Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa taarifa yako tuzo zimeandaliwa na ubalozi wa Tanzania huko afrika kusini, sasa hivi balozi nyingine nazo zinaandaa matuzo mbalimbali ili aonekane anakubalika, kama yule mtangulizi wake alivokuwa anaandaa udokita na uporofesa
Una laana ya Lumumba wewe. Huyo Mungu wa wapi unayemsema wewe? Au Mungu wa CCM aliyewafunza kukata watu mapanga?Magufuli ni chaguo la Mungu wasiopenda wahame nchi maana bado ana miaka 7 ya kuingoza nchi hii
Woote hamna kitu!! Hapa penyewe kupotezwa ni haki ya wananchi.Hapo kwa Nkrunzinza ndiyo wameharibu kabisa
Lakini sihangai sana maana tuzo zenyewe zimetolewa na mwafrika.Woote hamna kitu!! Hapa penyewe kupotezwa ni haki ya wananchi.
Wakibiti na Mkuranga mbona huwataji?, dhambi hii ya ubaguzi haitaicha chadema salama hata kidogo
Tu-mbwa twa CCM tumekuja tena! Tuliwahigi kusema makofuri kashinda tuzo gani vile mwaka ule?
Nchi ya babako hii hadi watu wahame,hiyo miaka 7 atakuongoza wewe na mkeoMagufuli ni chaguo la Mungu wasiopenda wahame nchi maana bado ana miaka 7 ya kuingoza nchi hii
![]()
Johannesburg, Afrika Kusini. Rais John Magufuli ametunukiwa tuzo ya amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) kwa kuendeleza shughuli ya kulinda amani na kupigania usawa wa kijamii.
Kamati ya tuzo za Mandela kwa mwaka 2017 ilipokea maombi ya wawania tuzo 4,956. Wengine waliotunukiwa ni Rais Uhuru Kenyatta aliyeshinda tuzo ya Mandela ya Demokrasia kutokana na kuendeleza demokrasia nchini Kenya.
Pia, Mahakama ya Juu nchini Kenya na Jeshi la Zimbabwe zimetunukiwa tuzo ya ujasiri (Mandela Boldness) kwa kufanya uamuzi kwa kijasiri kwa masilahi ya mataifa yao.
Rais wa Taasisi ya Mandela, Dk Paul Kananura amesema Rais Kenyatta ametunukiwa kwa kudhihirisha demokrasia kwa kukubali uamuzi wa Mahakama ya Juu hivyo kuheshimu kanuni za utengano wa mamlaka. Mahakama ya Juu ya Kenya ilibatilisha matokeo ya urais katika uchaguzi wa Agosti 8,2017 yaliyompa ushindi Kenyatta na kuamuru uchaguzi kurudiwa ambao alishiriki na kuibuka mshindi.
"Hii inaonyesha kuwa Rais Kenyatta amechangia katika uimarishaji wa demokrasia Kenya,” amesema Dk Kananura. Rais wa Chad, Idriss Itno amepata tuzo ya Mandela ya Ulinzi (Mandela Security) kutokana na sera ya kupambana na ugaidi katika maeneo ya Sahel na Ziwa Chad. Mwingine ni Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza aliyetuzwa tuzo ya ujasiri (Mandela Courage).