TANZIA Agnes Gerald ‘Masogange’ afariki dunia Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge, Dar

TANZIA Agnes Gerald ‘Masogange’ afariki dunia Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge, Dar

soon possible yule chizi wa Insta utasikia anasema eti ni mipango ya bashite ... ndo mtaamini kama dunia inawatu waliyelaniwa... R.I.P sister Agnes
 
Watanzania wenzangu, bila kuangalia dini ya mtu, leo naomba niwafunze kitu kimoja. Anapokufa mwanadamu yeyote yule inapaswa wewe ambae uko hai umuombee mwenzio Mungu amjaalie mafikio mema bila kuangalia alijuwa na amali gani anayoifanya. Maana yake ni kwamba huwezi kujua ni amali gani alikuwa anaifanya kwa siri marehemu huyo ambayo ilikuwa inampendeza Mungu na vile vile mwisho wake ni kiasi gani ulikuwa mwema au mbaya.
Tuombeane mema. Naanza mimi.
"Mungu amlaze mahali pema peponi, Amin"

*Maombi yako hayaongezi wala kupunguza kitu mbele za muumba, yeye pekee ndie ajuae amali za mja wake.


mnnnnhhhhhh leo umeokoka?
 
Wadau nilipita Mama Ngoma Health Centre Mwenge na kukuta watu wakilia kuuliza naambiwa Video Queen Masogange amefariki muda mfupi uliopita.


=========
UPDATES:
=========

Video queen maarufu Bongo Agness Gerald maarufu kama Agness Masogange amefariki Dunia leo katika Hospitali ya Mama Ngoma Mwenge jijini Dar Es Salaam.

Alikuwa anasumbuliwa na Homa ya matumbo pamoja na tatizo la kupungukiwa na damu.

Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.


Moja ya swala la haraka nililoweza tambua ni kua kulikua na "negligence" kwa upande wa wanafamilia na madoktar wa hiyo healthcare centre.

Tatizo la kupungukiwa na damu ni kubwa, na walikua nae tangu jana.

Wangempeleka Muhimbili, ndio sehemu yenye ICU za nguvu na uwezo mkubwa wa kudili na emergencies za haina hii.
 
ntakufaje ni swali la kila mmoja,mbele yako nyuma yetu.
 
Back
Top Bottom