TheCrocodile
JF-Expert Member
- May 31, 2021
- 1,199
- 3,307
Abdel Raphael (42) Mkazi wa Mtaa wa Uwanja halmashauri ya mji Geita amekutwa amefariki ndani kwake akiwa kwenye mfungo wa siku 30 akitarajia kufufuka Desemba 8.
Mmoja wa waumini waliokuwa wakishiriki ibada ya pamoja na marehemu ambaye alikuwa mchungaji wao anasema marehemu aliwaaminisha kuwa ifikapo Desemba 8 atafufuka lakini kufikia siku hiyo akawa amefariki na mwili wake kuharibika.
"Tulikuwa tumefunga tangu tarehe 28 mwezi wa 11 ilivyofika tarehe 2, kwenye chumba chake cha maombi kumcheki alikuwa mzima, tarehe 3 kwenda kumwangalia ile hali ilitutisha tukakuta ameanguka kitandani, yupo kifua wazi, yupo kwenye bukta, ikabidi tumkusanye miguu, tumuoshe vizuri. Tukamfunika mdomo, macho vizuri, tukamlaza vizuri, halafu tukaenda kutoa taarifa katika uongozi wa mtaa kwa ajili ya taratibu zinazofuata", amesema Jumanne Zuberi ambaye ni muumini mwenzake.
Chanzo: East Africa Radio