Afghanistan: Vinyozi wapigwa marufuku kuwanyoa au kuwapunguza ndevu wanaume

Afghanistan: Vinyozi wapigwa marufuku kuwanyoa au kuwapunguza ndevu wanaume

Taleban inapaswa kubadilika iachane na misimamo mikali ya kidini. Mungu halazimishi mtu mambo fulani, ametoa uwezo wa kufuata au kutofuata lakini hukumu yake utakutana nayo huko umautini. Hizi ni aina za siasa za kiimla tu wanazotumia taleban kutawala. Wanatawala mpaka nywele za wananchi hizi ni siasa za kijuha kuwahi kutokea duniani
 
Wapiganaji wa Taliban wamepiga marufuku , vinyozi katika mkoa wa Helmand nchini humo kutowanyoa au kuwapunguza ndevu wanaume, wakisema hatua hiyo inakiuka sheria ya Kiislamu.

‘’Mtu yoyote anayekiuka sheria hiyo ataadhibiwa’’ , Askari wa Taliban wamesema. Baadhi ya vinyozi katika mji wa Kabul wamesema kwamba pia wao walipata maagizo kama hayo. Maagizo hayo yanasema kuhusu kurudishwa kwa sheria kali kama zile zilizokuwepo wakati kundi hilo lilipokuwa madarakani awali , licha ya ahadi ya kwamba litaanzisha serikali itakayokuwa na misimamo ya wastani.

Tangu ilipochukua madaraka mwezi uliopita, Talibani imewapatia adhabu kali wapinzani wake. Siku ya Jumamosi , wapiganaji wa kundi hilo, waliwapiga risasi na kuwaua watekaji wanne na miili yao kuzungunshwa katika barabara ya mkoa wa Herat.

Katika ilani iliochapishwa katika saluni, kusini mwa mkoa wa Helmand , maafisa wa Taliban walionya kwamba vinyozi lazima wafuate sheria ya Kiislamu katika kunyoa nywele za kichwani na ndevu. Hakuna hata mtu mmoja aliye na uwezo wa kulalamika, ilisema notisi ilioonekana na BBC.

"Wapiganaji hao wanaendelea kuja na kutuagiza kutonyoa ndevu’’, alisema kinyozi mmoja mjini Kabul’.
Mmoja wao aliniambia kwamba wanaweza kutuma maafisa kuchunguza ili kutukamata. " Kinyozi mwengine , ambaye anasimamia mojawapo ya saluni kubwa , alisema kwamba alipokea simu kutoka mtu aliyesema ni afisa wa serikali.

Walimtaka kutofuata mitindo ya Marekani na kutowanyoa watu ndevu zao. Wakati wa uongozi wa kwanza wa Taliban kuanzia 1996 hadi 2001, Kundi hilo lilipiga marufuku mitindo tofauti ya nywele na kusisitiza kwamba wanaume wafuge ndevu. Lakini tangu wakati huo, unyoaji wa ndevu na nywele fupi miongoni mwa wanaume wa Afghan umekuwa maarufu.
Uislam taab kweli kweli.
 
Hao Taliban ni wahuni tu, hawana lolote kwanza wameirejeshea nchi mikosi tena. Nimesikia kwamba tayari wameshaanza kughubikwa na njaa ambayo tayari imeathiri takriban watu milioni tatu.

Kitakachofuata hapo ni vita vya wenyewe kwa wenyewe wananchi hawatavumilia huo ujinga wao, tusubiri ni swala la muda tu.
Huna uhakika unachosema bali umesikia.
Taarifa ya vyombo vya habari mbalimbali duniani.
 
Sharia za Kiislamu zimeficha uovu mwingi sana.
Mambo wanayo fanya makundi ya Kigaidi ya Kiislam yote yapo kwenye Sharia za Kiislamu. Ingawa mengi hayapo kwenye Qurani.
Sharia za Kiislamu sio za hiari bali ni lazima.
Hapa kwetu walianza chokochoko za Mahakama ya kadhi kwa kusingizia kuwa watajikita na baadhi tu ya mambo kama Mirathi, Ndoa na Mambo ya Dini kama Mavazi ya Staha.
Lakini hakuna mahali katika Uislamu panaposema fateni maagizo machache ya Sharia za Kiislamu.
Kuchagua mambo matatu tu ilikuwa gia tu ya kuanzia, Sharia inabidi zifuatwe zote.
Wangeanza na matatu, kesho wanaongeza manne, keshokutwa kumi, mwisho kama wakipata nguvu ya kutawala wanayaingiza yote kwa nguvu tena kwa hata wasio kuwa Waislamu.
Hii janja janja ndio inayotufanya sisi tusiokuwa Waislamu kukataa kwa nguvu zote mambo ya Mahakama ya Kadhi.
Mioyoni tunajua hii ni gia tu ya kuifanya Nchi kuwa.
Islamic State.
 
