AIM Global, Qnet, Forever Living, One Coin, GNLD na wengine mbadili mbinu za utapeli, hii ya utajiri ndani ya siku 2 imepitwa na wakati

AIM Global, Qnet, Forever Living, One Coin, GNLD na wengine mbadili mbinu za utapeli, hii ya utajiri ndani ya siku 2 imepitwa na wakati

Sikujiunga nao lakini walinikosakosa washenzi wale ikanibidi kuigiza ufukara uliopitiliza wakaanza kunishauri niingie benki nikope nipate hiyo milion 4 niweze kujiunga kwenye fursa nikawashitukia ikafika kipindi nikawaambia kua nataka kwenda kusoma wao wakadai kusoma ni kupoteza muda kama naweza ninunue kifurushi cha elimu ambacho nitasoma through e- learning katika moja ya vyuo vyao huku nikiendelea kukusanya dola 200 kama commission ya kuwa kwenye fursa.

Wakajigamba kuwa wamearchive a lot of things ikiwemo magari na majumba ya kifahari hadi ikafikia hatua ya kuniambia niache kazi yangu kwa kua hata wao walikua waajiriwa wapo waliojitambulisha kuwa walikua marubani, madaktari na kazi nyingi ambazo ni white color jobs ila waliziacha baada ya kuona fursa iliyopo Q-NET.

Kilichonishangaza ni wengi wao walionesha sura za majonzi na hali ya kupigwa na maisha nikagundua hata tabasamu walilioonesha lilikuwa fake. Walionesha maigizo ya hali ya juu ya kuitana mabilionea mimi nikaona ni ujinga kufata mkumbo japo walifanikiwa kuwanasa rafiki zangu wawili. Nikaamua kuachana nao nipo zangu chuo napalilia kamshahara kangu nikimaliza nije nivute pesa benki niendeleze miladi yangu.

Haya mambo ya kusalimiwa GOOD MORNING saa tisa alasiri halafu tukaitikia yatatupeleka kubaya. Top gainers ni waanzilishi pesa inayopatikana inakuja kwako kama chenji wenye kupata tayari wanakuwa wameshajipatia. Tuweni makini hawa siyo watu wema. Jiulize kwa roho zetu sisi Watanzania nani atatamani ufanikiwe wakati hauna undugu naye? Kama ni kusaidiana ili tuwe na maisha bora na kuoneana huruma kwa nini hiyo pesa wanayoomba utoe ili ujiunge nao wasikutolee wao kwa maana ya kuinuana? STAY SAFE HAWA NI MATAPELI KAMA WALIVYO MATAPELI WENGINE.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Juzi mmoja kanitext PM Instagram, blaa blaa na inshu ya business kibao anatokea mult Aloe vera nikasema safi, nikamwambia nipe maelekezo ya kazi tupige pesa, mara anaanza kutuma video, zao blaa blaa tupu.

Nikamwambia kuwa serious na unacho fanya, so video ndio nitakuwa nauliza maswali, hajanijibu hadi Leo
 
Q-net muda huu saa nne na robo usiku huu wanasalimiana Good morning kwa vidole viwili, kuna jirani yangu nimeshuhudia kwa macho yangu alienda mpaka benk kukopa 5M akawapelekea, alinishawishi nikamwangaliaaaaa.... hahaaaa, nikamwambia ahsante sana, siku hizi aniongeleshi, eti anashindia huko ofisini kwao mpaka saa nne usiku.

mara wameaidiwa Iphone mara Toyota, kuna Mama mmoja n mstaafu alishapeleka 5M kwa hao jamaa sasa hivi anazunguka eti kutafuta partners wengine, basi nilimkuta anamshawishi mzee mmoja hivi ninaemfaham kabisa. Pale pale nikamchana live yule Mama akaniambia we kijana hujui kitu, nikamwambia sawa Mama kama sijui kitu mbona tokea uweke hiyo 5M umekuwa ni mtu wa kuzunguka tu hutulii kwako mwishowe upate maradhi bure, hujatajirika na hiyo Toyota na Iphone mbona hawajakupa eti si ndo nipo natafta Partner ili akaunti yake ijae,

Nikaendelea kumwambia kwamba hakuna pesa zinazokuja kwa haraka hivyo isitoshe wewe umeishastaafu hukutakiwa kuanza kuzunguka na kuhangaika hivi mara huku mara kule eti unatafta Partner wa Q-net, halafu hao Q-net wanakmwabia wanafahamika mpaka Serikalini wanakuonyesha picha walizopiga na viongozi wa Serikalini, mimi nilimuambia huyu aliyetaka kunishawishi kwamba picha zina-editiwa ndugu kuwa makini, nimeona mengi mpaka watumishi ninao wafaham wamecha kazi nao wanaangaika kutafuta Partners.. inahuzunisha sana Serikali inabidi iangilie kwa jicho pana zaidi kuhusu hawa Q-net et all.

