Very true...Ila pia bado majority population ya western countries ni religious people..so ishu sio kuondoa dini kabisa coz utaonekana kiongozi shetani(Kama Obama) issue ni kuencourage critical thinking ndo maana wazungu despite dini kuwepo bado wanaendelea coz wanatanguliza akili kwanza.
Ni kweli kwamba majority ya watu wa western countries ni religious. Lakini hata hao inategemea na wapi, na religion wanaichukulia vipi.
Kwa mfano, Ulaya watu wengi wanajitambulisha kwamba hawaamini Mungu, atheists. Nchi kama Finland na Spain around 20% ya nchi hawaamini Mungu. Netherlands ndiyo around 45%, yani karibu nusu. Nchi kama Estonia watu hao wako around 60%, Czech Republic wako around 78%. Na hawa watu hawapendi uongo wa dini na Mungu, lakini wamejiwekea mifumo inayojali utu, inajali uhai, ina demokrasia, inajali watoto, inajali wazee.
Sisi tuna unafiki wa kuendekeza Mungu na dini halafu tunaminyana, kuuzana na kuuana kila siku.
Hata hao wenye kuamini Mungu na dini, kwa kiasi kikubwa wanaamini kiutamaduni tu, wanapenda sense of community ya kanisani, wanapenda kwaya, wanapenda architecture za makanisa zile stained glasses, na hao ni wazee ambao wanaenda kuisha sasa, vijana hawana affiliation na dini sana.
Wale wenzetu wamebaki na dini kama hobby, sisi tunatumia dini kama uchawi.
Ndiyo maana Africa makanisa ya uponyaji na kusaidia watu wafanikiwe kiuchumi yanashamiri.
Watu wengi wanafuata dini kama mbadala wa waganga wa kienyeji, dini inatumiwa kama uchawi tu, iwaponye, iwaletee mafanikio, wenye kufuata dini kwa misingi ya dini hasa ni wachache sana.
Yani ni hivi, kwa wenzetu in the west umuhimu wa dini umepunguzwa sana dunia inayoendelea kwa sababu ya sayansi.Mtu akiumwa kuna huduma nzuri za afya, si kwetu mtu akiumwa sehemu nyingi hakuna tumaini, inabidi aombe Mungu tu, atake asitake.
Nchi zina ajira kwa kila mtu, mpaka mtu mwenye mtindio wa ubongo yule anapangiwa kazi kwa mujibu wa uwezo wake. Mimi nimekuja New York mara ya kwanza nilikuwa napanda basi la asubuhi kabisa kwenda kazini, kukaw na jamaa mmoja ana matatizo kama ya Down Syndrome or something like that, hawezi kusema vizuri, hata kutembea kwake kwa tabu. Lakini jamaa alikuwa anapanda basi hilo hilo kila siku, halafu kwenye basi ana kelele kuongea na watu, halafu wazungu wanampenda kichizi wanapiga stories naye (alikuwa black). Jamaa ana matatizo ya mfumo wa ubongo lakini alikuwa na kazi yake supermarket anapanga vitu, na jamii inamthamini, na yeye anachangia uchumi wao kwa kiasi chake, analipwa mshahara wake.
Nikasema huyu ashukuru sana kazaliwa Marekani, angekuwa Tanzania watu wangemfungia ndani asionekane, ingekuwa aibu kwa familia huyu kuonekana, licha ya kupanda basi na kufanya kazi.
Unaona watu wanavyothamini utu wa mtu hata mwenye kilema hapo? Jamii iko so inclusive.
Huko kwetu watu wazima wenye afya zao na akili zao hatutumii hiyo human resource, unajua vijana wanaokaa bila kazi tunapoteza nguvukazi kiasi gani kwa mwaka hapo?
Hawa watu walishagundua kwamba dini ipo kama utamaduni, sasa tutajipangia sheria zaenye maadili ya utu, ndiyo maana unaona kuna sheria kali dhidi ya ubaguzi wa watu walemavu au kubagua watu kwa race, au kubagua wanawake na wazee. Dini ipo, lakini sheria ndiyo kali zaidi.
Sisi hatufuati dini wala sheria, tunafuata unafiki na ubinafsi tu.
Sasa kama una taifa lenye nguvukazi kubwa sana, unaipoteza kwa umachinga na ubodaboda tu, unategemea utaendelea vipi kiuchumi?
Angalia nchi masikini zinavyoamini dini.
Ni vigumu sana kukuta nchi masikini ambayo haina historia ya Ukomunisti kuwa na atheists zaidi ya 20%
The least religious countries in the world showcase a diverse range of cultural, historical, and societal factors that have led to lower rates of religious affiliation. These countries have witnessed a gradual shift towards secularism, as individuals increasingly identify as non-religious or...
wisevoter.com