Aibu ya Barabara ya Mwendokasi Mbagala, inaanza kuzibwa viraka hata kabla ya kazi kuisha

Ukiona Barabara imejengwa halafu inaanza kuwekwa viraka ujue kuwa ilijengwa chini ya kiwango.

Humo wanamo chimba ni kuwa mashine za uhakiki ubora zimeona mna kasoro za uimara. Ndio sababu ya kufanyiwa marekebisho.
Straburg naona wako vizuri katika ujenzi wa Barabara za mwendo kasi
 
Naomba kutoa ufafanuzi, mosi hakuna barabara inayozibwa viraka kabla haijaanza kutumika, mleta mada ungeweka angalau picha tungeweza kukusaidia kujua ni nini kinaendelea , kama ni yale maeneo pembeni ya vituo vinavyojengwa uliona wanakoroga cement na mchanga kwa ajili ya ujenzi wa vituo unaokamilishwa utakuwa uko very wrong , pia barabara kabla haijakabidhiwa inafanyiwa quality testing na ambapo pataonekana na mapungufu mkandarasi anarekebisha kwa maelekezo ya mwenye mradi, na kimsingi kazi ambayo imefanyika chini ya kiwango marekebisho anafanya mkanadarasi kwa gharama zake. Kwa mada hii hakuna uhalisia zaizi ya mleta mada kuleta mambo ya kufikirika na kusadikika kuliko uhalisia. Ukiwa na suala lolote la DART piga simu ya bure 0800110147 kwa ufafanuzi zaidi.

Kuhusu mabasi kutoenda Mbagala, ufafanuzi ulitolewa mapema.
 
Huo sio ukarabati hiyo picha ya kwanza ni eneo walikua wanachanganya cement kwa ajili ya ujenzi unaoendelea kwenye kituo pembeni hapo na hiyo picha ya pili inaonekana dhahiri ni mchanga umemwagika kutoka kwenye lori la mkandarasi, tuwe wakweli na kuacha kuleta taharuki kwenye masuala ya msingi, pita leo utuletee ushahidi wa kina kwamba zege imevunjwa na inajengwa upya. Barabara ikishasafishwa kabla ya kukabidhiwa utaona upotoshaji ulioleta.
 
Watasingizia mchanga hauna ubora
 
Halafu si mkandarasi huyu huyu kapewa na tenda ya gongo la mboto?
 
Hawajaanza leo, walianza kwa kukata vipande na sasa wanaipiga ribiti ili iwe ngumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…