Sent from Nokia 7 Plus
 
Dola 200@pp!😄😄!
Juzi walinisumbuaaa...ikabidi na mm niwaletee mahesabu yangu ..mishe nazofanya..wakabaki kusema sawa madame lakini toka huko bwana njoo mjini tupige hela..nikasema mbona unachoingiza mie naingiza zaidi yako mkuu? Wakabaki oh mwanamke unakaa migodini toka huko bwana😄😄!
Hyo dola 200 had umpate mtu alipie hyo 4m ni.leo?? Upuuzi tu
Kuna mmoja Tanga, nilimuambia anipe bank statement yake yenye flow ya mil 100 tu kwa mwaka, hata mil 3 hajawahi ingiza kwa mkupuo.........mil 100 miaka 3 hawezi fikisha.... atanshawishi bil 1 eti!!!!!!!

Maana ana miaka 3 hapa Sinza anadai nikinunua SAA mil 5 na kuita watu, Basi business plan ya bilioni moja kwa mwaka napata..

Muda wa kuondoka naona anadandia lift, halafu ndio miaka 3 yote kakaa huko na kiongozi


Jamani life sio kamari
 
mm nilishawishiwaga sana kujiunga forever , kila aliyenishauri nilimwambia anilipie kiingilio tukianza piga hela nitamrudishia wote wakakimbia
Kuna mmoja aliniambia ntaingiza mil 2 kwa wiki nkipambana .... yeye ana 2 yrs huko. Kumbe hata nauli elf 10 tu anakopaga kwenye Tigopesa yangu akirud anampa kijana.....

full suti na daladala, jua Kali hili .,.wengi kama machinga tu......mfano wao Blandina Njau ndio kafanikiwa, kila siku huyo ndio stori
 
Huku kuna jamaa yangu kaacha Kazi serikalini uko _Qnet, eti nae ni mkurugenzi wa kampuni kiingiliyo mil. 5 kasharubuni wadau wengi,
Huu ni ushauri wa bure.

Haya makampuni ya fursa hebu wajitahidi kubadili mbinu za kutapeli watu. Hii ya kutajirika ndani ya siku 2 imepitwa na wakati.

Qnet acheni kukodi magari ya watu na kujifanya ni yenu. Na visimu vya Iphone 6 Iphone 8. Badilini mbinu basi.

Kupiga picha na selfie kwenye magari ya watu na haina maana. Huu ni utapeli wa kitoto. Jitahidini kua wabunifu.

Nina hasira baada ya mtu ninaemheshimu juzi kunipeleka kwenye seminar ya mambo ya kipumbavu.

Hovyo kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah hao watu wanaboa kinyama, mimi kuna kipindi ndugu yangu mmoja alinisumbua kweli yaan na ni mwanafunzi wa chuo, siku naenda huko maeneo ya mikochen ananiona sijatupia official anaanza kuniambia kuwa huku unatakiwa kuwa umepiga pamba. Nikataka kugeuza akanishawish tena nikaingia nikakutana na watu wamejigawa kwenye jengo humo kila mtu yuko busy mara naanza kusalimiwa GOOD MORNING na n saa 03:..pm

Yan mpaka nikaanza kuchanganyikiwa kuona kama hawa watu wako serious au wananitania,wakaja kunipigia promo za biashara yao weee kila nikiwasikiliza wanalazimisha kuwa nitapata faida sasa na mimi nikawa najiuliza mbona wao hawataji faida wanayoipata kutoka kwangu?

Wako busy na madoc.. Kibao mpaka naondoka nilikua nishasalimiwa goodmorning za kutosha na ni jioni. Mpaka leo namfatiliaga huyu ndugu yangu niome mabadiliko aliyo nayo lakin naona hamna kitu sasa sijui hiuo Qnet imeathirika na covid au vp?
 
