Afande Sele hafahamu kuwa miradi iliyotekelezwa na Rais Samia kipindi hiki ni mingi kuliko wakati mwingine wowote?

Afande Sele hafahamu kuwa miradi iliyotekelezwa na Rais Samia kipindi hiki ni mingi kuliko wakati mwingine wowote?

Ndugu zangu Afande sele kawashangaza Sana mamilioni ya watanzania ambao wanaendelea kuhoji kuwa Ina maana Afande sele hajaona ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia madarakani alivyojenga na kuboresha secta ya Elimu hapa nchini? Watanzania wanahoji kuwa Afande sele amesahau Mara hii namna watanzania walivyokuwa wanahaha kulipa michango ya ujenzi wa vyumba vya madarasa Hadi wengine kukimbia Kaya zao?

Wanauliza je, hakuona mh Rais wetu mpendwa akitoa fedha kwa ajiri ya kwenda kujenga vyumba vya madarasa kila shule? hakuona miaka ya nyuma wengine wakienda muhula wa pili kuanza masomo yao kwa kuwa tu hakukuwa na madarasa ya kutosha? Je wangekuwaje sawa na waliolipoti mwezi wa kwanza?

Wanauliza Kwamba huyu msanii hajaona namna uamuzi wa serikali wakufuta Ada ya kidato cha tano na sita ilivyoweza kuwasaidia watoto wa wanyonge kupata Elimu bila shida? Wangapi walikuwa wanashindwa kuripoti shule kwa kukosa Ada? Je haoni Jambo hilo limeleta neema kwa familia masikini? Huyu msanii haoni kuwa hizo Ni faida za Tozo zetu?

Huyu msanii kwamba hajaona namna zahanati na vituo vya Afya vilivyosambazwa kila Kona ya nchi hii ndani ya muda mfupi wa Rais Samia? Kwamba hajaona wananchi walivyopunguziwa adha ya kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma za Afya? Haoni suala Hilo limesaidia hata wamama wajawazito kujifungulia hospitalini na hivyo kupunguza hatari ya kutokea kwa vifo vya mama na mtoto?

Huyu msanii haoni namna huduma za maji zilivyosogezwa Hadi vijijini na hivyo kupunguza Ile kero ya watu kuamka alfajiri kutafuta maji toka kilometa kadhaa? Anadhani pesa hizo zimetoka wapi? Au alitaka watanzania waendelee kuhenyeka kufuata maji umbali mrefu?

Huyu msanii hajaona juhudi za serikali kuinua maisha ya mkulima kwa uamuzi wake wa kutoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini? Haoni namna ambavyo kwa Sasa mbolea inapatikana kwa Bei nafuu ya elfu 70 kwa DAP ambayo msimu uliopita iliuzwa kwa laki na 40? Haoni Jambo Hilo litachochea uzalishaji kuongezeka msimu ujao! Haoni kuwa uchumi wa mkulima unakwenda kuinuka hasa ukizingatia Ni secta iliyo ajiri kundi kubwa la watanzania na ndio pumzi ya watanzania wengi

Hapana siyo kuwa haoni Bali kaamua tu kujipa upofu na kufanya upotoshaji kwa umma ambao hata hivyo umempuuza tu, watanzania hawamshangai maana bado wanakumbuka kuwa amewahi kuvua nguo jukwaani,kwa hiyo wanaona anatatizo linalohitaji ushauri wa kisaokolojia

Watanzania wanaendelea kumuunga mkono mh Rais wetu mpendwa, maana wameona juhudi zake katika kuijenga nchi yetu na maendeleo yaliyopatikana na namna yalivyogusa maisha ya watanzania kwa kupunguza kero zilizokuwa kidonda ndugu kwao

Watanzania wanasema Tanzania itajengwa na sisi watanzania, hatuwezi tukakaa tu ili wenzetu walipe Kodi na Tozo huko kwao halafu sisi tuletewa huku, Hatutaweza Kuendelea na aibu hiyo, Sasa Tumeamua kuijenga Tanzania yetu na mh Rais wetu mpendwa Samia ameongoza njia hiyo na watanzania tunamuunga mkono

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia watanzania walipo
Wewe ndiye unauliza na sio WaTanzania.
Enzi ya JPM alikuwa anaenda saiti na kushuhudia Sasa hivi anatoa pesa nendeni mkatekeleze! Matokeo yake Ina Waziri Mkuu anavyokomalia ULAJI na upotevu wa Fedha!
Je umeiona kibanda ya mlinzi kujenga Kwa mil. 11 kama sio maajabu!
Huo mchanga na sementi waliagiza nje?? Wewe endelea kuupokea buku 7 ujekuleta uzi wa sifa?? Bogus!
 
