Uchaguzi 2020 Aidah Kenani (CHADEMA) wa Nkasi Kaskazini amuangusha bwana Ally Kessy (CCM)

Hawakusahau wameanza kujistukia.
Wanampango wa kupitisha kama 3 hivi tena wanyonge na wasiokuwa na majina kama geresha ya kuhalalisha wizi wao.

Ghiliba hizo.

Ilikuwa la kheri mno kuwasusia Mi-CCM bunge lao hili la wizi.

Aluta continua
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Tulionya humu kwamba chadema ikipata wabunge 10 mwka huu mkatambike, ndio hao sasa.
 
Namhurumia huyo dada kahela kake ka viposho kina Msigwa watakagombania kwa kupiga mizinga.
 
Namuombea huyu dada apewe usirikiano na CHADEMA, laa sivyo atakuwa na wakati mgumu sana bungeni. Kutimiza majukumu yake ya kibunge na kufuata matakwa/masharti ya Chama.
Akale bata tu
 
Huyu Ally Kessy ana kiherehere, nafikiri ni mkakati wa Chama kumuondoa bungeni. Haiwezekani hata kidogo mbunge wa CCM kushindwa kwa namna mambo yalivyo majimboni mwaka huu. Kessy hatakiwi aingie bungeni mara hii ndio maana kapigwa chini.
 
Hiyo ilipangwa na CCM pia maana hawakuwa wanamtaka Ally Mabodi a.k.a Kessy
 
Ally Kessy kafelishwa makusudi, anashindaje mtu wa CHADEMA?.

Kuna hujuma hapo...
 
Napata hisia huu ni mpango maalum ulioandaliwa na system ili kuonesha wapinzani walikua na nafasi ya kushinda sema wananchi ndio wamewakataa
 
Atapewa ukuu wa mkoa.
 
CHADEMA watumie ile mbinu yao ya kufunga midomo kwa plasta za kugangia vidonda tuone kama itafanya kazi huku mtaani aka kitaa.

Bunge litapa heshima yake baada ya wahuni wa chama cha wahuni kupigwa chini. Historia imejirudia Watanzania tangu mwaka 1992 waliukataa mfumo vyama vingi. Mwl. Nyerere akatulazimishia kupitia zidimu fikra. Matokeo ya uchaguzi 2020 yameonesha Watanzania hawautaki mfumo wa damokrasia ya vyama vingi.

Ukiaangalia asilimia ya kura alizopata Rais JPM dhidi ya wapinzani ni kubwa sana. Inaakisi zile ambazo Mwl Nyerere na Mzee Mwinyi walikuwa wa kizipata wakishindana na kivuli.

Safari hii upinzani kwa sababu ya kuendekeza siasa za hovyo hovyo wamegeuka kuwa kivuli chenye uhai.
 
Hongera kwa huyo mama kushinda Hilo Jimbo yawezekana wananchi wamemuona yupo vizuri zaidi anaweza kuwaletea maendeleo yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…