Afghanistan: Vinyozi wapigwa marufuku kuwanyoa au kuwapunguza ndevu wanaume

Afghanistan: Vinyozi wapigwa marufuku kuwanyoa au kuwapunguza ndevu wanaume

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Wapiganaji wa Taliban wamepiga marufuku , vinyozi katika mkoa wa Helmand nchini humo kutowanyoa au kuwapunguza ndevu wanaume, wakisema hatua hiyo inakiuka sheria ya Kiislamu.

‘’Mtu yoyote anayekiuka sheria hiyo ataadhibiwa’’ , Askari wa Taliban wamesema. Baadhi ya vinyozi katika mji wa Kabul wamesema kwamba pia wao walipata maagizo kama hayo. Maagizo hayo yanasema kuhusu kurudishwa kwa sheria kali kama zile zilizokuwepo wakati kundi hilo lilipokuwa madarakani awali , licha ya ahadi ya kwamba litaanzisha serikali itakayokuwa na misimamo ya wastani.

Tangu ilipochukua madaraka mwezi uliopita, Talibani imewapatia adhabu kali wapinzani wake. Siku ya Jumamosi , wapiganaji wa kundi hilo, waliwapiga risasi na kuwaua watekaji wanne na miili yao kuzungunshwa katika barabara ya mkoa wa Herat.

Katika ilani iliochapishwa katika saluni, kusini mwa mkoa wa Helmand , maafisa wa Taliban walionya kwamba vinyozi lazima wafuate sheria ya Kiislamu katika kunyoa nywele za kichwani na ndevu. Hakuna hata mtu mmoja aliye na uwezo wa kulalamika, ilisema notisi ilioonekana na BBC.

"Wapiganaji hao wanaendelea kuja na kutuagiza kutonyoa ndevu’’, alisema kinyozi mmoja mjini Kabul’.
Mmoja wao aliniambia kwamba wanaweza kutuma maafisa kuchunguza ili kutukamata. " Kinyozi mwengine , ambaye anasimamia mojawapo ya saluni kubwa , alisema kwamba alipokea simu kutoka mtu aliyesema ni afisa wa serikali.

Walimtaka kutofuata mitindo ya Marekani na kutowanyoa watu ndevu zao. Wakati wa uongozi wa kwanza wa Taliban kuanzia 1996 hadi 2001, Kundi hilo lilipiga marufuku mitindo tofauti ya nywele na kusisitiza kwamba wanaume wafuge ndevu. Lakini tangu wakati huo, unyoaji wa ndevu na nywele fupi miongoni mwa wanaume wa Afghan umekuwa maarufu.
 
Hii sio dini ni mateso kwa wasiojitambua.... Toka lini mambo ya Mungu yakawa ya kulazimishana?
Hahahah si allah ndi anavyotaka😂
Yaan taab tupu
Lakin sasa vishehe vya bongo huko misikitin wanawasimanga simanga wakristo na mapungufu yao wanasahau ya kwaoa
Utasikia wakristo wanaibiwa
Sadaka wakat hata wao wanaombaga sadaka kwa kisingizio cha kutangaza din na kujenga misikiti
Wakat kaz inayofanya sadaka kwao inafanya hizo hizo kwa wakristo
Bado mashehe wanauza dua😂
Yaan ni mengi ila nikianza kuyaandika yote hawakawiii kuitaman shingo yangu😂
 
Hao Taliban ni wahuni tu, hawana lolote kwanza wameirejeshea nchi mikosi tena. Nimesikia kwamba tayari wameshaanza kughubikwa na njaa ambayo tayari imeathiri takriban watu milioni tatu.

Kitakachofuata hapo ni vita vya wenyewe kwa wenyewe wananchi hawatavumilia huo ujinga wao, tusubiri ni swala la muda tu.
 
Sasa itakuwaje mtuu unatembea na msitu wa ndevu
... tembea nao mola wako ni mjuvi wa wajuvi; je, haikumpendeza wa kiumeni wawe na nywele safu safu kukihusuru kinywa? Mola wako ni mjuvi wa yote!
 
Hii ndio dini hatari duniani na inatishia kuenea dunia nzima tayari imejikita kwenye mataifa makubwa ulaya na amerika
 
Back
Top Bottom