Afrika tunashindwa na nchi za Asia tulizopata uhuru muda sawa. Shida ni nini?

Afrika tunashindwa na nchi za Asia tulizopata uhuru muda sawa. Shida ni nini?

Nani atashika hio laws Sasa wakat hao watunza laws ndio corrupt wakubwa.
Unakamatwa na rushwa Takukuru unawapa rushwa mambo yanaisha.
Jela utakaa kama huna pesa
Kunakuwa na chombo cha kusimamia organs kama Takukuru.

Kiwe tied na wananchi na wawe na full control ya kuwawajibisha viongozi hao wa Takukuru endapo hawatatenda haki.
 
Sio Mawala advocates hao kweli? 😂
Ukiiba bilioni 10 unatoa milion 500 police,DPP,Hakimu wanagawana.
Kisha unachagua hukumu kuadaa umma.
Faini milioni 90 au jela miaka 3.
Miaka ya 80 palikuwa na wahasibu ndugu waliiba Hela makusudi wakazificha hawakukimbia makusudi ili wakamatwe wakaenda jela hukumu ikatoka wakaamua kuhukumiwa miaka 5 jela ili wakitoka wakafanye biashara na ndivyo walivyofanya wakawa wafanyabishara wakubwa tu
 
Sawa..Ila sisi ni watu wa 21st century tunaelimu hatuwezi tesana hivyo....okay corruption solution yake ni good laws na prison...coz wazungu wanafanya hivi na wanaendelea
Sio kwa bongo hii. Huku suluhu ni kupelekana ahera tu.

Mob Justice ni mbaya ila imesaidia sana kuishape jamii hata maaskari wanajua kuwa kuna wezi ambao wao jela kwao kama nyumbani hadi wamezoeleka.

Inapotokea fursa ya wananchi kuwafyeka huwa inawapa hata wao ahueni. Wanaacha mmalize kazi wao wanafuata mzoga tu.
 
Wizi ni ngazi ya familia hadi juu Kila mmoja kwa level yake.Mwingine atauza nchi,baba anaiba ofisin analeta home,mama nae anampiga baba apate za vicoba,dada wa kazi nae anapiga za matumizi huku anawashindisha watoto wa boss viporo ili atume kijijini kwa mzazi wake amlimie mazao, mzazi kijijini nae anakula bata kilabuni ye ndo boss akitamba kwamba ye ndo anajua kuzaa binti anafanya kazi mjini.

Tufanye maombi tu kuondoa hii roho ya upigaji
Maombi yanataka imani ili yafanye kazi sasa mtu anaiba ili akamuhonge malaya au kufeera mashoga. Huyo maombi yatasaidia nini kwake?🤣
 
Ngoja waje wabongo kutetea Marekani hapa utafikiri ni baba yao mzazi. Mtu anakaza misuli mpaka ya tako kuisifia marekani na kuudharau uafrika wake.
Kwanza kabisa mnatakiwa kuacha kuamini miungu ya watu.

Huwezi kuendelea kama unapangiwa dini na Roma, Uyahudi au unasoma dini kwa Kiarabu na kuhiji Mecca na kuelekea Al-Qabr unaposali. Mpaka hapo tu ushahsindwa kwa sababu saikolojia yako ishashikwa umejiweka chini ya Mzungu, Myahudi au Muarabu.

Pili, tunatakiwa kutaka kweli kuendelea kama jamii. Waafrika wengi tunaridhika kirahisi, tunasema hewala hewla, tunaishi kwa kudura za Mungu (ambaye tumepachikiwa tu). Hatuna ari ya kweli ya kutaka maendeleo, tumekubali umasikini wetu na hivyo hatuwezi kuupita.

Inatakiwa tuukatae umasikini, tukubali kwenda kwa mazoea na utamaduni tu, tukubali kukataa tamaduni mbovu, mifumo mibovu na viongozi wabovu, au angalau tujue jinsi ya ku phase out vizuri vitu vibovu. Sasa hivi tunaheshimu sana tamaduni hata kama mbovu, tunaheshimu sana wakubwa na historia.

Umeuliza haya matatizo ya historia tunayapita vipi?

Huwezi kupita tatizo la historia mbaya kama bado unaiheshimu hiyo historia mbaya.

Mfano.

Afrika mpaka leo inatumia US dola kufanya intra-African trade. Biashara kati ya nchi za Africa inafanyikankwa US dollars. Mmarekani anapata nguvu ya ku control hii biashara kupitia US Federal Reserve (tawi la Benki Kuu ya US la New York). Hiki kitu kinaipa nguvi US dollar bila sababu. Kwa nini Waafrika wasifanye biashara zao kwa kutumia hela zao na kuiondoa US katika biashara za Africa? Hakuna sababu nzuri.

Rais William Ruto wa Kenya kaanza kulipigia mbiu hili. Settlement system tayari ipo Addis Ababa Ethiopia.

Lakini sioni Waafrika wakilichangamkia jambo hili. Wanalalamika tu hawana dola. Kwani kufanya biashara kati ya Waafrika ni lazima kuwa na US dollar?

Unaona ujinga wa akili tegemezi zinazoangalia historia tu bila kutaka kui challenge hapo?
 
Hakuna watu corrupt kama wachina popote pale ie kwao au nje ya kwao. Ila ni wachapa kazi.
Singapore, Thailand, Indonesia na Malaysia ni nchi ambazo zipo maeneo strategic hasa the strait of Malacca.

