Ahukumiwa miaka 30 jela kwa kumlawiti mke wake

Ahukumiwa miaka 30 jela kwa kumlawiti mke wake

Mahakimu wengi wa mikoani huwa hawatendi haki haki harta kidogo wanataka sifa eidha watapandishwa cheo au watapelekwa dar mfano
Mmama aliyekutwana nyama ya swala eti anatumikia kifungo miaka 20 kweli ‘huyo hakimu angekuwa nduguye angefanya hayo iliniuma sana
 
Mahakama ya Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Boniface Mtweve(28) mkazi wa kata ya Lugarawa kwa kosa la kumlawiti mke wake (27) ambaye jina lake limehifadhiwa.

Awali akisomewa shitaka hilo na mwendesha mashtaka Asifiwe Asajile mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Isaac Ayeng'o ilielezwa kuwa mwanamke huyo alienda kwenye harusi na kuchelewa kurudi nyumbani kwake ambapo aliporejea majira ya usiku alimkuta mumewe nje akimsubiri huku akiwa amekasirika.

Amesema kuwa mtuhumiwa huyo alimuamuru mkewe kuingia ndani na alipoingia akaanza kimfokea kuwa ametoka kwa wanaume na hakuwa kwenye harusi hivyo anataka amuoneshe kuwa yeye ni ndiye mwanaume ndani ya nyumba ambapo akachukua mafuta na kumfanyia kitendo hicho kitu ambacho ni kinyume cha sheria kifungu namba 154(1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.

Ameongeza kuwa kulipokucha mkewe alitoa taarifa kituo cha polisi na kisha mtuhumiwa alikamatwa na kufikishwa mahakamani ambapo alikana shitaka hilo lakini baada ya kufanyika uchunguzi na kutolewa ushahidi wa pande zote mbili mtuhumiwa alikutwa na hatia na katika utetezi wake aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwani ana watoto wadogo wanaomtegemea.

Kutokana na utetezi huo hakimu huyo aliyapokea maombolezo yake kisha kumhukumu kifungo hicho cha miaka 30 jela huku mwendesha mashtaka huyo Asifiwe Asajile akisema adhabu hiyo iwe fundisho kwa wale wote wenye tabia hizo kwani kitendo hicho ni cha kikatili na udhalilishaji.

View attachment 2869886
#WasafiDigital
Mke kabaki na mzigo wa kulea watoto peke yake.
Angekausha tu...maana mara moja haidhuru na inavumilika, japo si nzuri kiafya, huenda mke pia aliichoka ndoa, hivo alikuwa anatafuta pa kutokea.
(MSININUKUU VIBAYA.
NI MTAZAMO WANGU MIMI BINAFSI)
 
Mke kabaki na mzigo wa kulea watoto peke yake.
Angekausha tu...maana mara moja haidhuru na inavumilika, japo si nzuri kiafya, huenda mke pia aliichoka ndoa, hivo alikuwa anatafuta pa kutokea.
(MSININUKUU VIBAYA.
NI MTAZAMO WANGU MIMI BINAFSI)
Mke yuko sahihi.umaskini usikuvue utu wako
Hapo amemlawiti angekuja kumlawiti tena na tena from there angeanza dharau.hakuna mwanamke ambae amefanyiwa huo udhalimu akaishi vizuri na mume wake.kila siku wanaume wanataka tako jipya.akafie jela huko
 
Hapo ndo pale wanaposema Umeruka mkojo umekanyaga mavi... Mwanamke alifanya kwa hasiraa itakuwa hadi sasa haamini kaachiwa mzigo wa watoto apambane nao..!! Haina kukata rufaaa wala kupindishaa..[emoji16][emoji16][emoji16] kama mwana wangu flani alijaza kitumbo mwanafunzi tukamwambia torokaa akawaa anajichekeshaa oohoo mzahaa sio mzahaaa..
 
Back
Top Bottom