Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
1.Africa itapata wapi pesa za kulipa madeni inayodaiwa na Marekani?
2.Kwa nini Africa iache kupokea misaada kutoka Marekani?
3. China tayari inauza hadi toothpicks na Urembo Africa, Russia tayari inauza ngano,mbolea na AK47 kwa wingi Africa, Brazil inauza wigi za wanawake, Africa Kusini inatuuzia juice, India inatuuzia hadi dawa za maumivu na viongozi wengi wa Africa wanatibiwa huko. Unataka biashara gani zaidi kati Africa na BRICS?!
4. Nchi nyingi Africa zinauza mazao ya kilimo na rasilimali ghafi, unataka wauziane mahindi na madini kati yao?!
5. Unaposema teknolojia ya Marekani isitumike Africa unamaanisha pamoja na Internet, GPS, Ndege, Microsoft, Twitter, Facebook, WhatsApp, VISA?
6. Mitumba inaweza kuzuiwa ukiwa na "wajasiriamali" wengi kama Vunjabei na wengine wa Kariakoo wanaoweza kujaza soko la Africa na nguo za bei rahisi za Kichina
7. Miradi mingi ya Africa sasa hivi wanachukua mikopo kutoka China, huku ndiko kujitegemea unavyomaanisha??

Afrika walipe tu madeni wanayodaiwa sasa na Marekani kisha nchi zote ziache kupokea fedha na misaada toka Marekani. Afrika ianze kufanya biashara kati ya nchi na nchi ndani ya Afrika na nchi nyingine zile za BRICS na nyinginezo.
Afrika ili iendelee ihakikishe teknolojia yoyote toka Marekani haitumiwi Afrika na ile Mikataba ya kiulinzi na Marekani ivunjiliwe mbali na mikataba yote ya kibiashara isitishwe mara moja. Afrika izuie mitumba na bidhaa zinazoweza kupatikana kwingineko mbali na Marekani kuingia Afrika.
Afrika isimame imara dhidi ya Marekani ili ijitegemee!!