Southern China Sea kupitia strait of Malacca, inapitisha 5.7 Trillion worth of trading goods na hizo nchi zinachukua tax kutoka nchi nyingi, ikiwemo USA. hiyo income ni sawa na kuwa na mafuta.

Mkuu hata ukiwa corrupt vipi, thats a lot of money for small countries kama hizo, lazima kutakuwa na maendeleo. Waafrika hatuna biashara za kimataifa, labda Suez canal ambayo nayo inaipa sana hela Egyp.

Mifano mingine ni Panama canal na Strait of Hormuz kwa Panama na Iran.

Kuna nchi nyingine zimebarikiwa tu, zipo kwenye strategic areas.
Bongo hakuna biashara ya kimataifa na ile ya Tanzanite na Gold ni nini? 😂 Sema tu watawala ni wabinafsi na hawajali maslahi ya taifa as a whole bali wao watapewa nini na hao wawekezaji wanaokuja kunyonya resources.

Mtu anapewa billion 50 ya hongo anawamegea wenzake 10B kisha anasainisha mkataba wa miaka 90 wa vitalu vya madini. Watu wanajichotea mara elfu ya hio billion 50 wakimaliza hio miaka ni wameacha mahandaki tu.

Kiongozi hapo akishapewa hizo hela atakula yeye na familia yake tu. Watajenga majumba ya kifahari na magari. Raia wa kawaida mtapigwa mabomu mpishe site alipopewa muwekezaji. Huu ndio mfumo wa bongo.

Kwa ubinafsi huu bila kupigana nakoz na watawala hatutoboi. Tutabaki kulalama tu miaka nenda rudi wajukuu wetu ndio watakaoteseka..Wakati wangeweza kuja kuogelea kwenye utajiri wa rasilimali kama wafanyavyo warabu wa Dubai tunaotamania maisha yao. We unadhani wangekubali kuchimbiwa mafuta kwa kupewa 3% ya faida kila mwaka wangeendelea wale?
 
Hii akili ndio wanayoitumia vijana wakikabidhiwa ofisi za umma kujinufaisha binafsi ndio hugeuka mafisadi wakiwa wazee.
Sijasema MTU awe mwizi. Ila kila MTU apambane Kwa ajiri ya familia yake.
 
Jamani tuongee serious, nchi Kama India, Singapore, Malaysia, Indonesia zimepata uhuru almost the same time na nchi za kiafrika. Cha ajabu wenzetu wameendelea Sana halafu sisi bado tuna umaskini wa kutupa.

Afrika jamani shida ni nini?
Ninaamini kuwa tungetawaliwa tungeuchangsmkia uhuru wetu, ukimpa mtu nyumba bure usijeshangaa ukaikuta imeota mti sebuleni, hana uchungu nayo.
 
Jamani tuongee serious, nchi Kama India, Singapore, Malaysia, Indonesia zimepata uhuru almost the same time na nchi za kiafrika. Cha ajabu wenzetu wameendelea Sana halafu sisi bado tuna umaskini wa kutupa.

Afrika jamani shida ni nini?
Muafrika anataka mambo matatu
1-Pombe
2-Mwanamke
3-Mziki
Akishalewa anataka mwanamke plus mziki.
Muafrika kazoweya Kutaaliwa na sio kutawala .
Mfano aingie Mzungu ofisi yyote atafanyiwa mambo yake haraka haraka na rushwa hatoi ,lkn muafrika mwenzako pesa unatoa na mambo yako hayendi tofouti sana na Waarabu Mzungu anaoekana mtu wa kawaida sana tu.

Waafrika bado HAWAJITAMBUA hawajui wanataka kitu gani ktk nchi zao.
 
Okay okay...so ur saying India haijaendelea
Ndio hapo inabidi tuweke definition ya maendeleo ? Maendeleo ni nini ? Unaweza ukasema nchi yako imeendelea kama majority ni masikini wa kutupwa ? Katika nchi zenye gap la classes India ni mojawapo
 
Jamani tuongee serious, nchi Kama India, Singapore, Malaysia, Indonesia zimepata uhuru almost the same time na nchi za kiafrika. Cha ajabu wenzetu wameendelea Sana halafu sisi bado tuna umaskini wa kutupa.

Afrika jamani shida ni nini?
Shida ni Upstairs Zetu
 
Hapana ,wananchi wakiamua kuiondoa serikali wenyewe pasipo kumwaga damu ,ni kama zile harakati za kudai uhuru alizozifanya Nyerere na watu wake ,kwasasa sisi tuna mkoloni mweusi tudai uhuru wa pili kumuondoa "MKOLONI MWEUSI".
🤣Okay okay...so njia ni uchaguzi si ndio...ukisema watu waandamane ni mwendo wa machozi tu
 
Kila taifa liishi kwa amani kivyake acha kukumbatia ukoloni jinga kabisa kuendelea kuua na kumwaga damu za Wazanzibar kisa muungano ni zaidi ya ukoloni wa mzungu

Muungano haulindwi kwa bunduki huo ni ukoloni mna akili za kipuuzi sana nyie majitu roho za kinyama zimewajaa roho za Wazanzibar zitaendelea kuwalilia maisha yote waacheni wawe huru na nchi yao kina wauma nini wao wakiwa huru kivyao ?
Kwani wamepata uhuru hatujawapa?
 
Back
Top Bottom