Wataleban wakiendelea na siasa za kijuha zenye misimamo mikali ya kidini utawala wao hautadumu utaondolewa kwa nguvu na wananchi wao wasiotaka hizo siasa za ajabu. Kwanza wameitia nuksi nchi yao imekumbwa na njaa na bado uchumi wa nchi yao haijulikani utatengemaa lini waache kusaidiwa na nchi zinazowaunga mkono, utawala wao umekuwa ni kituko duniani
 
Hao Taliban ni wahuni tu, hawana lolote kwanza wameirejeshea nchi mikosi tena. Nimesikia kwamba tayari wameshaanza kughubikwa na njaa ambayo tayari imeathiri takriban watu milioni tatu.

Kitakachofuata hapo ni vita vya wenyewe kwa wenyewe wananchi hawatavumilia huo ujinga wao, tusubiri ni swala la muda tu.

Taarifa ya vyombo vya habari mbalimbali duniani.

Taarifa kutoka vyanzo gani?
 
Usitusemee na wengine eti ndugu zetu,,,Kwa taarifa yako tu, hao wacongo na msumbiji kama si waisilamu hawatuhusu, watabakia kuwa ndugu zako wewe katika kristo. Kwa sisi waisilamu hatuna undugu na makafiri kaa utambuwe hilo.
Nani atake udugu na wewe sasa? Kwa kipi? Ebu kapake hina ndevu hizo.
 
Sababu ya kwamba wewe huitaki taarifa haimaanishi kuwa si kweli.

Tumeshawazoea

وَلَنْ تَرْضَىٰ عَنْكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۗ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُمْ بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ ۙ مَا لَكَ مِنَ اللَّهِ مِنْ وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ
Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu.
 
Usitusemee na wengine eti ndugu zetu,,,Kwa taarifa yako tu, hao wacongo na msumbiji kama si waisilamu hawatuhusu, watabakia kuwa ndugu zako wewe katika kristo. Kwa sisi waisilamu hatuna undugu na makafiri kaa utambuwe hilo.
Hivi wewe na hao wanaoipigania Dini ya Kiislamu ili itawale dunia, na kufuata Sharia zake.
Nani Kafiri.
Wenzenu wanajitolea kwa jasho na damu kuunda Islamic State pande zote za dunia.
Nao wanawaita ninyi mnao kaa tu na kukubali kuishi na wenye dini nyingine hasa Mayahudi na Wakristo kuwa ni Makafiri na mkiingia kwenye anga zao mnachinjwa vilevile.
Na kwabahati Mbaya kama wataiteka dunia na kuitawala watawajumuisha na nyinyi katika utawala wao na mtafurahia kujiunga nao.
Ila hilo hatutaruhusu litoke.

Bwana Yesu alisha yajua hayo na akatupa Upanga Mkali Sana.

Mathayo 10:34
Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.

Luka 22:35
Akawauliza, Je! Hapo nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? Wakasema, La!

Luka 22:36
Akawaambia, Lakini sasa mwenye mfuko na auchukue, na mkoba vivyo hivyo; naye asiye na upanga, na auze joho yake akanunue.

Luka 22:38
Wakasema, Bwana, tazama, hapa pana panga mbili. Akawaambia, Basi.
 
Usitusemee na wengine eti ndugu zetu,,,Kwa taarifa yako tu, hao wacongo na msumbiji kama si waisilamu hawatuhusu, watabakia kuwa ndugu zako wewe. Kwa sisi waisilamu hatuna undugu na makafiri kaa utambuwe hilo.
Kafir ni nini, tuanzie hapo kwanza kabla sijakutukania mama yako.
 
Tumeshawazoea

وَلَنْ تَرْضَىٰ عَنْكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۗ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُمْ بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ ۙ مَا لَكَ مِنَ اللَّهِ مِنْ وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ
Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu.
Lakum dinu kum, wal' ya din! usitulazimishe ugaidi wako hapa!
 
Back
Top Bottom