Ahukumiwa miaka 30 jela kwa kumlawiti mke wake

Ahukumiwa miaka 30 jela kwa kumlawiti mke wake

Mahakama ya Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Boniface Mtweve(28) mkazi wa kata ya Lugarawa kwa kosa la kumlawiti mke wake (27) ambaye jina lake limehifadhiwa.

Awali akisomewa shitaka hilo na mwendesha mashtaka Asifiwe Asajile mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Isaac Ayeng'o ilielezwa kuwa mwanamke huyo alienda kwenye harusi na kuchelewa kurudi nyumbani kwake ambapo aliporejea majira ya usiku alimkuta mumewe nje akimsubiri huku akiwa amekasirika.

Amesema kuwa mtuhumiwa huyo alimuamuru mkewe kuingia ndani na alipoingia akaanza kimfokea kuwa ametoka kwa wanaume na hakuwa kwenye harusi hivyo anataka amuoneshe kuwa yeye ni ndiye mwanaume ndani ya nyumba ambapo akachukua mafuta na kumfanyia kitendo hicho kitu ambacho ni kinyume cha sheria kifungu namba 154(1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.

Ameongeza kuwa kulipokucha mkewe alitoa taarifa kituo cha polisi na kisha mtuhumiwa alikamatwa na kufikishwa mahakamani ambapo alikana shitaka hilo lakini baada ya kufanyika uchunguzi na kutolewa ushahidi wa pande zote mbili mtuhumiwa alikutwa na hatia na katika utetezi wake aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwani ana watoto wadogo wanaomtegemea.

Kutokana na utetezi huo hakimu huyo aliyapokea maombolezo yake kisha kumhukumu kifungo hicho cha miaka 30 jela huku mwendesha mashtaka huyo Asifiwe Asajile akisema adhabu hiyo iwe fundisho kwa wale wote wenye tabia hizo kwani kitendo hicho ni cha kikatili na udhalilishaji.

View attachment 2869886
#WasafiDigital
Ogopa sana ukikutana na jina atufiwe au atufilwe,kijana alitaka kupeleka home michezo ya mjini!
 

1 Kor 6:9-11​

1 Kor 6:9-11 SUV​

Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi.
 
Hapo ndo pale wanaposema Umeruka mkojo umekanyaga mavi... Mwanamke alifanya kwa hasiraa itakuwa hadi sasa haamini kaachiwa mzigo wa watoto apambane nao..!! Haina kukata rufaaa wala kupindishaa..[emoji16][emoji16][emoji16] kama mwana wangu flani alijaza kitumbo mwanafunzi tukamwambia torokaa akawaa anajichekeshaa oohoo mzahaa sio mzahaaa..
Watoto watakua tu,Kuna watu wanafariki na watoto wanalelewa na mama,huwezi kuvunjiwa utu uendelee kumvumilia kisa watoto,,,,Sasa kichaa kama huyo anaweza hata kulea watoto?
 
Back
Top Bottom