Capt Tamar
JF-Expert Member
- Dec 15, 2011
- 12,340
- 16,383
Nilikuwa naangalia al jazeera jana,watu wananinginia kwenye ile ngazi pembeni,kumbe kila mwarabu anatamani kuishi kwa makafiri aisee! Mungu amewabariki sana makafiri,na bado anazidi kuwabariki kwa kila kituwewe uko nyuma ya wakati.taarifa hizi zipo kabisa wewe unasema photosho.mimi nilivyoona ile video kwa nje sikujua ndani ya ndege kuna hali gani
Hao hawawezi fika USA, ila kuna wale tu ambao walikuwa wakiwasaidia kama kutasfiri/waandishi wa habari, na waliokuwa wakifanya kwenye mashirika yao, wengine walishapelekwa Marekani, na wengine bado ila wataenda.hao kwenye ndege hiyo ni lift tu wanabwagwa hapo qatar tu, kwani kuwashusha ingekuwa ngumu.Wazee wa fursa wakiona marekani ileeeee....
Hivi unadhani USA wataruhusu hao watu kuingia nchini kwao? Hao wataachwa hapo hapo Qatar wapige vibarua..
Hilo hilo ndo naulizia na mimi, pia hiyo ndege ya mizingo ina baba tani zaidi ya 150, watu 640 ni kidogo sana nikama tani 60 tuWanajeshi wa US ambao tuliwaona wapo kwenye ndege na ni wengi mbona siwaoni hapo??
Hiyo haikwenda kuchukua wanajeshi ilienda beba diplomat people ila walichokutana nacho sasaWanajeshi wa US ambao tuliwaona wapo kwenye ndege na ni wengi mbona siwaoni hapo??
Huwa Kuna safety factor mkuu. Sio kuwa uambiwacho na kichwa kuwa kipo sahihiHiyo ndege imekuwa ya mwendokasi sasa
Maana limebeba uzito x5 ya kawaida yake
Na rubani akakubali na ikapaa duu
Kuna movie zingine hazihitaji popcorns kabisa [emoji23][emoji23]
Mkuu kwaio ilienda tupu?Hiyo haikwenda kuchukua wanajeshi ilienda beba diplomat people ila walichokutana nacho sasa
we kipofu utaonajeSioni hata mmoja aliyevaa barakoa
utaonaje nawewe ni kipofuSioni hata mmoja aliyevaa barakoa
Unajua bhana sawa waafrika ni wapumbavu wa fikra hususan viongozi wetu .Baada ya kushuhudia Waafghanistan wakijaribu kudandia ndege ya Jeshi la Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khamid Karzai mjini Kabul jana, Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetoa picha inayoonesha watu 640 wakiwa ndani ya ndege yake ya kijeshi...
Waliachwa wanashangaaHilo hilo ndo naulizia na mimi, pia hiyo ndege ya mizingo ina baba tani zaidi ya 150, watu 640 ni kidogo sana nikama tani 60 tu
Kujaa kwa watu katika Uwanja huo wa Ndege kulitokana na taarifa za uzushi kusambaa awali Mjini Kabul kuwa Jeshi la Marekani linatoa usafiri wa bure kuwapeleka wananchi wa Afghanistan kwenda Marekani na Kanada,...
Asa mkuu hao waarabu wananafikiana wenyewe kwa wenyewe unadhani mwarabu ataweza kukimbia kwa mwarabu mwenzake?Aisee, kumbe wanazipenda nchi za kikafiri namna hii? Dini ya haki! π
Wapo mkuu,angalia vizuri hiyo picha.Sioni hata mmoja aliyevaa barakoa
Mbona haina viti?Hiyo haikwenda kuchukua wanajeshi ilienda beba diplomat people ila walichokutana nacho sasa
Hiyo ni ndege ya mizigo
Kwahiyo kaona asiwapeleke kwake awapeleke kwa mwingineπππBaada ya kushuhudia Waafghanistan wakijaribu kudandia ndege ya Jeshi la Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khamid Karzai mjini Kabul jana, Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetoa picha inayoonesha watu 640 wakiwa ndani ya ndege yake ya kijeshi...
View attachment 1895144
Wahuni tuu hao waliwaachia tuu wapande π π π πBaada ya kushuhudia Waafghanistan wakijaribu kudandia ndege ya Jeshi la Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khamid Karzai mjini Kabul jana, Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetoa picha inayoonesha watu 640 wakiwa ndani ya ndege yake ya kijeshi.
Idadi hiyo ya watu inatajwa kuwa zaidi ya mara tano ya uwezo wa ndege hiyo kubeba abiria na moja ya idadi kubwa zaidi kuwahi kubebwa katika ndege hiyo aina ya Boeing C-17 Globemaster III. Waliofanikiwa kuingia ndani ya ndege hiyo walitumia mlango ambao haukufungwa vizuri wakati ndege hiyo ikiwa katika uwanja wa ndege mjini Kabul.
Wizara ya Ulinzi ya Marekani imeripoti kuwa haikuwa na mpango wa kuwabeba watu hao, lakini ililazimika kutokana na vurugu zilizotokea katika uwanja wa ndege jana. Inaripotiwa kuwa watu wawili wamefariki baada ya kuanguka kutoka kwenye ndege hiyo.
Kujaa kwa watu katika Uwanja huo wa Ndege kulitokana na taarifa za uzushi kusambaa awali Mjini Kabul kuwa Jeshi la Marekani linatoa usafiri wa bure kuwapeleka wananchi wa Afghanistan kwenda Marekani na Kanada, ndipo mamia ya watu walipovamia uwanja huo wakijaribu kupata usafiri huo wa bure na kuyaokoa maisha yao kutoka kwa Wataliban.
Waliofanikiwa kupanda ndege hiyo - wakiwamo wanawake na watoto wachanga - wamefanikiwa kutua salama nchini Qatar.
Wapiganaji wa Taliban wamefanikiwa kuchukua udhibiti wa Mji Mkuu na mipaka ya nchi. Uwanja huo wa ndege ndio sehemu pekee iliyo chini ya udhibiti wa Jeshi la Marekani.
Chanzo: Guardian US
View attachment 1895144