Afrika ndiyo kinara wa kufanya kazi ngumu lakini kisukari ni tishio je kazi ngumu sio mbadala wa mazoezi?

Kwangu kazi ngumu naweza kusema ni mbadala wa mazoezi. Changamoto kubwa huku kwetu ulaji wetu ni mbovu hauzingatii afya.

Mazoezi/kazi ngumu iendane na msosi mzuri(mahitaji ya mwili)
 
Population kubwa ya Afrika iko vijijini siyo "miji iliyochangamka." na hata hiyo miji unayosema utakuta watua wanshindia chips, mayai, soda na kijiweni; utakosa vipi kisukari kama maisha yako ndiyo hayo?
 
Mkuu, naomba uhusiano wa kisukari na mazoezi. Kuna kitu nataka kujifunza.
assume umekula ubwabwa wako ama ugali wa kutosha, unapoenda kufanya mazoezi ile energy ya carbohydrate itatumika na Mwili hautatengeneza mafuta ya ziada.

ILa umepiga ubwabwa wako halafu unalala ama umetulia ile energy haitumiki na ibabadilishwa kuwa fat, hii fat ina ongeza resistance ya insulin kwenye Mwili, kunapokua na resistance ya insulin cell za Mwili hazi absorb sukari na kupelekea sukari kusafiri kwenye mishipa ya damu hivyo kupata kisukari.

Sio Tu wanga, mafuta, vyakula vya viwandani na junks food nyingi zipo kundi hili.
 
Shukrani kwa maelezo yako mujarabu. Kwenye hiyo paragraph ya mwisho, umenipa jibu la swali ambalo nilikuwa nimejiandaa kuliuliza. Thanks Chief 👊
 
Kweli kabisa mkuu hii nchi kuna mda nikiiwaza naona kabisa ni kama sisi kwa dunia ni zile grade za mwisho mwisho [emoji1787][emoji1787]
 
Kweli kabisa mkuu hii nchi kuna mda nikiiwaza naona kabisa ni kama sisi kwa dunia ni zile grade za mwisho mwisho [emoji1787][emoji1787]
Ndo ivo, yaani huku ukiumwa kwa wengine ni kicheko maana watakuvuna vilivyo.

Ndo serikali ihamasishe tule matunda, dadeki ndizi utanunua buku, ila mind you mkulima wa hiyo ndizi anaweza pata sh 50, mnyororo wa ulaji hapo kati ndo balaa.
 
Kwanza ni kujua kisukari kinaletwa na nini nipo jibu linapatikana
 
Mwezi wa kwanza tumemzika dogo wa 1998 , amekufa kwa kisukari kabla ya hapo kimemsumbua miaka 2 nyuma.
 
Mkuuu, umemaliza. Ngozi nyeusi na kiasi ni mbingu na ardhi
 
Kwanza ni kujua kisukari kinaletwa na nini nipo jibu linapatikana
Nimeona wachangiaj wengi wamejitaid kuelezea kuhusu kisukari ila mim nafikir kisukari kinasababishwa na hitilafu kwenye kongosho ,pia na ulaj mbovu unakuta mtu anakula vyakula ambavyo sio rafiki sana Kwa mfano anakula mara Kwa mara nyama nyekundu,soda Kwa wingi,chips ,bia na vinywaj vyenye sukar sana,kumbuka mtu huyu anapofanya hivyo hata kama atafanya mazoez inakuwa Kaz Bure,pia nimeona Kuna tiba yenye seli(stem cell) imewasaidia watu wengi wenye changamoto ya kisukari ikiwemo kubust immunity na kutibu hitilafu ya kongosho,na nimeona wengi wameondokana na maradhi haya hatari maana kisukari ni ndg yake na presha,na utakuta mtu mwenye presha (high blood pressure)yupo kwenye risk ya kupata kisukari.Kwa ufupi haya maradhi ni hatari na yanaua haraka sana,yanasababisha upofu ,uanith ,uharibifu wa Figo ,in na viungo vingine vya mwili,kinachotakiwa ni kuchukua hatua haraka sana
 
1. Kazi ngumu si mbadala wa mazoezi. Mazoezi kama kukimbia yanawezesha ufumiaji na mzunguko wa damu, pia kuna mazoezi ya kunyoosha viungo.
2. Mchango wa sumu za mashambani na anti-biotics ni mkubwa sana kuelekea kudorora kwa afya.
 
Miaka ya 90, kisukari ulijulikana ni ugonjwa special wa matajiri. Wastaafu serikalini,wafanyabiashara matajiri ( wanaokula kiulaini) nk nk.

Uswahilini, na maskini, wenye kupata chakula Kwa taabu, wakulima vijijini,kunywa soda ilikuwa Hadi sikukuu, hawakuwa na tatizo la sukari.

Mimi,nahusisha kisukari mojakwa Moja na ulaji wa vyakula vya mafuta na kula kupitiliza, unene na kutofanya kazi ngumu za Kutoka JASHO.

Ni hayo tu.
 
Sema vyakula vya wanga mkuu. Sisi tunatumia sana nafaka zenye carbohydrates sana kama mahindi na mchele na ngano. Hili lina mchango mkubwa sana kwenye gonjwa la sukari.
Kabisa mkuu upo sahihi.
 
Mkuu, naomba uhusiano wa kisukari na mazoezi. Kuna kitu nataka kujifunza.
Ukifanya mazoezini au kazi ngumu unaunguza au kutumia sukari nyingi kama energy.
Ukiwa unakula tu na haufanyi mazoezini hii sukari inalundikana mwilini na ndo hiyo huleta ugonjwa
Bush dokta kwa msaada ya gugo
 
Mnazunguka zunguka, mara carbihydrate mala life style ..

Ishu ni moja tuuu.

Regulation of sugar kwenye blood, hii ni kazi ya Insulin.
ikiwa na afya hii kula ulavyo mwil una in-built capability ya ku regulate sukari kwa Insulin.

Iki feli hii hata uwe unakunywa maji tu,kisukari kitakuondoa
 
Kisukari na kudindisha vinahusiana vipi Mzee? Au huo upofu?
Sukari ina uhusiano mkubwa sana na upofu pamoja na urijali,
Huwa inaua mishipa midogo ya damu na moja ya mishipa hiyo ni ilie inayosimamisha uume pamoja na macho
 
Mfumo wa maisha maana afrika watu wanapenda sana vitu vitam
Sio kweli hakuja watu wanakula vitu vyenye sukari kama wazungu, kinachowasaidia wazungu ni huduma za afya zipo bora pia tamaduni ya upimaji wa afya mara kwa mara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…