Uchaguzi 2020 Aidah Kenani (CHADEMA) wa Nkasi Kaskazini amuangusha bwana Ally Kessy (CCM)

Uchaguzi 2020 Aidah Kenani (CHADEMA) wa Nkasi Kaskazini amuangusha bwana Ally Kessy (CCM)

Hawakusahau wameanza kujistukia.
Wanampango wa kupitisha kama 3 hivi tena wanyonge na wasiokuwa na majina kama geresha ya kuhalalisha wizi wao.

Ghiliba hizo.

Ilikuwa la kheri mno kuwasusia Mi-CCM bunge lao hili la wizi.

Aluta continua
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Tulionya humu kwamba chadema ikipata wabunge 10 mwka huu mkatambike, ndio hao sasa.
 
Namhurumia huyo dada kahela kake ka viposho kina Msigwa watakagombania kwa kupiga mizinga.
 
Huyu Ally Kessy ana kiherehere, nafikiri ni mkakati wa Chama kumuondoa bungeni. Haiwezekani hata kidogo mbunge wa CCM kushindwa kwa namna mambo yalivyo majimboni mwaka huu. Kessy hatakiwi aingie bungeni mara hii ndio maana kapigwa chini.
 
Hiyo ilipangwa na CCM pia maana hawakuwa wanamtaka Ally Mabodi a.k.a Kessy
 
Ally Kessy kafelishwa makusudi, anashindaje mtu wa CHADEMA?.

Kuna hujuma hapo...
 
Napata hisia huu ni mpango maalum ulioandaliwa na system ili kuonesha wapinzani walikua na nafasi ya kushinda sema wananchi ndio wamewakataa
 
Eti Kessy kadondoshwa[emoji15]!

Yaani yule Kessy aliyekuwa anapiga kelele bungeni meko aongezewe muda!?

Hayo ni maigizo na maagizo kutoka remote centre!

Hilo ni chenga la macho ili ionekane zoezi limekuwa fair! Utasikia meko anavuojua kunanga atasema "kama uchaguzi haukuwa huru na haki mbona huyu mpinzani alitangazwa?"

Huu ni mchezo umechezwa na tiaises kwa maelekezo maalum, then hakutakuwa na kitu cha kushangaza huyo Kessy akija akiteuliwa kuwa mbunge!
Atapewa ukuu wa mkoa.
 
CHADEMA watumie ile mbinu yao ya kufunga midomo kwa plasta za kugangia vidonda tuone kama itafanya kazi huku mtaani aka kitaa.

Bunge litapa heshima yake baada ya wahuni wa chama cha wahuni kupigwa chini. Historia imejirudia Watanzania tangu mwaka 1992 waliukataa mfumo vyama vingi. Mwl. Nyerere akatulazimishia kupitia zidimu fikra. Matokeo ya uchaguzi 2020 yameonesha Watanzania hawautaki mfumo wa damokrasia ya vyama vingi.

Ukiaangalia asilimia ya kura alizopata Rais JPM dhidi ya wapinzani ni kubwa sana. Inaakisi zile ambazo Mwl Nyerere na Mzee Mwinyi walikuwa wa kizipata wakishindana na kivuli.

Safari hii upinzani kwa sababu ya kuendekeza siasa za hovyo hovyo wamegeuka kuwa kivuli chenye uhai.
 
Hongera kwa huyo mama kushinda Hilo Jimbo yawezekana wananchi wamemuona yupo vizuri zaidi anaweza kuwaletea maendeleo yao.
 
Back
Top Bottom