Afande Veronica yupo barabarani kukusanya hela au kufilisi Raia?

Duh kazi ipo.
 
Ninajiuliza sana swali hili- - Kwanini polisi wanapenda sana hela ? Kuna wengine wanapokea hata rushwa ya elfu moja toka kwa wapiga debe. Inanisikitisha.
 

Kuwe na taa kuongoza Zebra crossing zote muhimu.

Hii itaondoa rushwa. Pia kuwe na camera ku-record kila kitu.

 
Iyo pesa una pewa risiti au mna yamaliza kimya kimya tuanzie apo kwanza
Inadaiwa wanaambiwa wakusanye kiasi fulani kwa siku la sivyo wanahamishwa wanapelekwa Nangurukuru. Je, faini ina uhalali? Nimesimama mwenyewe kupisha watu, wakiisha naondoka mwingine anaamua kupita anakimbia then unapigwa faini. Wewe kama Polisi kwanini hukusimamia watu kuvuka? Yeye anasimama pembeni ya barabara anaangalia tu. Lakini sababu pale Trafiki walipo kuna zebra, alitakiwa baada ya kuona watu wa kuvuka wamejaa, alitakiwa asimamishe magari watu wavuke then aruhusu magari. Sio Dreva wanajisimamisha wenyewe watu wanavuta, then akiondoka unamwambia apark pembeni kwamba Uliondoka watu hawajaisha. Dar wavuka barabara wanaisha?
 
Tumia Dash Cam DVR Camera.

Mimi popote wanaponisimamisha wanaiona Camera wanakwenda moja kwa moja kwenye point naomba leseni ya udereva, namwonyesha. Naomba kadi ya gari, nampatia alafu ananiambia nenda.
 
Acha majungu jomba hao watu hawana kazi ya kufanya mpaka wawekwe na polisi kuvuka zebra.
Hujiongezi kwamba nao wanapata cha Kwao hapo? Kazi gani zilizopo za kuwaingizia pesa kirahisi zaidi ya hiyo?
 
Soma tena alichoandika.
 
ujamuelewa. Anacho lalamikia ni kwann kila siku ni naru wale wale wanaochelewa kuvuka/wanaotaka kuvuka gari likitaka kuondoka?
 
majungu tu unaleta hapa.

kubeba jina zima la mtu anayekuhudumia eti una malalamiko naye ni uzwazwa.

watu watajuaje kama huna visa naye!!!
Hapa ameokoa wengi sana,siku yakikukuta utaelewa,hakuna watu wa hovyo kama askari wa barabarani........wapiga dili wengine pale Ubungo External
 
Kuna traffic wanakaa mbezi malamba mawili, kila siku asubuh wanachaji bajaji zote zinazopita njia ya malambamawili kwenda mbezi buku, nadaladala zote zinazoenda mbezi - temeke, mbezi- gmboto mbezi - kinyerezi zote zinachajiwa 2000,

Yaan nikisema zote namanisha zote zitakazofanya kazi kwasiku hiyo. Wanakaa kila siku zaweek saa 12 mpaka saa 5 asubuh
 
Je Polisi ipo namba ngapi kwenye orodha ya rushwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…