Age-mates wangu waliojiingiza kwenye ndoa wamechoka, wanatia huruma. Mimi ambaye bado "napuyanga" naponda raha tu

upuuzi mtaacha lini
kenge blue



 


Mafanikio ni zaidi ya kuwa na mipango thabiti. Wapo waliokuwa hodari na wakafa maskini.
 
Nadhani ifike mahali waafrika tufungue akili kidogo.

Hivi ni LAZIMA kila mtu aoe/olewe?

Hivi ni LAZIMA kila mtu awe na watoto?

Kwani mtu hawezi kujiamulia mwenyewe aina ya maisha anayotaka kuishi, na sisi kama jamii tukaheshimu maamuzi hayo?

Nadhani matatizo mengi tunayoyaona leo kwenye ndoa yanatokana na watu kuhisi WANALAZIMIKA kuoa/olewa kwa sababu ya shinikizo kutoka kwa jamii.

Ni kweli ndoa ina umuhimu wake, lakini kama wanavyosema wazungu "Marriage is not for everybody".

Pengine kuna watu wangeishi maisha mazuri sana ya amani kama wasingekua kwenye ndoa, ila wanaishia kwenda kuteswa kwenye ndoa miaka nenda rudi, mwisho wengine wanauawa, wanapigwa, wanakufa kwa presha nk kisa jamii imeng'ang'ania kila mtu aolewe.
 
Endelea kufukuliwa kwa raha zako.
 
Aliolewa baada ya kila mwanamke aliyempata wakajikuta wote ni wanawake.
Wanawake walimkimbia.
 
Yupo mzee jirani yetu ana mitoto kama yote lkn yote imesambaa mikoa tofauti kutafuta maisha. Mzee anafanya kugongea msosi hapa home.

Kuzaa siyo kigezo kuwa uzeeni hutapata shida.
Mkuu swala hilo ni matokeo ya malezii mkuuu soo usijaji hivyo ,and bado ni bara kuliko ambaye aliyekula bata kipindi chake na wewe leo
 
Na siku ukiamua kuoa oa kimya kimya, usije siku ukatuunga kwenye group la Whatsapp ukitaka mchango wa harusi, hatutakuchangia hata mia
 
Jamaa kutongoza kazi. Anahitaji msaada.
 
Kwa sasa mwanamke unamtolea MAHARI unamuoa, cha ajabu anakuja kwako kufuata MALI (kama si kukuua kbsa)


Then anaendelea kuponda akiwa kwake na mikuyenge aitakayo nakujiita SUPER WOMAN.


Kwa ufupi wanawake wamehamishia magenge maduka na uharamia kwenye NDOA.
 
Ukiingia kwenye ndoa lazima ukutane na misukosuko,hii haikwepeki,lakini huwa ni ya muda tu na ukifanikiwa kuvumilia utafika mahali utasahau machungu yote,sasa wewe endelea tu kula raha,utakapofikwa na kiu ya kuoa utakuwa tayari umeshachelewa sana.Ndoa ni sakramenti ambayo kila binadamu anapaswa kuipitia,usishindane na nature mkuu......
 
Najua Umri wako ni kati ya 20 to 30
Kawaida sana hayo maneno tafuta interview za madam Rita umsikie
Maana halisi ya NDOA uanza ukishaanza kuinusa 40 ndo utaelewa kwann MUNGU alimpa Adam msaidizi ili aondoe upweke
Uko sahihi kabisa,umri wa 40 na kuendelea ni umri ambapo unaingia kwenye upweke,hapa watu wengi wanaachana na makundi na kila mtu anashikamana na familia yake,hapa ndipo kila mtu anashikilia kwa umakini shughuli za kiuchumi na kuacha makundi ya starehe,sasa utajikuta katika marafiki 20 uliokuwa nao wamebaki wawili au umebaki peke yako...
 
Finali uzeeni,mbuzi na mbwa hawana familia lakini uwa wanajivunia kuponda maisha
kwa sababu wanazeekea kwa anayewafuga,hivyo hawajali,kwa binadamu ni tofauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…