Ahmed Ally atoa kauli kuhusu sakata la Yusuph Kagoma na Yanga SC

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mmesikia huko πŸ˜‚

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, ametumia ukurasa wake wa Instagram kuelezea kuhusu mchezaji wao, Yusuph Kagoma, na uvumi unaozunguka hatma yake.
Ahmed Ally ameandika:
"Klabu yenu inampenda sana Yusuph Kagoma, yaani kila mkilala mnamuota. Roho zinawauma kumkosa na mngetamani aje kwenu. Lakini cha kufanya kwa sasa ni kuwa na subira".
"Kwa sasa Kagoma ana umri wa miaka 23, na kwa uwezo wa Mungu (Insha Allah) atabaki Simba kwa miaka zaidi ya 10. Akiwa na miaka 33 au 35, hapo ndipo atakapokuja kwenu".

"Mfumo ni ule ule kama mlivyosubiri mchezaji kutoka Zambia kwa miaka 7 au mchezaji namba 20 kwa miaka 15. Hivyo Kagoma naye ni mali halali ya Simba kwa sasa."


Ahmed Ally amesisitiza kuwa Kagoma kwa sasa ni mchezaji wa Simba na mashabiki wa klabu nyingine wanatakiwa kuwa na subira, kwani nyota huyo bado ana muda mrefu ndani ya Simba SC.

Soma pia;


=> Sakata la Yusuph Kagoma kusaini timu mbili Klabu ya Simba kukatwa alama
=> Mwigulu awaomba viongozi wa Yanga wapotezee suala la Kagoma ili aweze kucheza Simba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…