TANZIA Aga Khan Afariki dunia akiwa na Miaka 88

Hongera sana Farasi ni moja kati ya wanyama napenda sana shida ni utunzaji wake ni wa gharama sana. ikikupendeza utumegee hizo tafiti za koo hizo za kifalme.
 
Mumesahau Serena hotels, Jubilee Insurance, Aga Khan universities Karachi, Nairobi , Dar na Arusha (U/C), Nationmedia, Farmers’ choice, Allpack industries ltd, Premier Foods Industries, pia IPS building alijenga yeye kabla Nyerere hajamnyang’anya!
 
Ukoo wake wa asili ni Uturuki, lakini walisambaa sana dunia nzima kuanzia Pakistani hadi ulaya huko Italy na Switzerland na hata Marekani na kanada.
Asili ya Bagamoyo na Pakistan/ Afghsnistan! Walihama huko kwavile Sunni walikuwa wanawaua!
 
Kiongozi Mkuu wa 49 wa Madhehebu ya Shia Ismailia na mwanzilishi wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN), Mtukufu Aga Khan, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88.

Mtukufu Aga Khan anayefahamika kama Karim Al-Hussaini Aga Khan IV, alifariki dunia jana Jumanne Februari 4, 2025, jijiji Lisbon, Ureno akiwa amezungukwa na familia yake.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kwa umma, baada ya kifo cha mfalme huyo, Imamu wa 50 wa madhehebu ya Shia Ismailia atatangazwa kurithi mikoba ya Aga Khan IV.

Enzi za uhai wake, Mtukufu Aga Khan alifahamika kutokana na mchango wake kwenye shughuli zinazochangia kuimarisha ustawi wa maisha ya binadamu katika maeneo mbalimbali ulimwenguni.

Mtukufu Aga Khan ameacha nembo isiyofutika maeneo mbalimbali duniani hususan nchini Kenya na Tanzania ambako alianzisha taasisi mbalimbali zilizoleta mchango mkubwa katika maisha ya raia wa nchi hiyo.

Uwepo wa Aga Khan nchini Tanzania unaonekana kupitia uanzishwaji wa kampuni mbalimbali ikiwemo ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Hospitali za Aga Khan na miradi mbalimbali katika sekta ya afya na elimu.
 
1. Tambaza
2. Azania
3. Jangwani
4. Zanaki


Zote hizi ni baadhi ya shule za Mtukufu Agha Khan
 
Fanya correction mstarinwakonwankwanza, ni Ismailia siyo "Islamia".
 
Jamaa alikuwa na uraia wa nchi tano.

United Kingdom
France
Switzerland
Portugal
Canada (Honorary)
 
Baada ya miaka 6 wakaachana
KATAA NDOA, NDOA NI UTAPELI HADI AGAKHAN IMEMSHINDA WAKAACHANA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…