Afariki akiwa kwenye mfungo wa siku 30, aliahidi kufufuka Desemba 8

Afariki akiwa kwenye mfungo wa siku 30, aliahidi kufufuka Desemba 8

watu ni wajinga kwakweli nilienda kanisa fulani watu et wanafunga siku saba kavu yaani ni walikuwa na hali mbaya mpaka wengine ni kama akili.zimewaruka
bahati nzuri sikusikia kesi ya kifo ila hali zilikuwa mbaya
 
Abdel Raphael (42) Mkazi wa Mtaa wa Uwanja halmashauri ya mji Geita amekutwa amefariki ndani kwake akiwa kwenye mfungo wa siku 30 akitarajia kufufuka Desemba 8.

Mmoja wa waumini waliokuwa wakishiriki ibada ya pamoja na marehemu ambaye alikuwa mchungaji wao anasema marehemu aliwaaminisha kuwa ifikapo Desemba 8 atafufuka lakini kufikia siku hiyo akawa amefariki na mwili wake kuharibika.

"Tulikuwa tumefunga tangu tarehe 28 mwezi wa 11 ilivyofika tarehe 2, kwenye chumba chake cha maombi kumcheki alikuwa mzima, tarehe 3 kwenda kumwangalia ile hali ilitutisha tukakuta ameanguka kitandani, yupo kifua wazi, yupo kwenye bukta, ikabidi tumkusanye miguu, tumuoshe vizuri. Tukamfunika mdomo, macho vizuri, tukamlaza vizuri, halafu tukaenda kutoa taarifa katika uongozi wa mtaa kwa ajili ya taratibu zinazofuata", amesema Jumanne Zuberi ambaye ni muumini mwenzake.

View attachment 2447111

Chanzo: East Africa Radio
Afadhali kafa yeye steering na picha linaishia hapo hapo kende malamu.
 
Mimi nikiona mtu yupo deep sana kiimana namkalia mbali. Afrika wamekuwa wajinga mno na haya mambo ya kiimani.
Nilihudhuria harusi moja , kabla ya sherehe tulikuwa na pilika za maandalizi huku tumechanganyika wanaume na wanawake. Mara ghafla likawekwa pazia eti kutengenisha wanaume na wanawake huku bibi harusi na bwana harusi wamekaa pamoja. Baada ya harusi watu wakachanganyika tena wanapiga stori. Wale ndugu zangu niliwachana live, waache huu upuuzi. Watu mmekuja mmechanganyika huko kwenye magari binafsi, daladala, siku za vikao mko pamoja halafu ghafla mnaweka pazia, ili iweje? Huko makazini mnachanganyika , misibani etc . Nadhani hawatarudia tena huu ujinga
 
Kuna andiko lolote linasema afanye hivyo au amejizulia tu mwenyewe?

Kama hakuna andiko linalotoa hayo maelekezo basi amejiua mwenyewe na njaa
Hata kama lingekuwepo unatakiwa utumie akili. Hivi itakuwaje nikikaa siku 30 bila kula? Mungu aliyeumba vyakula hakuwa mjinga. Wewe utoke tu huko ufunge siku sijui 20, huko ni kujiua kwa kukusudia
 
Back
Top Bottom