Ni ukweli usioweza kufichika kuwa ujenzi wa barabara zetu zote huwa ni wa kulipua. Nashindwa kujua kama barabara tunazojengewa au kujenga wenyewe, tunazingatia zaidi kupitika tu majira ya mvua au nafuu ya gharama za ujenzi? au ukosefu wa maono ya kuwa na barabara bora zinazovutia na kupitika majira yote ya mwaka.
Nimetembelea baadhi ya nchi za Afrika Mashariki na kati na kugundua kuwa barabara zetu na zile za Zambia Malawi, DRC na Burundi viwango vyake vinafanana kwa maana ya kuwa duni.
Barabara za Kenya zina nafuu kidogo ingawa ni nyembamba. Barabara za Rwanda ziko vizuri kwa viwango vyote vya kitaaluma, na kwa kiwango kikubwa ingawa ni finyu pia lakini, zinapata matunzo na maboresho..... Najiuliza, Tanzania tunakwama wapi?
Sitegemei kuiona Tanzania ikiorodheshwa kwenye ligi inayo angazia barabara bora Afrika Mashariki, achilia mbali barabara bora ndani ya bara Afrika.