The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,017
- 19,506
Serikali inayoongozwa na Talibani nchini Afghanistan imepiga marufuku wanawake kuongea ama kubadilishana mawazo. Ni marufuku wanawake kuongea na mwanamke mwezake na kumuelezea mawazo ama maoni yake.
Khalif Hanif, waziri wa tabia njema na mwenendo mwema katika jamii amesema ni marufuku wanawake kuongea wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ni kinyume na mafundisho ya kiislamu hasa ya Mtume na Allah. Mwanamke aongee na mumewe tu.
Kumbuka hivi karibuni Talibani ilipiga marufuku saluni za kike na za kiume na kutangaza kwamba ni marufuku kwa mwananchi wa Afghanistan kunyoa nywele na ndevu kwani ni kinyume na mafundisho ya kiislamu. Pia Talibani ilipiga marufuku wanawake kupiga simu redioni ama mwanamke kuongea sauti yake ikasikika public.
View: https://x.com/HabibKhanT/status/1850241627530424578?s=19