Afariki baada ya kudaiwa kulishwa saruji na askari wa JWTZ

Afariki baada ya kudaiwa kulishwa saruji na askari wa JWTZ

Usiniwekee maneno kinywani Kaka! Kwa Bahati mbaya hakuna aliyefanya uchunguzi kujua ukweli wa kilichosemwa! Lakini nasisitiza, Raia tuache dharau Kwa hawa jamaa, wanapitia Mambo magumu mno kuhakikisha Taifa liko salama!
Raia wanawaheshimu sana hawa jamaa ila sema BAADHI yao hawajiheshimu na hawajitambui nahisi kwa sababu ya elimu ndogo.

Tutawatuma wabunge walizungumzie bungeni hili suala si kwa sababu ya huu uzi ila tumeona mengi saa nyingine mpaka askr polis wetu wanadharrishw na hawa wajing.
 
Mkazi wa Kijiji cha Gumba kata ya Gwata Wilayani Kibaha mkoani Pwani, Bakari Mbagara (63) amefariki dunia kwa kile kilichodaiwa kupigwa na waya wa umeme na kulazimishwa kula saruji na askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Koplo Chibumba Lugola wa Kikosi cha 121 FIR Ngerengere.

Mbagara alifariki dunia Januari 2 na kuzikwa Januari 3 mwaka huu, katika makaburi yaliyopo kijijini cha Gumba.

Akizungumza na Mwananchi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani,Wankyo Nyigesa alikiri kutokea kwa tukio hilo huku akisema wanaendelea kumshikilia mtuhumiwa Lugola anayedaiwa kutekeleza mauaji hayo.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Raia wanawaheshimu sana hawa jamaa ila sema BAADHI yao hawajiheshimu na hawajitambui nahisi kwa sababu ya elimu ndogo.

Tutawatuma wabunge walizungumzie bungeni hili suala si kwa sababu ya huu uzi ila tumeona mengi saa nyingine mpaka askr polis wetu wanadharrishw na hawa wajing.
askari polisi mwenyewe hawawagusi hawa jamaa na ndiyo maana wale madereva wa malori huwa wanafurah sana wakiwa na mjeda pemben maana hawatosumbuliwa sana huko njian
 
Kusumbuliwa kivp
kuna jamaa mmoja wa malori wakat wa story za hapa na pale akasema kuwa maana si huwa wanaombaga lift unakuta wengine wanaenda mbali na yupo na sare zake sasa ikatokea walipigwa mkono Dereva kaenda wamechonga wee jamaa haelewi ile anarud kwenye gari yule mjeda akamuuliza vp mbona mnachukua muda sana akamwambia jamaa anataka hela na mm sina na haelewi basi yule mjeda akamwambia hebu subiri hapa hapa nikaongee nao basi baada ya mda anarudi anamwambia twende aisee hajui waliongea nini jamaa akawasha gar moto
 
Ahaa kumbe hivo sawa sawa kaka
 
askari polisi mwenyewe hawawagusi hawa jamaa na ndiyo maana wale madereva wa malori huwa wanafurah sana wakiwa na mjeda pemben maana hawatosumbuliwa sana huko njian

usiseme hawawagusi unajidanganya.
beba mbao,halafu pandisha mwanajeshi mbele tena mvishe na cheo cha kanal.
 
Huyu nae auawe kwa kunyongwa, death sentence kabisa, hivi si vitendo vya kuviendeleza hata kidogo, huyo mwanajeshi ni Jambazi mkubwa sana, kama Sabaya kabisa. Iwe mfano, naamini Serikali ya Mama Samia, hili ataonyesha mfano halisi. JWTZ haifundishi wanajeshi wake kuua raia wake, huyo atakuwa ni jambazi kwa tabia zake, auawe kwa kunyongwa kabisa.
 
Hawa jamaa ni wale wapuuzi majeuri, mwanajeshi hana mamlaka ya kumpiga raia kivyovyote na wala hiyo siyo kazi yake.
Na wao ni waajiriwa tu wa serikali kama waajiriwa wengine.

