Afariki akiwa kwenye mfungo wa siku 30, aliahidi kufufuka Desemba 8

Afariki akiwa kwenye mfungo wa siku 30, aliahidi kufufuka Desemba 8

Hivi kanda ya ziwa kuna shida gani psychiatric cases ni nyingi mno au kwa kua mnaamini mna akili nyingi?
 
"In my culture, death is not the end. It’s more of a stepping off point, you reach out with both hands and Bast and Sekhmet, they lead you into a green veld where you can run forever."

King T'challa.
 
Abdel Raphael (42) Mkazi wa Mtaa wa Uwanja halmashauri ya mji Geita amekutwa amefariki ndani kwake akiwa kwenye mfungo wa siku 30 akitarajia kufufuka Desemba 8.

Mmoja wa waumini waliokuwa wakishiriki ibada ya pamoja na marehemu ambaye alikuwa mchungaji wao anasema marehemu aliwaaminisha kuwa ifikapo Desemba 8 atafufuka lakini kufikia siku hiyo akawa amefariki na mwili wake kuharibika.

"Tulikuwa tumefunga tangu tarehe 28 mwezi wa 11 ilivyofika tarehe 2, kwenye chumba chake cha maombi kumcheki alikuwa mzima, tarehe 3 kwenda kumwangalia ile hali ilitutisha tukakuta ameanguka kitandani, yupo kifua wazi, yupo kwenye bukta, ikabidi tumkusanye miguu, tumuoshe vizuri. Tukamfunika mdomo, macho vizuri, tukamlaza vizuri, halafu tukaenda kutoa taarifa katika uongozi wa mtaa kwa ajili ya taratibu zinazofuata", amesema Jumanne Zuberi ambaye ni muumini mwenzake.

View attachment 2447111

Chanzo: East Africa Radio
Mbona habari ina utata hii,kama alikuwa kwenye mfungo wa siku 30 ilikuwaje akasema atafufuka December 8?ilikuwaje mfungo wa kifo?
 
Hivi mwanaume asipokila lazima afe baada ya siku ngapi?
Na mwanamke asipokula lazima afe baada ya siku ngapi?

Yaani walivyomkuta yupo hio ilibidi wampe chakula pale pale angeamka.

Wenzake ni wajanja walikuwa wakitoka kwenye maombi wanapiga msosi.

Biblia imesema tutafufuka siku ya mwisho sasa inakuwaje yeye afufuke trh 8 mbona leo trh 17?
Kuna watakatifu wake Mungu wanagonga siku 13 - 14 bila ya kula chochote wala kunywa maji, hakika uwezo wa Mungu umepitiliza akili na maarifa yetu sisi Binadamu.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
watu ni wajinga kwakweli nilienda kanisa fulani watu et wanafunga siku saba kavu yaani ni walikuwa na hali mbaya mpaka wengine ni kama akili.zimewaruka
bahati nzuri sikusikia kesi ya kifo ila hali zilikuwa mbaya
Jaribu nawe kufunga hizo siku 7 kavu uone kama Mungu anajaribiwa, hao ni Mashujaa wa imani na hawatakuwa na hali mbaya milele sababu kila jambo huwa lina wakati wake.

MUHUBIRI 3:1-15.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Hivi mwanaume asipokila lazima afe baada ya siku ngapi?
Na mwanamke asipokula lazima afe baada ya siku ngapi?

Yaani walivyomkuta yupo hio ilibidi wampe chakula pale pale angeamka.

Wenzake ni wajanja walikuwa wakitoka kwenye maombi wanapiga msosi.

Biblia imesema tutafufuka siku ya mwisho sasa inakuwaje yeye afufuke trh 8 mbona leo trh 17?
Ukimkuta mtu amekaa muda mrefu bila kupata chakula wala maji usijaribu hata siku moja kumpa chakula ale maana atakufa papo hapo cha kufanya.

Mkorogee glucose kama ipo anywe halafu subiri kama 30 min halafu mpe uji mwepesi lishe wa moto fanya hiyo lishe ya uji kwa wiki angalau moja asubuhi mchana na jioni huku ukiongeza na matunda baada ya hapo ndo aanze kula chakula sasa .

N.b
Ukishamkorogea glucose ni vyema ukamuwaisha kwenye kituo cha afya ili kujiepusha na kesi zisizo na ulazima .

Na jibu lako la kwamba mwanaume (na pia mwanamke) anakaa siku ngapi bila kula ni hili hapa

1. kama akiwa anakunywa maji pekee ataweza kufikisha hadi miezi miwili ila.

2. Kama hanywi hata maji basi wiki mbili ni nyingi
 
Mimi nikiona mtu yupo deep sana kiimana namkalia mbali. Afrika wamekuwa wajinga mno na haya mambo ya kiimani.
Naisi waafrika tuna shida,umeongea kweli,dhana ya dini ni mapokeo na ilikuwepo Toka mababu zetu na pia waliamini huyu mungu tunayemwamini sasa.Tatizo linakuja tunapovuka mipaka na kujiona ni wathamani na pia tunajua zaidi ya muumba wetu.Mungu aliweka chakula na mimea mbalimbali kwa ajili yetu ili itupe energy na tuweze kuishi na kufanya kazi.shida pia inaanzia kwa viongozi wenyewe namna ya kuwapa watu elimu hii.
 
Jaribu nawe kufunga hizo siku 7 kavu uone kama Mungu anajaribiwa, hao ni Mashujaa wa imani na hawatakuwa na hali mbaya milele sababu kila jambo huwa lina wakati wake.

MUHUBIRI 3:1-15.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
my friend mi huwa nafunga mpaka zile arobaini za kwaresma ila huwa najiangalia na natumia akili,yaani mtu mpaka unaona fyuzi zinakatika?mtu mpaka anaanguka kanisani hiyo ni akili?mtu unafunga mpaka unashindwa kuomba ebu nambie mtu njaa imekuzidi utapata wapi kumwomba Mungu?
Mda mwingine akili ni muhimu
 
Hivi mwanaume asipokila lazima afe baada ya siku ngapi?
Na mwanamke asipokula lazima afe baada ya siku ngapi?

Yaani walivyomkuta yupo hio ilibidi wampe chakula pale pale angeamka.

Wenzake ni wajanja walikuwa wakitoka kwenye maombi wanapiga msosi.

Biblia imesema tutafufuka siku ya mwisho sasa inakuwaje yeye afufuke trh 8 mbona leo trh 17?
Mwanaume siku 4 tu anadanja ila sisi ni siku 7
 
my friend mi huwa nafunga mpaka zile arobaini za kwaresma ila huwa najiangalia na natumia akili,yaani mtu mpaka unaona fyuzi zinakatika?mtu mpaka anaanguka kanisani hiyo ni akili?mtu unafunga mpaka unashindwa kuomba ebu nambie mtu njaa imekuzidi utapata wapi kumwomba Mungu?
Mda mwingine akili ni muhimu
Yeye alitaka kufa ili afufuke
 
Back
Top Bottom