TANZIA Aga Khan Afariki dunia akiwa na Miaka 88

TANZIA Aga Khan Afariki dunia akiwa na Miaka 88

Hizi taarifa huwa available unapozihitaji.

Mimi ni mpenzi wa mbio za farasi na kuna wakati niliishi UK (masomoni) wana uwanja wa mbio za farasi uitwao Ascot. Pale ni kiunga cha watu wote matajiri khasa koo za kifalme na matajiri wengine wengi tu.

Nilikuwa pale nafanya tafiti za koo za kifalme ndo nikawa na uwezo wa kuwachambua hawa watu, "very simple process" wapata habari zote.
Hongera sana Farasi ni moja kati ya wanyama napenda sana shida ni utunzaji wake ni wa gharama sana. ikikupendeza utumegee hizo tafiti za koo hizo za kifalme.
 
Mumesahau Serena hotels, Jubilee Insurance, Aga Khan universities Karachi, Nairobi , Dar na Arusha (U/C), Nationmedia, Farmers’ choice, Allpack industries ltd, Premier Foods Industries, pia IPS building alijenga yeye kabla Nyerere hajamnyang’anya!
 
Ukoo wake wa asili ni Uturuki, lakini walisambaa sana dunia nzima kuanzia Pakistani hadi ulaya huko Italy na Switzerland na hata Marekani na kanada.
Asili ya Bagamoyo na Pakistan/ Afghsnistan! Walihama huko kwavile Sunni walikuwa wanawaua!
 
Screenshot 2025-02-05 091022.png
Kiongozi Mkuu wa 49 wa Madhehebu ya Shia Ismailia na mwanzilishi wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN), Mtukufu Aga Khan, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88.

Mtukufu Aga Khan anayefahamika kama Karim Al-Hussaini Aga Khan IV, alifariki dunia jana Jumanne Februari 4, 2025, jijiji Lisbon, Ureno akiwa amezungukwa na familia yake.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kwa umma, baada ya kifo cha mfalme huyo, Imamu wa 50 wa madhehebu ya Shia Ismailia atatangazwa kurithi mikoba ya Aga Khan IV.

Enzi za uhai wake, Mtukufu Aga Khan alifahamika kutokana na mchango wake kwenye shughuli zinazochangia kuimarisha ustawi wa maisha ya binadamu katika maeneo mbalimbali ulimwenguni.

Mtukufu Aga Khan ameacha nembo isiyofutika maeneo mbalimbali duniani hususan nchini Kenya na Tanzania ambako alianzisha taasisi mbalimbali zilizoleta mchango mkubwa katika maisha ya raia wa nchi hiyo.

Uwepo wa Aga Khan nchini Tanzania unaonekana kupitia uanzishwaji wa kampuni mbalimbali ikiwemo ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Hospitali za Aga Khan na miradi mbalimbali katika sekta ya afya na elimu.
 
1. Tambaza
2. Azania
3. Jangwani
4. Zanaki


Zote hizi ni baadhi ya shule za Mtukufu Agha Khan
 
Kiongozi wa waislamia duniani ajulikanaye kama HH The Aga Khan amefariki dunia akiwa na Umri wa miaka 88.

Kwa Tanzania, Aga Khan atakumbukwa sana kwa kujenga miundo mbinu mizuri sana ya kutoa huduma za afya na elimu. Shule za Tambaza (Dar), Mkendo (Musoma), Mzizima (Tanga) ni baadhi ya shule zilizojengwa na Aga Khan Tanzania lakini pia alijenga mahospitali mengi sana karibu kila mkoa.

Mungu aipumzishe roho yake pema peponi
=============
A notice on the website of the Aga Khan Development Network - the development organisation he founded - announced his death, saying that he "passed away peacefully in Lisbon on 4 February 2025... surrounded by his family".

It said: "His Highness Prince Karim Al-Hussaini, Aga Khan IV, 49th hereditary Imam of the Shia Ismaili Muslims and direct descendant of the Prophet Muhammad (peace be upon him), passed away peacefully in Lisbon on 4 February 2025, aged 88, surrounded by his family.

View attachment 3225600
Fanya correction mstarinwakonwankwanza, ni Ismailia siyo "Islamia".
 
Jamaa alikuwa na uraia wa nchi tano.

United Kingdom
France
Switzerland
Portugal
Canada (Honorary)
 
Alizaliwa Switzerland na baadae akawa na uraia wa UK lakini makazi yake ya kudumu yalikuwa ni Monaco ambako kwa sababu za kikodi baadhi ya matajiri wengi huishi pale.

Alichukua taji hilo la kuongoza Washia akiwa na umri wa miaka 20 na hadi anafariki ameacha utajiri wenye thamani ya pauni bilioni 11.

Ameacha watoto wanne Princess Zahra, Prince Rahim, Prince Hussain na Prince Aly Muhammad pamoja na wajukuu wanne.

Prince Rahim ndie mkubwa akiwa na umri wa miaka 53 na ndie anetarajiwa kutangazwa kuchukua taji la baba yao. Rahim alizaliwa kwa mke wa kwanza mzungu mwingereza aitwae Sally Croker-Poole.

Mke wake wa pili pia alikua ni mzungu mwingereza ambae walioana mwaka 1988 na akamzalia mtoto mmoja na baada ya miaka sita wakaachana.

RIP.
Baada ya miaka 6 wakaachana
KATAA NDOA, NDOA NI UTAPELI HADI AGAKHAN IMEMSHINDA WAKAACHANA
 
Back
Top Bottom