Isanga family
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 22,981
- 47,826
Yanga wanajitambua sana na huyu Kitine ni kiboko sio saizi ya kina Karia..
Hivi wewe ukienda benki kujua Hali ya mkeka wako unaanza na maongezi na Afisa wa benki au anakupa mkeka wako, ukiona Una tofauti ndio , utaupitia mkeka wa benki nataarifa zako kuona tofauti zipo wapi , na ndio maana uwekaji wa taarifa za kimaandishi ni muhimu, na kupeana taarifa Kwa wakati. Wewe Leo unalipa deni langu , nakala hunitumi, Mahesabu yatakubaliana hapo ktk Hali kama hiyo.Nani kasema hayo? Huu ni upotoshaji ambao hautusaidii. Yanga hawajatoa risiti yoyote wao wamekabidhi barua tu. Kama tuna risiti tunaogopa nini kufanya reconciliation? Mashabiki wa Tanzania tumekubali kifanywa manyumbu. Makolo wamefanywa manyumbu, na sisi wanataka kutufanya manyumbu, hatutakubali.
View: https://www.instagram.com/p/DKwV0zRsI76/?igsh=MWtxbnE1cGMxem8yNQ==
Unapayuka sana,unaelewa '.......wameambatanusha INVOICE........" ,unajua invoice maanake nini?
Ushajiuliza ikiwa Yanga hajalipwa, vipi marefa, timu zilizo shiriki kwenye hiyo michuano au nao TFF wanawadai, jambo linalo hitaji watalamu lifanyike kiutaalam. Sasa Yanga yupo tayari mpaka kuwatumia mauditor wa TRA, Yanga wanataka transparency TFF wanataka busara.
Porojo na nyaraka ni vitu tofauti"Klabu ya Yanga wao wamefika hapa TFF wameleta barua na kuondoka na wamesema hawana chochote cha kuzungumza na sisi na hata Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao alipomuita CEO wa Yanga wazungumze alikataa, hizi ni taasisi kubwa na sio kila jambo tunapaswa kuandikiana barua kama tunatoa posa"- Cliford Ndimbo Afisa Habari wa TFF.
"Kama CEO wa Yanga SC hajui bingwa anapata nini kwanini wanasema wanadai kiasi hicho cha fedha wanachosema."
Maneno ya Cliford Ndimbo Afisa Habari wa TFF.
Hata unapotaka kuweka pesa unaandika mkeka wa pesa uliyo nayo siyo porojo ama diamondo saundoHivi wewe ukienda benki kujua Hali ya mkeka wako unaanza na maongezi na Afisa wa benki au anakupa mkeka wako, ukiona Una tofauti ndio , utaupitia mkeka wa benki nataarifa zako kuona tofauti zipo wapi , na ndio maana uwekaji wa taarifa za kimaandishi ni muhimu, na kupeana taarifa Kwa wakati. Wewe Leo unalipa deni langu , nakala hunitumi, Mahesabu yatakubaliana hapo ktk Hali kama hiyo.
Umeeleza vyema hata Mimi ambaye Sina uelewa juu ya taaluma ya fedha nimeelewa vizuriMaswala ya fedha yana UTAALAMU wake, kwa vyovyote vile.
Wachambuzi watafata ya mpira ya HATUCHEZI NA TUNACHEZA!!
East Africa Radio mbona mnatulisha MATANGO PORI??? Huyo ni muandishi wenu katika kipindi cha "kipengaextra"? Mmemuuliza alichokisema?? Anajua tofauti ya BARUA NA INVOICES? Nyie mkitaka kudai mtu au kudaiwa mnaletewa barua?? Au invoice na delivery note?? Na wewe ukilipa au kulipwa si unapewa au kutoa Payment Voucher na Receipt??
WACHAMBUZI WANAOITA "BARUA" na TFF wapo sawa kweli?? Young Africans Sports Club wamefanya kitu kizuri. Na KAMA TFF NDO WANADAI KWELI, INAWASAIDIA WAO KWA ASILIMIA 100.
YANGA wamefanya professionally! Wana akili nyingi saaaaaana ase!!! Sijui nani kawashauri. Hiyo ndo CPA (UHASIBU/ACCOUNTANCY! LAZIMA UTUMIE UTAALAMU WA UHASIBU...
HAO WAANDISHI WANAYEONGEA WATAKUWA AWAELEWI,. AU WASILOLIJUA NI HIVI. YANGA WAMEPELEKA INVOICES. SIYO BARUA!!!
Mfano:
MIMI NINA KAMPUNI NAKUDAI, WEWE UNA KAMPUNI UNASEMA KUNA MADENI UNANIDAI....
*NAKULETEA *INVOICE NA DELIVERY NOTE KUKUDAI PESA ZOOOOTE.
*WEWE UNAPASHWA KUNIPA *PAYMENT VOUCHER NA RECEIPT.
TUMEMALIZA.
Ukikataa, au atujaelewana ndo tunawaita TRA (Tanzania Revenue Authority) NA WATAALAMU WA MADENI, NA MIMI NA WEWE. Tuanze kuoneshana kimoja kwa kimoja. Ndo YANGA wamefanya. Na tutaonyeshana nini, documents. Invoice yangu namba flani, naoneshay; haya wewe onesha ulinilipaje?? Kama ulinilipa au kunikata onyesha risiti ya serikali/EFD na Payment Voucher namba ngapi... simple and clear!
Umeelewa Bwana Mkubwa??
Hizo sheria zimetungwa baada ya tarehe 8 March?Kama kawaida
Jumapili msije tu wala sisi hatuna noma na nyie kutokuja.
Sisi tunataka sheria ifuatwe tu.