Ahsante Rais Samia, hatimaye HESLB wafuta VRF kwenye system yao

Ahsante Rais Samia, hatimaye HESLB wafuta VRF kwenye system yao

Siamini deni nililolikuta. Ni kubwa.
Nina hoja 2:
1. Kwa nini deni limetajwa kama "provisional loan balance"? Ninavyojua, provisional sio rasmi.

2. Kwa statement hii ", You are in service queue number 20156. Customer with service number 9400 Is currently being attended. Please continue to wait!!", je nipo kwa mstari wa huduma gani?
Naomba ufafanuzi kwa anaeelewa kadiri ya HESLB.
 
Sorry wadau.Hivi provisional loan balance ndio deni halisi lililobaki baada ya kufutwa kwa VRF?
 
Provisional loan balance ndo den halisi unalodaiwa, pia value retention fee pamoja na penalty vimeondolewa kidogo sana sijui kwanini bod hawataki kuviondoa kabisa?bado mzigo utakuwa mkubwa kwa wanufaika
 
Siamini deni nililolikuta. Ni kubwa.
Nina hoja 2:
1. Kwa nini deni limetajwa kama "provisional loan balance"? Ninavyojua, provisional sio rasmi.

2. Kwa statement hii ", You are in service queue number 20156. Customer with service number 9400 Is currently being attended. Please continue to wait!!", je nipo kwa mstari wa huduma gani?
Naomba ufafanuzi kwa anaeelewa kadiri ya HESLB.
Total charges ndio zinaongeza deni. Je hizi charges hawakuziweka kwenye salary slip wakati wanaanza kukata?
 
Nimejaribu sana kuingia kwenye hiyo website sifanikiwi sijui kwanini
 
Value retention fee imefutwa kias ,haijafutwa yote,naona bod wanataka waendelee kuwadidimiza wanufaika hawana huruma kabisa
 
Kama heslb wana nia nzuri wafute tozo zote ili den liweze kuwa himilivu kama den la taifa lilivyo ,bila hivyo wanufaika waandike maumivu,Pia sidhan kama wahusika wanastahili kuendelea kuwepo ofsin,kwa sababu wameshindwa kaz kabisa
Kabisa kiongozi,huenda sisi Waafrika tumetawaliwa na roho mbaya sana

Sent from my Nokia 2.4 using JamiiForums mobile app
 
Kama heslb wana nia nzuri wafute tozo zote ili den liweze kuwa himilivu kama den la taifa lilivyo ,bila hivyo wanufaika waandike maumivu,Pia sidhan kama wahusika wanastahili kuendelea kuwepo ofsin,kwa sababu wameshindwa kaz kabisa
Wanakata kiasi kidogo sana, wamenipunguzia 630,000/=
 
Wanakata kiasi kidogo sana, wamenipunguzia 630,000/=

Sijui wanaona wakipunguza watu watanufaika walikuwa wamezoea kuwaumiza watu sasa kitendo cha Mh Raisi kuamua kuondoa VRF ,watu wa loan board wameumia sana nafikiri kuna jinsi walivyokuwa wana nufaika na hizi tozo za ajabu ,sijui kwa nin hawataki kuwa wazalendo wakafuta hizo tozo na maisha yakaendelea
 
Kama tunavyojua, kwa mujiba wa katiba yetu Mheshimiwa Rais halazimiki kufuata ushauri wa mtu yeyote yule.

Hivyo basi tunapokuwa na rais msikivu tena anayefanyia kazi maoni na malalamiko ya watu wake ni baraka kubwa kwa taifa

Kwa sasa ukiangalia statement ya deni lako kwenye mfumo wa bodi ya mikopo (olas.heslb.go.tz ) utaona kuwa wameondoa tozo zote za VRF, yaani hata zile walizotoza zamani (kabla ya agizo la rais) wameziondoa

Wanufaika wa mikopo tunamshukuru sana Mheshimiwa rais kwa kusikia na kuyafanyia kazi maombi yetu. Tulilalamika sana wakati wa mwendazake lakini tukajibiwa kuwa 'hapangiwi'.

Sasa ni muda wa kila mnufaika mwenye uwezo wa kulipa na alipe, tena wamerahisisha unaweza kulipa hata kwa M-pesa na malipo yako yanaonekana hapohapo kwenye mfumo.

Pia niwakumbushe wadau, twendeni vizuri na mama, naiona katiba mpya hususani wakati wa ungwe yake ya pili Mungu akimjaalia na wananchi wakampa ridhaa.

---- update----
Wadau wengi wameuliza namna ya kuangalia, naamini bodi watatoa maelekezo zaidi lakini kwa hapo ngoja nieleze kwa ufupi.

Ingia kwenye website

View attachment 1830801

Kwenye dashboard (juu kushoto) chagua loan repayment
View attachment 1830804

Kisha baada ya apo, chagua beneficiary/lonee/ employee login

View attachment 1830805

Baada ya hapo ingiza namba yako ya form four kwa format inayo onekana

View attachment 1830806

System itaiangalia namba hiyo kwenye database ya bodi na kukuketea jina lako mnufaika.

Baada ya hapo utathibitisha kuwa ni jina lako kweli kwa ku click hilo jina.

Baada ya hapo utajaza taarifa muhimu kama namba ya simu, email na taarifa za mwajiri pamoja na kutengeneza password.

Ukikamilisha utakua umeshatengeneza account kwenye mfumo wao

Baada ya hapo uta log in as registered user na utaona taarifa zako zote za deni lako. Pia utaona control namba unayoweza kuitumia kulipa mwenyewe.

Natumaini inaeleweka.
NB sijaweka picha za hatua za mwisho kwakua zinaonesha taarifa binafsi za mnufaika.
Kinachogombewa na wapenda demokrasia si mtu afanye anavyo jisikia, bali atende kulingana na sheria. Katiba ingekuwa wazi shutuma kwa Magufuli zisingekuwepo, na kama angekaidi umauti ungemkuta mtaani au gerezani. Wala mh Samia asingepewa shukrani, kwani anatimiza wajibu wake.
 
Wanaogopa kurudisha hela kwa waliomaliza deni
Kama heslb wana nia nzuri wafute tozo zote ili den liweze kuwa himilivu kama den la taifa lilivyo ,bila hivyo wanufaika waandike maumivu,Pia sidhan kama wahusika wanastahili kuendelea kuwepo ofsin,kwa sababu wameshindwa kaz kabisa
 
Swala la kulinda thamani ya pesa lilitakiwa kuachwa na cha msingi ingepunguzwa asilimia........ yani ukope leo laki halafu baada ya miaka kumi ulipe laki hiyo hiyo? Aiseee

Waungwana riba kwao ni dhambi ndio maana ongezeko limetolewa mwanafunzi anafanya biashara gani ya uzalishaji wa hizo pesa ndani ya miaka mitatu?
 
Back
Top Bottom