Ahsante. Nani Angeamini Historia Niielezayo Kama Nisingeonyesha Ushahidi wa Picha?

Ahsante. Nani Angeamini Historia Niielezayo Kama Nisingeonyesha Ushahidi wa Picha?

Na mengi yaliyotokea huenda hatuyajui kwahio tutaendelea kuyapokea na kila mwenye la zaidi kuongezea na kila anyedhani hapa au pale hapako sawa kukosoa na kuelezea kilicho sawa ni kipi..., Ndio hivyo tutaendelea kupata version bora moja au versions tofauti na zote kuzielezea.. Kwahio msomaji akapata His or Her Story....

Sidhani kama nafasi imejaa ya kupata habari zaidi...
Logikos,
Baada ya kutoka kitabu cha Abdul Sykes mwaka wa 1998 wengi walishtushwa na niliyoandika.

Prof. Haroub Othman aliomba miadi na Mwalimu.

Alimwambia Mwalimu historia yake na ya uhuru wa Tanganyika imebadilishwa na kitabu changu.

Akamuomba na yeye aeleze upande wake ukweli ujulikane.

Nani huyu Abdulwahid Kleist Sykes?

Ilikuwaje Mwalimu hajamtaja popote katika maisha yake wala hayumo katika historia ya uhuru wa Tanganyika?

Prof. Haroub Othman mwalimu wangu ananieleza mazungumzo yake na Nyerere tumesimama nje ya Msikiti wa Ibadh.

Ilikuwa mwaka wa 1998.

Alitaka kusikia historia ya Abdul Sykes kutoka kwangu.

Nilimwambia akazungumze na Ahmed Rashaad Ali hawa walikuwa marafiki toka 1936 wakiwa wanafunzi shule ya msingi.
 
Back
Top Bottom