Ahukumiwa miaka 7 jela Kwa kula nauli ya mwanaume!

kadiri kasimba

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2022
Posts
588
Reaction score
1,150
Mwanamke mmoja wa Nigeria amehukumiwa kifungo cha miaka 7 jela au kulipa kiasi cha 420,000 pesa za Nigeria kwa kosa la kula nauli ya mwanaume 30,000 ambayo alitumiwa na mwanaume Emmanuel kisha hakwenda kwa mwanamume huyo.

Mwanamke huyo alishtakiwa na mwanaume ambae alituma nauli hiyo kwa kusema alimtumia nauli mwanamke huyo lakini baada ya kutuma nauli mwanamke huyo hakuweza kwenda.

Mahakama imemkuta na hatia mwanamke huyo na kumfunga miaka 7 jela aidha amlipe Emmanuel N420,000πŸ˜‚πŸ™ŒπŸ»
 
Waingize hii subsection kwenye katiba yetu, maana nauli zinaliwa mno na hawa mademu wa kibongo.
Hiini fursa ya kibiashara. Unawatumia 30K wanawake 10 ambayo inakua laki 3. Kati ya hao sio chini ya wanawake 8 hawatakuja. Ukichukua 8 mara 420K inakuja 3360000. Ukitoa 300K ya mtaji, 60K ya kugharamia wale mademu wawili waliokuja, milioni 1 ya kumlipa wakili jumla 1360000. 3360000-1360000, umetengeneza faida ya milion 2 kirahisi kabisa
 
Tatizo ushahidi, siyo kila ukishtaki unashinda kesi kuna nyingine utashindwa na kutakiwa kulipa fidia kwa udhalilishaji.
 
Mamdogo Amehlo ungekuwa ushafungwa miaka saba saba mara ngapi?
 
Wanawake wa CHADEMA jiandaeni kwenda miaka saba jela

Wala sio siri nyie na huyo Mwanamke wa Nigeria mnafanana kula nauli tena huyo Mnigeria mtoto
 
basi tu πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€kuna raha hela ya kwanza unakula ya pili ndo unaenda
Uoni kwamba unamkwaza muhusika na hata akija kuwa na wewe hawezi kukuchukulia kwa namna nzuri
 
Asijishangaze.Alipe mtonyo wa gangwe kwa kumsababishia sonona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…