Kipofu pekee yake ndo hawezi kupongeza jitihada anazifanyia Rais wetu, katika kata ya Businde wilaya ya Kyerwa: shule ya sekondari Businde imejengewa vyumba vya madarasa vipya vitano, shule ya msingi Omunchwekano kumejengwa vyumba vitatu vipya vya madarasa, hiyo ni kata moja na sasa kuna maandalizi ya kujenga Kituo Cha afya, ajira za kada muhimu ktk maisha za afya na elimu zimetolewa hata kama hazitoshi Ila nia inaonekana, miundo mbinu inaendelea kujenga labda kwa mtu asotembea kujionea, huo ni mwanzo na mara zote mwanzo ni ngumu.
 
Hao Watanzania ni kina nani na wanapatikana wapi ?

Brother you are out of touch..., Afande Sele ndio ana-represent mitizamo ya wadau wengi huku kitaa na kama mtaendelea kuziba masikio na kujifariji mtajikuta mnajenga ukuta badala ya kuziba ufa....
View attachment 2352672
Nipo mtaani naona uhalisia wa namna mh Rais wetu mpendwa anavyokubalika na watanzania
 
Nipo mtaani naona uhalisia wa namna mh Rais wetu mpendwa anavyokubalika na watanzania
Mtaa Gani wakati watu wanalia bei ya vyakula vipo juu na tozo zipo kila sehemu yaani bei za vitu vipo juu na hapohapo tozo zinawekwa kila sehemu watu wa mtaani kwako wakikusikia watakuzingua.
 
Mtaa Gani wakati watu wanalia bei ya vyakula vipo juu na tozo zipo kila sehemu yaani bei za vitu vipo juu na hapohapo tozo zinawekwa kila sehemu watu wa mtaani kwako wakikusikia watakuzingua.
Vyakula vipi wanavyolia Bei kuwa juu,
 
Tunataka tujitegemee, hatutaki tukope kwa kila kitu hata vilivyo ndani ya uwezo wetu, lazima Sasa tuanze kujibana ili kuijenga nchi yetu kupitia vipato vyetu, Hatutaki mzigo wa madeni uwe mkubwa kuliko mabega yetu
Ha ha haaa, kumtetea huyu bibi mzururaji huku akipitisha kopo la kuomba omba mtapata tabu. Nothing new with this ajuza. Anaomba, anahongwa mihela kibao analeta nchini, asilimia zaidi ya 70 anafuja na top leaders wake, masikini wanakamuliwa tozo za kiwizi wizi ambazo nazo zaishia mikoba ya vibaka wake.

Tozo ni wizi wa wazi, kataa tozo!!!
 
Kwanza tumia lugha ya Hekima na busara ndio upate kujibiwa, uwe na heshima na adabu kwa mh Rais hata Kama wewe haujapata malezi ya wazazi wako
 
Hivi huoni saizi namna huduma za serikali zilivyo boreshwa kuanzia mahospitalini Hadi shuleni, Sina wasiwasi na huduma za serikali na hata nipatwe na shida nitakwendaa hukohuko serikalini kupata huduma
Jibu ulichoulizwa sio porojo za urojo wa mtu aliyevimbewa ngisi. Aliyekutuma mwambie aache kuibia wananchi, tumechoka!
 
Kwanza tumia lugha ya Hekima na busara ndio upate kujibiwa, uwe na heshima na adabu kwa mh Rais hata Kama wewe haujapata malezi ya wazazi wako
Wezi wa awamu hii mnavaa ustaarabu fulani kumbe majizi balaa tena mnaibia mpk vipofu na walemavu. Kuna siku Mungu atawaumbua tu.

Wewe na lile bibi lako wote wezi tu....nasema achezi kuibia watu, wizi ni dhambi, wizi ni haramu! Mtaumbuka siku 1
 
Usitukolezee nazi kwenye kachumbali yenye ndimu Kali.......hiyo miradi labda ya tozo .....uko mnaupiga mwingi
 
Wezi wa awamu hii mnavaa ustaarabu fulani kumbe majizi balaa tena mnaibia mpk vipofu na walemavu. Kuna siku Mungu atawaumbua tu.

Wewe na lile bibi lako wote wezi tu....nasema achezi kuibia watu, wizi ni dhambi, wizi ni haramu! Mtaumbuka siku 1
Sihitaji kijibizana na wewe maana umejaza matusi matupu, Mimi huwa sijibu matusi, Mungu akujalie moyo wa hekima na busara tu, Nachokuasa Ni kuwa uwe na heshima na adabu kwa mh Rais, Kama unataka wewe nishambulie na kunitukana Mimi kwa kadri uwezavyo kutukana lakini uwe na adabu kwa mh Rais wetu mpendwa
 
Mpendwa wa nyoko
 
Zahanati zilijengwa na mashule kibao zama za BRN. Sasa maajabu gani ya kushangaza utawala huu eti tozo zimejenga choo cha shule. Ujinga sana
Huyu mataga mleta post alikuwa hajazaliwa kipindi cha BRN ,kwa sasa ndiyo anadhani ndiyo tumepata uhuru.
 
Back
Top Bottom