Aibu ya Barabara ya Mwendokasi Mbagala, inaanza kuzibwa viraka hata kabla ya kazi kuisha

Aibu ya Barabara ya Mwendokasi Mbagala, inaanza kuzibwa viraka hata kabla ya kazi kuisha

A

Anonymous

Guest
Leo, naomba kutoa dukuduku langu kuhusu hali ya barabara ya mwendokasi iliyojengwa kutokea Kariakoo Gerezani kuja Mbagala Rangi Tatu.

Kwa taarifa, barabara hii inakaribia kukamilika kwa asilimia 95, na majaribio ya kutoa huduma kwa wananchi yalifanyika hivi karibuni kwa takribani wiki 2.

Lakini kwa kusikitisha, barabara hii sasa inaonekana imeharibika kabla haijaanza kutumika, na inazibwa viraka kila mahali.

Hali hii ni aibu kwa serikali yetu, na inazua maswali kuhusu uaminifu wa mkandarasi na wasimamizi wa ujenzi.
IMG_20230810_075240_755.jpg
IMG_20230810_075239_992.jpg
 
Yale manguzo meupe kwenye vituo vya mwendokasi ndio yanawaaibisha zaidi.
 
Mkuu umeongeza usalama wa ID yako kwa kuwa anonymous.

Kama unaweza kupata picha, tupia hapa mkuu
 
Mkuu ni kero tupu, T1 kile kipande cha Mikumi national park, kimetengenezwa juzi kati, kimekamilika kikiwa na mabonde mengi tu, sasa kinarudiwa tena na mkandarasi yule yule na vimachine kama toy's, mlima wa kushukia Mikumi (T1),nao umeshaharibika within 3mths, tunafeli wapi kama nchi?,angalia mkeka wa Zambia (T2)umesimama mno kutoka pale nakonde hadi chinsali, sisi tunafeli vipi?wajenzi wote ni wachina, hawa wa kwetu wanatufelisha wapi?
 
Uaminifu wa Serikali pia uko mashakani. Humo ndio upigaji umo, matokeo yake kinachotengenezwa kinakuwa chini ya viwango, kinachukua muda mrefu kukamilika na si ajabu fungu la fedha lisitoshe.
 
mimi sidhani kama pale wanaziba viraka, kuna kitu cha kiuhandisi ambacho mimi na wewe hatukijui, maana wao wenyewe ndio wanachimba vimiraba kwenye barabara then wanaziba.

naamini kuna kitu cha chenye maana kwenye ulimwengu wa kiuhandisi ambacho sisi wengine hatukijui. ilikupasa ukaulize au utafute mtaalamu uulize kuliko kuja huku kuunda shutma.
 
Nadhani kama siyo wanafanya ukaguzi, basi kuna vitu vingine vya kiufundi wanafanya au (expansion joints 🤣🤣🤣) maana wanakata kisehem siyo kikubwa sana kama upana wa centimeter 10 labda na urefu wa Centimeter 50 au meter 1, wanaziba. Ila siyo kama ni wanaziba vilaka, haina ubovu huo kwa sasa
 
zNchi ngumu sn hii kweli ht mie nimeona inakatika au kupasuka af wanaziba tena ukiona seem wamezungushia mchanga af wameweka maji ujue hicho ni kiraka
 
Back
Top Bottom