Air Tanzania yapigwa Marufuku kufanya safari zake Katika nchi 28 za Umoja wa Ulaya kwasababu za Kiusalama

ni ujinga kupingana na ukweli kwa sababu kupinga hakufanya uongo kuwa kweli. Ndiyo maana kuna mashirika ya kusimamia usafiri wa anga. Timiza masharti iweze kuingia kama huwezi kaa huko.
Umejua ni masharti gani ATCL haija-comply? Au wewe ukisikia beberu amesema basi ni 100% wako sawa hujui kuwa hapa duniani kuna figisu nyingi sana. Bwana mdogo kuwa uyaone!!
 
Mnapewa funzo bado hamuelewi na wala hamjifunzi kitu ndani yake?

Fanya uswahili nyumbani kwako, usiupeleke kwingineko.
Kama huna viwango na hufuati taratibu zilizopo, unataka watu washushe viwango kwa ajili yako?

Hovyo Kabisa.

Kuna mengi ya kuwalalamikia wakoloni hao; lakini kuna upuuzi usio vumilika kwenye nchi za hovyo kama hii yetu sasa hivi.
 
Naona hapo kuna kiwingu cha kisiasa tu. Ndege zote za ATCL zinazosafiri masafa marefu ni mpya sana kuliko baadhi ya ndege za mashirika ya Ulaya, na zimetengezwa na makampuni yanayoaminika sana Ulaya,yaani Boeing na Airbus. Kwa tuhuma hizo za kutokuwa ndege salama inabidi ATCL wawashitaki watengezajiowa ndege hizo (Boeing na Airbus) kama waliwauzia ndege zisizokuwa salama huko Ulaya; yaani mzigo huo wawatwishe washirika wao.
 
Ujinga ni mzigo!

Kusoma hujui au lugha ni tatizo wewe kunguni wa mama Abdul?

Umeambiwa wamezuiwa bada ya kushindwa kufika viwango vya kimataifa vya usalama wa anga sasa vyombo vinayodhibiti ubora wa viwango hivyo ulaya huko vinamilikiwa na upinzani?
 
Air Tanzania imeshatua sana tu hapo Heathrow siku za nyuma.
 
Inatakiwa sasa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) Eng. Peter Ulanga ajitokeze haraka kuelezea kadhia hii ya hatari kwa usalama wa abiria watakaotumia ndege katika anga la nyumbani, pia kwenda Dubai, India na China usalama upo vipi.
 
Umoja wa Ulaya (EU) umetangaza kuzuia ndege za shirika la ndege la Air Tanzania kuingia katika anga la nchi wanachama wake, jumla ya nchi 28, kwa madai kuwa shirika hilo halijakidhi vigezo vya kimataifa vya usalama wa anga.
 
ATCL zinazosafiri masafa marefu ni mpya sana kuliko baadhi ya ndege za mashirika ya Ulaya

Air Tanzania wasifanye mzaha maana pamoja na mamia ya abiria kutumia ndege za ATC pia Rais hutumia huduma hizo katika ziara kibao, mfano juzi juzi Kwenda Rio de Janeiro Brazil, China n.k

President of Tanzania, Samia Suluhu Hassan - G20 Rio De Janeiro Brazil

View: https://m.youtube.com/watch?v=mDBuSC9It0g
 
Kwani ina route za huko au ni ile ya akina Mengele?😂
Zipo route za kwenda huko hasa kwa viongozi wetu wakuu. Na ikimbukwe moja ya mikakati ya Tanzania ni kuhakikisha shirika hili linabeba watalii moja kwa moja toka nchi za ulaya na kwingineko duniani na kuwatua nchi kwetu kutembelea vivutio mbalimbali. Wazungu hawakubali kupigwa pesa yao mara mbili.

Kama kuna mambo ya kurekebisha ili kukidhi viwango vya Ulaya ni sawa yafanywe.
 
Kwanza hatuna route za huko
 
Kwa udogo wa ubongo wako ulitakiwa kuhurumiwa lakini wengi watakucheka. Air Tanzania inaweza kuwa tishio kwa nani? Hii ambayo nina uhakika miaka 10 ijayo haitakuwepo au itakuwa imekabidhiwa kwa mwarabu?
Eti nina uhakika,kwani uhakika wako wewe unatusaidia nini sisi,wewe ni Mungu,ulijua leo TZ ingekuwa na treni ya SGR au ulijua kuwa hilo shirika lako la ATCL lingeweza kumilike ndege zake lenyewe tena mpya zaidi ya 7,acha kuishi maisha ya kusadikika ya kufikiri kuwa mtu mweusi hawezi fanya miujiza...
 
Air Tanzania imeshatua sana tu hapo Heathrow siku za nyuma.
Hiyo ilikuwa miaka ya 70 na 80 nakumbuka sana
Enzi hizo tulikuwa na uzalendo haswa boss
Hata Somali Airlines ilikuwa inakuja Tz na kulikuwa na ndege nyingi zinatua Dar na kuondokea Dar kuja nje
Nimepandia huko Air France, Lufthansa, SwissAir hizo nimepanda na kuja nazo nje miaka ya nyuma sana ikiwamo na ndege zetu pia
Je tumepatwa na nini leo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…