Kuna video moja na zipo nyingi youtube inaonyesha wanajeshi wa kimarekani wapo field yaani vitani wanacheza mpira na watoto wa kiarabu wa sehemu ile.
Jamaa wako humble kabisa wala hawana makeke sababu wanajua na wao ni binadamu tu ukiondoa zile gwanda.

Ila hawa jamaa wa kwetu huku wanajiona kama demigods fulani hivi baada kuvaa zile uniforms ni uonevu, ushenzi na uhuni.
Hii inaweza isiwe kwa wote lakini wengi wao wako hivyo.

Na watanzania wengi ni waoga na wala hawajui haki zao na ndio maana hawa jamaa wanapata nafasi ya kufanya hivi kwa kujiamini.
Mfanyie hichi mwananchi wa marekani lazima uishie pabaya sababu wananchi wanajua wajibu na haki zao.

Kuna video nyingine inaonesha askari mmoja mzee wa kimarekani mweupe amevamia gari ya blacks parking lot sababu alikuwa suspicious kwamba wanaweza kuwa waharifu na akawa anawadai vitambulisho na leseni kwa nguvu.
Wale jamaa wakagoma kutoa vitambulisho kwa kuwa walikuwa wamepark gari na ile sababu ya kuwa suspicious sio valid.
Akatishia kuita backup na wale jamaa wakasema wewe ita tu hiyo backup.

Baadae akaja askari mwengine naye ni mweupe jamaa alikuwa humble sana wakayamaliza faster tu.
Aliwaambia kwamba hakukuwa na sababu ya yule askari kuwafata wala kuwadai vitambulisho kivyovyote na akawaomba samahani kwa usumbufu uliojitokeza na kuwapotezea muda wao.
Yule boya bonge wa kwanza akafukuzwa kazi siku ileile bila kupepesa macho na yule mzee inaonesha alikuwa kwenye 60s means ana miaka zaidi ya 30 kazini bado kidogo astaafu lakini kwa ujinga wake kafukuzwa kazi na ile video ikaenda viral.

Yote hayo sababu jamaa walijua haki zao na wajibu wao kama wananchi.

Kuna video nyingine ni marekani inaonesha jamaa yupo kwake eneo la kwake anarecord kwa simu alafu anakuja Askari mmoja wa upepelezi anamwambia toka hapa sasa hivi!
Yule jamaa jeuri ila kwa upole akamuuliza Umelewa? huku amesimama palepale, askari akajibu unasemaje wewe?
Jamaa akasisitiza are you drunk?
Askari akakaza kwamba hapa ni kwangu na uondoke sasa hivi.
Jamaa akapanda kwa hasira kwamba hapa ni kwangu na wewe ndio uondoke! haiwezekani mimi nisimame kwangu alafu wewe unakuja kunilazimisha niondoke ili niende wapi?
Yule askari akaanza kuondoka taratibu huku akiwa mpole na yule mwenye nyumba akiendelea kuporomosha matusi kwa kizungu you Stop drinking at work BOY!, get outta here goddamnit.

Ila hapo mtanzania angetii kwa kwenda kulala hata kwa jirani sababu ya uoga na kutokutambua haki zake.
Huyu wa huku porini apigwe miaka mingi ili iwe fundisho kwa wajinga na waonevu wengine wote.
 
Daah anampa adhabu mtu mwenye miaka 60 ili iweje Tanzania imejaaa vijana wasio na malezi ya wazazi wote wawili hili ndio tatizo ni ngumu kwa kijana alielelewa vizuri na kummcha Mungu harafu akafanya upuuzi huo hata angekua na vyeo gani? hiyo Karma ya kuua mtu itatafuna uzao wake bila yeye kujua...
 
damu ya mtu haiendagi bure
 
Juzi walikaribia kumtesa mtu mmoja asiyekuwa na hatia pale makongo.
Jamaa alikuwa anatokea mwenge. Alipofika pale Getini VTC lugalo akakaomba msaada askari mmoja mlevi naye akamuita ndani wakaanza kumpiga
Ati wanamuuliza una simu kama hii halafu u makosa nauli?
Pumbavu sana hawa
Wanajeshi wamehitimu shule?
 
Back
Top Bottom