuchambua zahanati, shule, madarasa, miradi ya maji iliyojengwa awamu ya Tano na sita kabla ya tozo? Kisha uweke hapa tozo zimeanza kukusanywa lini, kiasi Gani kimepatikana, na uweke madarasa, shule, zahanati na miradi ya maji iliyojengwa Kwa pesa za tozo?

Kumbuka tumeendelea kukopa na kupokea misaada tukiambiwa hizo pesa zinafanya miradi hiyo hiyo.

Waziri mwenyewe alijipiga kifua kuja kutufafanulia tozo, umeshuhudia mwenyewe kilichotokea na kinachoendelea Hadi chama na serikali wanatafutana. Sie wananchi sio wajinga kiasi hicho.
 
Lakini serikali ilitangaza changamoto imeisha.
Iliisha kwa kumaliza kero Ile ya wanafunzi wengine kwenda muhula wa pili unapoanza, lakini saiz hata kabla wanafunzi hawajachaguliwa tayari serikali imeshaweka mkakati wa kujenga vyumba karibu elfu nane ili wanafunzi wakute tayari yamekamilika kuliko zamani ambavyo ulikuwa ukiona viongozi wakikimbizana na wananchi mwezi December Hadi January kujenga madarasa Hadi mengine kujengwa chini ya viwango kutokana na uharaka
 
Miradi ipi hiyo na unalinganisha na kipindi gani wakati wa nani tujue nanlist hapa
 
Yote yalishatolewa kitakwimu na serikali Kama ambavyo hata majuzi ukisikia vituo vya Afya 234 vimejengwa, Takwimu zipo ukihitaji kuzipata maana serikali imekuwa wazi Sana
 
Ni tozo hizo zilizopelekea kusogezwa kwa huduma karibu ya mwananchi, watanzania wameridhishwa na namna miradi ilivyotekelezwa kutokana na tozo, kila mtu anajivunia mafanikio tuliyoyapata kwa kuwa tunajuwa Ni nguvu zetu
Kodi inakazi gani
Mikopo inakazi gani
Ushuru
Tozo we buana aliyekutuma mwambie kabisa mamilioni ya watanzania tumemwelewa sele ila wewe na yeye hapana
 

Unasema wananchi wanamuunga mkono Rais, je huyo Rais aliwauliza Kama wanakubaliana na hiyo tozo yao.
 
Kinacho fanywa na mtoa mada ni sawa na usaliti uliofanywa na vibaraka wakati wa ukoloni, kutetea watesi wetu(watu weupe) ili waendwlee kunyonya ndugu zao kwa ahadi za kupewa sigara na pombe kutoka ng'ambo. Kwa sasa wanyonyaji ni wenzetu!!! Very sad.
 
Yote yalishatolewa kitakwimu na serikali Kama ambavyo hata majuzi ukisikia vituo vya Afya 234 vimejengwa, Takwimu zipo ukihitaji kuzipata maana serikali imekuwa wazi Sana

Weka hapa tozo imekusanywa kiasi Gani na imetumikaje?

Kumbuka tozo zimeanza kukusanya lini na hivyo vituo vya afya vimekamilika lini? Mnaleta majibu mrpesi kwenye mambo ya msingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…