PostGE2025 Afrika (Tanzania) haitopona mpaka Viongozi wake wabadilike

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Kwanini viongozi wengi wa Kiafrika ikiwemo nchi yetu ya Tanzania hukengeuka pale wanapopata nafasi ya kuongoza nchi zao?

Wasalaam Wakuu!

Ni swali linaloumiza kichwa na kutufanya tutafakari kwa kina: Kwa nini viongozi wengi Barani Afrika ikiwemo nchi yetu Tanzania wakishapata madaraka hugeuka na kuwa wabadhirifu wa mali ya umma?

Tumeona mara nyingi mtu akiingia kwenye uongozi akiwa mnyenyekevu, akiahidi mabadiliko, akionyesha uzalendo lakini muda mfupi baadaye anageuka na kuwa kinyume kabisa cha alichokiahidi.

Waafrika /Watanzania wengi hupambana kwa gharama kubwa kutafuta madaraka.
Hutumia nguvu, pesa, propaganda na wakati mwingine hata damu kumwagika ili tu kukalia kiti cha uongozi.
Lakini cha kushangaza, mara tu wanapofanikiwa, hutawaliwa na tamaa wanageuka mafisadi, wabinafsi, na wezi wa raslimali za umma.

Wanaingia kwenye mikataba ya kifisadi yenye maslahi binafsi,
huiba mali za nchi na kuzihamishia Ulaya na mataifa ya mbali,
wakati wananchi wao wanaendelea kuteseka kwa umaskini, ukosefu wa dawa hospitalini, elimu duni, njaa, na kipato duni.

Inasikitisha kuona mali za Afrika zinazidi kuinufaisha Ulaya kuliko Waafrika wenyewe.

Badala ya kujenga viwanda, kuboresha miundombinu, kutengeneza ajira kwa vijana na kukuza uchumi,
viongozi wengi wa Afrika huagiza bidhaa kutoka nje hata zile ambazo tunaweza kuzalisha sisi wenyewe.
Matibabu yao ni nje ya nchi, mapumziko yao Ulaya, watoto wao wanasoma shule za kifahari za ng’ambo,
lakini wananchi wanaowatumikia wanasoma kwenye madarasa yenye madirisha yaliyovunjika na kulala bila mlo kamili.

Je, tatizo ni mfumo? Ni fikra? Ni kutokuwepo kwa uwajibikaji?

Kiongozi anapokuwa na mabilioni alioficha nje ya nchi yake wakati taifa lake linaomba misaada,
linaonyesha wazi kuwa tatizo si ukosefu wa rasilimali bali ni ufisadi, tamaa na upotevu wa maadili ya uongozi.

Mara nyingi mali hizo wanazoficha nje ya nchi huishia kupotea wanapokufa,
zinakuwa faida kwa mataifa ya kigeni,
wakati wao wanazikwa katika nchi zile zile walizozifisadi, walizozinyonya, walizozipora bila huruma.

Afrika haitapona mpaka viongozi wabadilike

Tunapaswa kuweka mifumo imara ya uwajibikaji, kusimamia sheria bila upendeleo,
kuthamini utaifa kuliko matumbo binafsi.
Kiongozi aliyezalishwa Afrika anapaswa kuthamini ardhi yake kama Ulaya wanavyothamini kwao.
Kwa nini wao wafiche mali kwetu, na sisi twaficha mali kwao?

Afrika inaweza kuendelea ikiwa tu viongozi wake wataamua kuondokana na ufisadi, tamaa, ubinafsi na dhuluma.
Tuchague kujenga badala ya kubomoa.
Tuchague uzalendo badala ya ulafi.
Tuchague ustawi wa wananchi badala ya faida za mtu mmoja
 
Huu ni ukweli ambao wengi hawataki kuusikia

Moja ya changamoto ambazo zinafanya africa haipigi hatua ni viongoz wake

Ni kikwazo
 
Back
Top Bottom