Ego is the Enemy
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 8,201
- 16,246
Mkuu mzungu anaumiza saana kichwa sie huku acha tuwaze vumbi la kongo na kula tunda kimasihara.yaani sie twapenda Mambo ya kuburudisha ubongo Ila sio vya kuumiza ubongo.Yaani wamekuja empty handed, kwa kuwa ngozi yao ni nyeupe, mabenki matano yameungana na kuwaamini kuwakopesha ilihali mabenko hayo hayo hayawezi kuwaamini locals wenye mali zisizohamishika wakawakopesha kiasi hicho cha pesa.
Na kuna mijitu inashangilia eti tz imepata mwekezaji
Na kufanya tafiti.
Ivi unajua ukienda bank na idea yako ambayo ni viable wanakupa hela ama hulijui.
Acha tu nikudokezee kidogo Kama wajua pamba sec ya hapa mwanza Kuna msela aliona fursa kuwa fremu zijengwe kuzunguka hiyo shule.
Akaongea na mamlaka husika wakubali idea yake.
Akazama benk akawaelezea akawapa makubaliano so bank wakatoa hela wakajenga frames so makatano Yao wanajua wenyewe.
Banks ni sehemu ambayo watu tunatunzia pesa zetu Mana hatuna mawazo gani tuzifanyie.
Na benki hizohizo ni sehemu ambayo watu wanaenda kuchukua hela ambao Wana mawazo ya kuwa watazifanyia Nini. We're linked together by banks.
Ila lazima uwe na kitu Sasa ,eti wazo unashindwa angalau uthubutu Sasa hata angaalau uonekane.
Nipo radhi nimuongezee mtaji mama muuza karanga na matunda road kuliko mdogo wangu amelala eti bro mtaji.chacharika piga vibarua pata ya kwako mfukoni fungua kitu uelemewe nikuone Sasa ulipopungukiwa.