Huu ni ushauri wa bure.

Haya makampuni ya fursa hebu wajitahidi kubadili mbinu za kutapeli watu. Hii ya kutajirika ndani ya siku 2 imepitwa na wakati.

Qnet acheni kukodi magari ya watu na kujifanya ni yenu. Na visimu vya Iphone 6 Iphone 8. Badilini mbinu basi.

Kupiga picha na selfie kwenye magari ya watu na haina maana. Huu ni utapeli wa kitoto. Jitahidini kua wabunifu.

Nina hasira baada ya mtu ninaemheshimu juzi kunipeleka kwenye seminar ya mambo ya kipumbavu.

Hovyo kabisa.
Hahahahahah, noma sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm aiseeeee ilibaki kidogo tu nidakwe na hawa wahuni wa QNET, nilichukuliwa na mfanyakazi mwenzangu, ile nafika tu mle ilikuwa jioni ya saa 10 nasikia good morning, sasa nikaanza kushangaza, huyu mfanyakazi mwenzangu ni msomi wa kiwango cha master's na mle ndani kuna wasomi wengi tu ninao wafahamu, inakuaje hivyo, nikapiga moyo konde, baadae tukaingia chumba kimoja, mm na yule dada mwenyeji wangu, kisha akaja dada mmoja kutambulisha mambo na kile wanachofanya, akaondoka akaja dada mwingine kwa ajili ya wasilisho la kwanza, daaaaaah baada ya hapo tuliagana nikaalikwa wasilisho la pili. Jambo la kushangaza mpaka nikashituka ni nguvu kubwa ya ushawishi iliyokuwa inatumika kunishawishi nianze biashara tena kwa kunishawishi mpaka nikope pesa kwa watu kwa madai ya kwamba inarudi ndani ya wiki [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] mwisho niliwaona mafala tu na kuwapotezea mpaka leo hawaamini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anae jua kuusu Aim global atujuze kiundani , maana si kusumbuliwa.
Huu ni ushauri wa bure.

Haya makampuni ya fursa hebu wajitahidi kubadili mbinu za kutapeli watu. Hii ya kutajirika ndani ya siku 2 imepitwa na wakati.

Qnet acheni kukodi magari ya watu na kujifanya ni yenu. Na visimu vya Iphone 6 Iphone 8. Badilini mbinu basi.

Kupiga picha na selfie kwenye magari ya watu na haina maana. Huu ni utapeli wa kitoto. Jitahidini kua wabunifu.

Nina hasira baada ya mtu ninaemheshimu juzi kunipeleka kwenye seminar ya mambo ya kipumbavu.

Hovyo kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hivi kuna hawa wanajiita CROWD 1, juzi Aunt yangu aliniita akaniambia twende kwenye semina nzuri sana ya kuuaga umasikini

Kwenda nikaisikia hiyo Crowd one, Mara watutajie sijui nani amepata Billion 3, nikiwatazama wanavyoisifia na hali zao zilivyo ni vitu viwili tofauti kabisa

Tena hela ya kujiunga walinitajia 270K tu

Wote Hawa ni chengachenga tu



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeangalia michango ya mawazo ya watu humu ndani inasikitisha kweli,kila mtu kasimulia matukio tu lakini hakuna mtu aliye kuja na simulizi la uzoefu katika moja ya hizo network marketing.Ni kweli zipo unprofessional and illegal scheme ambazo zinawahadaa watu ili kuwarubuni but siyo zote.Hiyo Qnet mnayoiponda as if ipo kwa lengo la kuwaibia watu naweza kusema ni a big NO maana nina jamaa zangu watatu wanapiga kazi sana na huu ni mwaka wa tatu nawaona wanapata exposure ya kwenda nje huko Malaysia kwaajili ya mikutano ya kupeana mbinu na uzoefu wa biashara,kikubwa hapa siyo kuingia fursa halafu unabaki unabweteka na shemejiyo nyumbani ukiamini umetapeliwa badala ya wewe nawe kufanya network marketing ili kile ulichokiwekeza kiweze kurudi na mwisho wa siku uendelee kunufaika na hiyo fursa kwa kufanya kazi.Hapa kazi tu !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom